Tanzania ni nchi iliyobarikiwa utajiri mkubwa sana kwenye rasilimiali kuanzia ardhi nzuri ya kilimo, madini, vicutio vya asili, n.k. lakini bado tupo nyuma sana kimaendeleo, Kenya ni nchi ambayo ina rasilimali chache lakini wametufunika kwasababu wamewekeza zaidi kwenye watu (elimu, ujuzi) na wamejitahidi kuweka mazingira bora kwenye biashara.
Kwetu hapa mazingira yanatuangusha sana
Kwetu hapa mazingira yanatuangusha sana
- Usumbufu wa TRA
- Task Force - Wamefanya wengi wafirisike nakufunga biashara
- Mambo mengi bado tunapanga foleni maofisini badala ya kufanyia online.
- kodi na tozo kibao
- mlolongo mrefu kushugulikia leseni, vibali, usajili, n.k. kwenye ofisi za serikali
- Mpaka leo hatuna mfumo maarufu wa Paypal kuturuhusu watanzania kupokea pesa kutoka Ulaya, Marekani, n.k. tumebanwa kufanya malipo pekee
- bandarini kulalamikiwa kuwa na kodi nyingi, mlolongo mrefu kutoa mzigo, n.k.
- n.k.