Hivi uchumi wa Dunia unamilikiwa na asilimia ngapi ya watu wote waliopo Duniani?
Kuna wakati Waziri Mkuu wetu Tanzania, aliwahi kuliambia Bunge kwamba Uchumi wa Tanzania unamilikiwa na Watanzania wa nane tu! Na kwamba ukiwashughulikia hao uchumi utayumba! Katika hao Watanzania wanane, sita kati yao ni wenye asili ya Asia.
Nachotaka kusema hapa ni kitu kimoja, kwamba daima idadi ya matajiri ni wachache popote pale duniani, ukilinganisha na masikini!
Suala na weupe/wazungu kumiliki uchumi kuliko weusi hilo sio jambo geni. Ni tatizo la kiasili!
Lkn Watanzania wa leo sijui kwa nini tunayafurahia mabaya ya wenzetu kana kwamba yetu ni mazuri!
Ni ujinga kuwacheka na kuwasimanga Wakenya katika suala la kiuchumi wakati shilingi yao tu ni imara mara 20 kuliko shilingi yetu.