Kenya: Zifahamu jamii mbili zenye nguvu nchini Kenya

Dah. Utakuwa mchaga wewe! Hivi unafahamu ule wimbo wa...utaacha mali yako utaendaaa...utaendaaa....utaendaaa.X15🙂...utaenda mbinguni kwa baba! Hehe natumai ujumbe wangu umekufikia!
Ha ha haaaaaa! huo ujumbe mbona kuntu[emoji4] [emoji4]
 
Ni kweli hayo makabila ni moto, lakini inabidi kupambanisha Wachagga, Wakikuyu, na Wahindi. Nadhani hiyo utakuwa mechi kali ya kununua gunia zima la popcorn.
Wahindi mwisho mkuu
 
Halafu niulize kaswali kadogo, hivi kwa nini wakikiyu wengi hawapendi kula samaki? CC MK254

Nafikiri ni exposure ya mtu tu, maana kule mlima Kenya hakuna ziwa, hivyo wengi wamekutana na samaki baada ya kutoka. Mimi nimelelewa mjini ambapo tulitangamana na Wajaluo na makabila mengine, hivyo nimekua na fursa ya kula vyakula vya aina nyingi.
Lakini taratibu Wakikuyu wameanza kupokea huo mlo wa samaki, kwanza Ukikuyuni wamejenga mabwawa kwa ajili ya ufugaji wa samaki.
Exposure tu basi, maana siku ya kwanza niliona watu wanakula pweza huko Dar nikapata kichefuchefu, leo hii mchuzi wa pweza ndio kila kitu kwangu kila nikiwa Dar.
 
Khaa najua kabila la Kaskazini Magharibi unaloliongelea ila suala la usomi ni nadharia tu..nilipokuwa chuo ratios za Kikuyu, Luhya na Jaluo zilikuwa sawa tu.

Sasa mbona hujatoa ufananisho wa Wakikuyu Tanzania?

Sent using Jamii Forums mobile app
Wakina rutashobya, rugemarila, rutashemwa.


In mpoki's voice
 
Na pia mabinti wetu waMeru kuna wengi weupe angalau kwetu Meru ni eneo karibu sana sana na equator.Wale watu wa Gambia na Senegal ni weusi kama makaa ingawa wanatoko Afrika kule juu mbali na equator.
Kitu ungewaeleza waTz ni kuwa Kenya kuna wabantu, waniloti na cushites.
 
jamaaa hawavumi lakini wamo...sijajua ni kwa nini wanapenda sana biashara maeneo ya mpakani..
 
Kwa jinsi unavyoongelea Wakinga nikajua wana maviwanda, ma-real estate, media houses, mashirika ya usafirishaji, mahoteli ya nyota nne na tano. Cha ajabu unaongelea biashara ya maduka yaani uchuuzi tena kwa Kariakoo halafu unafananisha na Jamii yenye investments kwenye huduma za kibenki, madini, viwanda, usafirishaji na mahoteli yenye hadhi. Kuwa serious basi Mzee.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
MK254,
Utani kidogo:
muhaya anayewakilisha wahaya wote wa jf kwa kuandika kwa kingereza ni huyu jamaa anajiita Rutashubanyuma.

sina hakika sana kama ni muhaya,huenda anatumia tu jina lenye ufanano na wahaya.

jamaa ana-topic yake hii hapa:Why Magufuli administration misses the point on government splurge
ukipata mda ipitie.

huko ni kingereza tu,tena sio kile cha kawaida tunacho jaribu kuandika akina sie,ni kile cha ma-jargon na
ma-synonym ambayo sio common sana kwa wazungumzaji wa kingereza.

kwa kuwa nipo opposite na opinion zake kuhusu JPM,niliamua nipambane naye kwa kiswahili tena kiswahili cha kihuni huku nikim-troll kidogo kidogo.[emoji23]

nikamwambie wewe andika tu hayo "majagoni" yako,nitakuwa nakujibu kwa kiswahili.

ikafika wakati akakasirika,akanichongea kwa moderator,hatimaye nikanyimwa access ya kuandika comment kwenye thread yake kwa muda wa siku kadhaaa.wahaya bhana.[emoji23] [emoji23] [emoji23]

ruta usinikasirikie,nimeandika kama utani tu.[emoji23] [emoji23] [emoji23]
 

nilikuwa hasa naangazia wakinga vijana
ambao wamechipukia kwenye ujasiriamali miaka ya hivi karibuni.kwa hakika wamefanikiwa kwa kiasi fulani hasa katika maduka mkubwa ya jumla.

sidhani kama wamejiingiza kwenye uwekezaji mkubwa wa viwanda,hata hivyo, kwa speed yao sitoshangaa wakianza kuingia huko.

wapo wakinga wazee ambao investment zao zinafahamika,mfano ni mmiliki wa kampuni ya usafirishaji ya super feo express na mmiliki wa peacock hotel.
 
Sawa lakini ku-generalize kwamba kwa biashara ya maduka wanawafunika Wachagga sidhani kama sawa. Hebu angalia mali za mtu anaitwa Mrema kafariki juzi halafu upate picha ya ninacho jaribu kusema. Huyo jamaa ana real estate projects za nguvu mpaka Nairobi ukiacha hoteli alizoacha na project nyingine zikiendelea. Je wa Peacock anaweza kufananishwa na huyo? Unajua biashara ya mabasi na malori ni kitu cha kawaida sana kwa watu wa Moshi? Fuatilia vizuri uone. Halafu uje kwenye usafiri wa anga pia. Labda TCAA watusaidie kuona wamiliki wazawa wa scheduled na chatter flights pia choppers.

Na si kwamba sitambui ujasiriamali wa Wakinga ila kuna upotoshaji kwa unachosema. Wakati wakinga wanachipukia kwenye maduka ya jumla kuna watu wanaingia mikataba na Wachina na Wajerumani kuwekeza viwanda vya vifaa vya Ujenzi Tanzania. Kuna watu wanamiliki biashara ya ku-export kahawa, kakao, pulses, maua na mbogamboga kwenda Ulaya na mahindi kwenda Kenya, DRC yaani wanalisha nchi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
hapo sawa geza ulole
 
Mwenye Peacock hotel sio Mkinga bali ni Mhehe,anaitwa Mfugale.
 

Aisei nimecheka kwa sauti hapa watu wananiona chizi, huo uzi wake naujua tena himo niliwahi kujitosa na kuandika mawili. Jamaa yuko sawa sana....
 
Mwenye Peacock hotel sio Mkinga bali ni Mhehe,anaitwa Mfugale.
sawa mzee wa busara...nilidhani ni mkinga.

hivi ni kweli hakuna mkinga mwenye kiwanda ukiachilia mbali maduka ya vifaa vya ujenzi wanayoyamiliki?
 
Why not? Unajua Mwenge toka Lugalo kwenda Mlimani city mpaka Makumbusho/Regent/Morocco ni center yenye biashara kubwa na pia prospect kubwa. Hapo acha Kawe city iliyopita U/C. Na itaipiku K'koo..


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Aisei nimecheka kwa sauti hapa watu wananiona chizi, huo uzi wake naujua tena himo niliwahi kujitosa na kuandika mawili. Jamaa yuko sawa sana....
jamaa ni shida sana yule...nadhani ana lala na dictionary ili aitumie kutafuta maneno magumu ya kingereza ili ayatumie katika thread yake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…