Jack Daniel's
JF-Expert Member
- May 18, 2015
- 1,008
- 835
(a) Hakuna lugha iliyokamilika, Kiingereza pia kina upungufu wa misamiati au neno moja linaloelezea kitu au jambo fulani: Jaribu kutuambia neno moja la Kiingereza linalojitosheleza kuelezea mifano hii;.....Wewe ndiye mwenye ushamba maana unategemea lugha moja ya Kiswahili ambacho chenyewe hakina maneno mengi ya msingi kwenye masuala ya uchumi.
Treni inaweza kuwa bila behewa na ikaitwa treni, kwa mfano ile inayotumiwa kwenye shunting.
Tatizo Kiswahili chenyewe magumashi na kinatumiwa sana na nyie wavivu, na ndio maana mpo nyuma hivi bila uelewa wa mambo mengi.
Unaposema "Kichwa cha treni" hayo ni maelezo ya maana ya neno locomotive, na sio mbadala wake.
Kama nilivyosema, nina uelewa wa ndani wa masuala ya reli, tatizo ni lugha yenyewe dhaifu na inakua tatizo kupata maneno yeke hata kwenye kamusi.
Kwa mfano, nimetafuta sana neno mbadala ya "Shunting", kuna siku niliandika ripoti fulani ya masuala ya reli ambayo nilitegemewa kuitafsiri pia kwa Kiswahili. Aisei nilihangaika kishenzi, lugha ya Kiswahili bado sana.
Mfano 1, pale unapokuwa umeshiba sana, ila chakula ni kitamu sana na hutaki kuacha....
Mfano 2, unakula chakula cha moto, hadi unafunua mdomo, na kutikisa kichwa ili chakula kipoe.....
Mfano 3, Kulala sakafuni bila kutandaza chochote, huku umelewa na upo uchi.....
Mfano 4, Kiswahili kuna kesho, keshokutwa, mtondo, mtondogoo, hebu tuambie kwa Kiingereza, siku zinazofuata baada ya 'Tomorrow'...
(b) Kwakuwa unazungumzia masuala ya treni, na umedai, kushindwa kuona neno moja la Kiswahili linaloelezea 'Kichwa cha treni' kunaifanya Kiswahili kuwa lugha ya 'magumashi' inayotumiwa na 'wavivu' na 'wasio na uelewa wa mambo mengi', naomba kuuliza:.......
Tuna neno 'behewa (umoja) au mabehewa (wingi) kwenye Kiswahili, tafsiri yake kwa Kiingereza ni neno 'railroad car(s)' au 'railcar(s)' au 'railway carriage(s)'.....Rail+road+car(s), rail+car(s), rail+carriage(s), Kichwa+cha+treni.....Ina maana tatizo la kukosekana kwa neno moja lipo kwenye lugha zote?......