Hivi wewe unajitambua kweli?, kama uchumi wote upo mikononi mwa watu wachache na majority ya wananchi hawana kitu zaidi ya kutumikishwa na hao matajiri, kunafaida gani?. Duniani kote nchi zinapambana kuhakikisha kwamba uchumi unakuwa distributef fairly kwa wananchi wote, wewe unaleta maneno ya ulevi hapa jamvini.
Nchi inayosifika duniani kuwa na uchumi mzuri na bora ni Norway, kwa sababu tu uchumi vipato kati ya wananchi wake havitofautiani sana, kwamba uchumi umegawanywa karibu sawa kwa wananchi wote, Norway haina hata tajiri mmoja kati ya matajiri wakubwa 100 wa dunia. Huwezi kuwa na nchi yenye matajiri elfu 10 na masikini milioni 20 na ukaona sio tatizo. Kenya ni nchi yenye matatizo mengi yaliyosababishwa na kufuata ubepari kichwakichwa.