KENYA: Mchungaji achomwa moto na Wananchi kwa kosa la Kumlawiti Mtoto

KENYA: Mchungaji achomwa moto na Wananchi kwa kosa la Kumlawiti Mtoto

Mhaya

JF-Expert Member
Joined
Aug 20, 2023
Posts
2,818
Reaction score
7,940
Mchungaji huko Nyeri anayeshutumiwa kumbaka mvulana wa miaka tisa ameuliwa na wanakijiji wenye hasira.

Simon Ndegwa, ambaye alikuwa mchungaji katika kanisa la True Disciple Ministry na anayefahamika vizuri na familia ya mvulana huyo, anashukiwa kufanya kitendo hicho cha kinyama kwa wavulana wadogo mara kwa mara.

Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi wa Kaunti Ndogo ya Nyeri Kati, Andrew Mbogo, polisi walifika eneo la tukio baada ya umati tayari kumchoma mshukiwa moto.

Taarifa za awali zilizokusanywa na polisi kutoka kwa wakazi zinaonyesha kuwa hii ilikuwa mara ya nne mshukiwa huyo akishtakiwa kwa makosa ya ulawiti.

Polisi wanasema mvulana huyo alidaiwa kutumwa dukani ndipo alipokamatwa na mshukiwa, ambaye alimvuta hadi nyumbani kwake, ambako anadaiwa kumbaka kabla ya kumruhusu kurudi nyumbani.

Mvulana huyo aliwajulisha wazazi wake, ambao walitoa taarifa kwa majirani, waliomchukulia hatua mchungaji huyo kwa kumpiga hadi kumuua.

Mvulana huyo anapata matibabu katika hospitali ya eneo hilo.

Screenshot 2025-06-03 212401.png
 
Tulikofikia ni pabaya sana.. Hawa viongoz wa kiiman ambao walitakiwa wawe mfano wa kuigwa kukemea dhambi na vitendo viovu ndo wamekuwa wafanyaj wenyew!
 
Usawa huu bado ulawiti unashamiri kwa nini? Mashoga wako wazi wazi na wamejaa telee, kwanini wasifwatwe hao, wanakimbilia kuharibu watoto wasio na hatia?

Inaumiza mnoo, madhara ya kupinga ushoga, ndo matokeo yake haya ulawitii. Lol
 
Wavimba macho hapa huwezi kuwasikia wakizungumzia dini yake.Ingekuwa ni ......... Iam just thinking loudly!
 
Back
Top Bottom