Kenya: Ndege mbili zagongana angani, wawili wafariki Dunia

Kenya: Ndege mbili zagongana angani, wawili wafariki Dunia

Ivi kale kamlio kabla ya taarifa ya habari bado n kale kale?

Nakumbuka miaka hiyo ukienda kwa bibi ni radio one tu imesetiwa na haijawahi kubadilishwa, ukitaka ugomvi na bibi fanya kutaka kubadilisha stesheni yake pendwa RADIO ONE.

Ukiwasha redio unachoruhusiwa kufanya ni kuongeza au kupunguza sauti tu.

Bibi hakuwa na saa wala hakujua kusoma ila yupo on time na anayajua majira mno, ile sayansi sijui ni ya aina gani akikwambia washa redio saa saba mchana imefika, ukiwasha kweli n ngoma saba kamili na kama haijafika basi ni kasoro dakika 2 au moja.

Wapumzike kwa amani waliofariki kwa ajali hiyo.
Wakati niko mdogo nilikuwa na uwezo wa kuangalia jua au kivuli changu na kujua ni saa ngapi kutokana na shughuli za kila siku tulizokuwa tunafanya ni mazoea tu

Sent from my TECNO KC8 using JamiiForums mobile app
 
Nimesikiliza kipindi cha Nipashe asubuhi ya leo 06.03.24 mtangazaji anasema watu wawili wamefariki kutokana na ndege mbili kugongana angani huko Kenya, lakini mtangazaji wa Kenya anasema ajali iliyouwa watu wawili ni ile ya mafunzo ambayo imeua Mkufunzi na mwanafunzi wake, ila hajasikika akisema ndege hizo zimegongana angani kama mlivyosema.
Ajali ni hiyohiyo inahusu ndege mbili za mafunzo, kwa habari zaidi ingia google niliisoma jana.
 
Mamlaka ya Usafiri wa Anga nchini Kenya imethibitisha kisa cha kugongana kwa ndege ya abiria ya kampuni ya Safarilink na ndege ya mazoezi.

Uchunguzi umeanza kubaini chanzo cha ajili hiyo.

‘’Uchunguzi umeanza kupitia mashirika mbalimbali ukiongozwa na Idara ya Uchunguzi wa Ajali za Anga na Huduma ya Taifa ya Polisi kubaini chanzo cha ajali,’’ Mamlaka ya Usafiri wa Anga Kenya imesema.

Abiria wawili waliokuwa kwenye ndege ya mazoezi wote wameaga dunia huku abiria 39 na wafanyakazi 5 katika ndege ya Safarilink wakiokolewa hadi eneo salama.

Shirika la ndege la Safarilink imesema kupitia mtandao waX kwamba muda mfupi baada ya kupaa mwendo wa saa tatu na dakika 45 asubuhi saa za eneo hilo, kishindo kikubwa kimesikika.

BBC
Kuna mwaka ilibakia kidogo ndege zigongane maeneo hayohayo ya Kenya


 
Back
Top Bottom