Kenya wana Katiba Nzuri, Tume huru ya uchaguzi, lakini Raila analalamika kuibiwa kura, na bei ziko juu, na tozo zimejaa

Kenya wana Katiba Nzuri, Tume huru ya uchaguzi, lakini Raila analalamika kuibiwa kura, na bei ziko juu, na tozo zimejaa

Majority wakiridhika hata na ujinga wanakuwa sahihi? Bora PhD ya Tale

..suala la katiba mpya sio ujinga.

..katiba mpya itatuwekea utaratibu mzuri zaidi wa kutatua changamoto za kiuchumi, kijamii, na kisiasa.
 
Nadhani inabidi kuirejea hii ajenda ya katiba mpya, ni kweli wananchi wanaitaka au ni wanasiasa ndio wanaitaka?

Kenya Wana katiba mpya, lakini bei za bidhaa ziko juu mpaka Leo Erick Omondi kaandamana Bungeni na akapigwa mabomu na kukamatwa. Na sisi wa katiba ya zamani bei ziko juu.

Tozo ziko juu, pale pale sawa na sisi wa katiba ya zamani.

Nadhani mabadiliko ya sheria zilizo chini ya katiba yanatosha. Mama Kaunda tume ya haki jinai, mapendekezo yake yakifanyiwa kazi, hutamuona mtu anasema katiba. Huko kwenye jinai ndiko wananchi wanakutana na mapolisi Kila siku.

Cha kushangaza, huko Kenya kwenye katiba mpya, Erick Omondi kaandamana, kapigwa mabomu, kakamatwa, na katiba mpya ipo inayotoa Uhuru wa kuandamana!

Let's go back to the drawing table. Ni katiba kweli tunataka au Kuna kitu tunataka lakini hatujui ni kitu gani! Ila Mimi kama nakiona Samia anakifanyia kazi, kwa ambao hawakioni, nitakuja na Uzi kuonyesha kwamba wananchi hawataki makaratasi na vyeo vipya.

Asamaleko!
We must stop dictatorship in Kenya, this is a democratic country cannot be ruled by two tribes since independence, stop it or we shall divide Kenya into two parts like Sudan and Eretrea

The last person to leave this country [emoji1139]should remember to switch off the lights and drop the keys to the neighbouring country, we will come back when everything is normal.
 
..suala la katiba mpya sio ujinga.

..katiba mpya itatuwekea utaratibu mzuri zaidi wa kutatua changamoto za kiuchumi, kijamii, na kisiasa.
Kwani sasa hatuna katiba au mpaka iwe mpya- na upya wenyewe ni nini hasa
 
Kwani sasa hatuna katiba au mpaka iwe mpya- na upya wenyewe ni nini hasa

..maoni ya wananchi kuhusu Katiba yalikusanywa na yapo ktk rasimu iliyoandaliwa na Tume ya Jaji Warioba.
 
..maoni ya wananchi kuhusu Katiba yalikusanywa na yapo ktk rasimu iliyoandaliwa na Tume ya Jaji Warioba.
wananchi gani- mbona unatuletea usanii maana sote tulikuwepo- YAANI Pemba, Kigoma kuongoza kwa idadi ya watu kutoa maoni kuliko Dar es salaam- halafu mnataka watu wazima tuunge mkono ujinga huo?
 
wananchi gani- mbona unatuletea usanii maana sote tulikuwepo- YAANI Pemba, Kigoma kuongoza kwa idadi ya watu kutoa maoni kuliko Dar es salaam- halafu mnataka watu wazima tuunge mkono ujinga huo?

..tubishane kuhusu maudhui yaliyoko ktk rasimu ya Tume ya Warioba na sio jinsi tume ilivyokusanya maoni.

..pia kuna nafasi ya kura ya maoni kuhusu katiba itakayopendekezwa hiyo ni nafasi nyingine ya wananchi kuunga mkono au kupinga katiba mpya.
 
Sitaki ku-justify kitu, nimeweka hoja tu
Hoja yenye agenda....!!?

Ni sawa na kufananisha nyumba ya nyasi na nyumba ya bati. Wote wanajikinga na mvua na wanapata usingizi. Kwa hiyo nyumba ya nyasi ni poa tu kama ilivyo ya bati. Zote zinasave same purpose.
 
Katiba mpya ndio itapunguza bei ya chakula? US wana katiba nzuri, mbona Trump hadi leo analalamika? Kwani katiba inazuia mtu kulalamika?
Katiba nzuri inawasaidia wananchi kwakuwatendea haki lakini sio viongozi wanaotaka madaraka kwa nguvu. Ubinafsi hautoisha
 
Back
Top Bottom