Kwa hiyo hao wakenya wa gazeti la standard, na media zote za Kenya pamoja na wasomi wote wanaosema lengo la kuuza kwa sasa ni ili kupata pesa za bajeti hawajui kitu wewe ndio unajua kila kitu?.
Mbona serikali isiwachie private sector kujenga SGR kama unahisi serikali haiwezi kuendesha mashirika kwa faida?. Unadhani mashirika yote yanayobinafsishwa yanatengeneza faida?, mbona KQ inatengeneza hasara, Kirubi anajuta kuwekeza pesa yake KQ, reli yenu ya zamani mbona mlibinafsisha lakini hali ni mbaya zaidi?.
80% ya UMEME wa Kenya huzalishwa na KenGen, ambapo serikali inamiliki 70% ya share, hii maana yake serikali ndiyo yenye maamuzi ya mwisho kuhusu bei ya UMEME kwa wananchi, ni hatari sana serikali kupoteza huo uwezo wa kuamua bei ya UMEME kwa wananchi. Mkiendelea kupunguza huo uwezo wa maamuzi mtapoteza nguvu ya kupanga bei, kumbuka UMEME ni engine ya uchumi wa nchi.
Acha kabisa kusema eti serikali inaweza kupanga na kudhibiti bei vile itakavyo, huo utakua sio uchumi huria, hivi kwanini hushangai bei ya Diesel na Petrol Kenya IPO juu kuliko nchi zote za EAC, moja ya sababu ni kwamba serikali yenu imeachia private sector kufanya kila kitu katika ununuzi, usafirishaji na usambazaji.
Tanzania serikali inasaidiana na private sector katika kutafuta wapi kunapatikana Diesel na Petrol kwa bei nafuu huko nje, then serikali wanasaidia yasafirishwe in bulk, sio kila importer asafirishe kivyakevyake, mwisho yanafika Tanzania yakiwa na bei ndogo.