Kenya: Mwanamke akamatwa kwa kuishi na wanaume wake wawili ndani ya nyumba moja

Kenya: Mwanamke akamatwa kwa kuishi na wanaume wake wawili ndani ya nyumba moja

‪Maurine Atieno wa Kenya amekamatwa na Polisi nchini humo baada ya kuonekana akiishi na Waume wawili Robert Ochieng na John Ochola ndani ya nyumba moja, inaelezwa Maurine amekuwa akiishi na Waume wake hao ambao pia wamekamatwa ndani ya nyumba 1 kwa wiki 2 sasa.

Mwanamke huyo amekamatwa baada ya majirani kulalamika na kutaka mamlaka husika kumchukulia hatua wakidai kitendo hiko sio sahihi.

Chifu wa eneo hilo David Onyango amesema kwamba mwanamke huyo amekuwa akiishi na waume hao wawili kwa pamoja kama waume zake wa ndoa, kwa muda wa wiki mbili sasa ndani ya nyumba moja.

Ndoa hiyo ya mitala kwa wanaume hao ilitokea pale baada ya Maurine ambaye aliolewa na Robert Ochieng ambaye pia amezaaa naye watoto wawili, kurudi nyumbani akiwa na mpenzi mpya aliyetambulika kwa jina la John Ochola aliyempata kwenye shughuli zake za kuuza samaki huku akimtaja kuwa mteja wake muaminifu, na kuamua kuishi nao wote kwa pamoja.

Chifu huyo ameendelea kwa kusema kwamba wanachunguza ni kwa namna gani watatu hao wamekubaliana kuishi ndani ya nyumba moja, na kwamba ndoa hiyo ya pili ya Maurine na John imethibitishwa na mama wa John ambaye amekiri na kusema kwamba mkwe wao huyo huwa anaenda mara kwa mara kuwatembelea nyumbani kwao.

Hata hivyo uongozi wa kijiji umesema kwamba hakuna sheria ambayo inaweza kutumika kuwashtaki, isipokuwa wataangalia namna ya kuwatenganisha watatu hao, ili kuepusha majanga yoyote ambayo yanaweza tokea.

Chanzo Eatv News

View attachment 877530
Wameridhiana!
 
Mwanaume anaendelea kutawala wanawake!Wanaume tumejipa haki ya kulala hata na wanawake 4 nyumba moja, ila wao wanawake ni kosa la jinai.Ipo siku wanawake watakinukisha tutakosa pa kujificha.Tulishawatangulia acha tuendelee kuwatawala tu mana hata sheria tunawatingia sisi.
 
Jirani na sisi hatulali siku hizi.We're no longer 'Behind Men..'We're side by side
Igweee! The council has spoken! [emoji1]
Mbona uhuni wote huo lakini? Tunajua sote kwamba dume wawili kamwe hawawekwi kwenye zizi moja. Umbali wa angalau kilomita moja unahitajika. What says you your royal highness?
 
Duh! Kwa hiyo wewe usiye mjinga unachangia mke wako na mwanaume mwingine nyumba moja? Acha povu kijana...

Hata hivyo, kama wenyewe wameridhika sioni tatizo, lakini usirudie kuita watu wajinga eti kwa sababu mna mitazamo tofauti...
Umenena vizuri tena msisitize kabisa mkuu
 
Kenya bhana...wameacha kukatama mashoga wanafuata watu wanaoenda njia sahihi
 
It is known as polyandry. Ujinga wa Watanzania wengine ni kukosa uelewa wa kinachoendelea duniani kwa kuwa this is a normal thing in different cultures around the globe...but Danganyika uchanganye na Tanzagiza kisha uongeze LDC na Maji Maji rebellion upate most stupid Africans to ever roam this continent.
Wacha upuuzi ww,acha ufala.
 
Umesahau. Ukichanganya na albino eaters you get the most scariest human beings in the world only found in bongoland kwa bongolala
 
It is known as polyandry. Ujinga wa Watanzania wengine ni kukosa uelewa wa kinachoendelea duniani kwa kuwa this is a normal thing in different cultures around the globe...but Danganyika uchanganye na Tanzagiza kisha uongeze LDC na Maji Maji rebellion upate most stupid Africans to ever roam this continent.
Pole broo,vipi wewe na hiyo mwenzio mlianzaje anzaje hadi mkampata mke mmoja?.Type maujanja hayo mkuu.
 
Ila wao wanakaa na sisi wanne ndani na ni sawa tu.Huu ujinga wa Waafrica sijui utaisha lini.
 
Pole broo,vipi wewe na hiyo mwenzio mlianzaje anzaje hadi mkampata mke mmoja?.Type maujanja hayo mkuu.
Sijui tulijipata aje kwenye hii love triangle ila we in love with one chick...
 
Igweee! The council has spoken! [emoji]
Mbona uhuni wote huo lakini? Tunajua sote dume wawili kamwe hawawekwi kwenye zizi moja. Umbali wa angalau kilomita moja unahitajika. What says you your royal highness?

Hahaha!, inategema lakini na nani anaweka huo umbali, na anauweka vipi. 😁
 
Nway, gender equality aside, how have you been getting on Nalendwa? Work with me here, as I smoothly change the topic. 😎
 
Back
Top Bottom