Bosi Michembe
JF-Expert Member
- Jun 24, 2011
- 271
- 87
Bujibuji mambo gani tena haya kaka yangu? Ile helicopter waliopanda hao viongozi imelipuka angani na kuanguka ikiwa imeharibika, si nzuri kama uliyoonyesha wewe. Na kwa uzuri zaidi mimi kwa wakati huu niko mjini Nairobi katika mihangaiko yangu ya kuitafuta shillingi, na Citizen TV wanaonyesha hiyo crash site ni porini (Kibiku forest, maeneo ya Ngong); na helicopter yenyewe iko nyang'anyang'a.
Ila kuna mambo mengi yanasemwa kuhusu ajali hii hapa Nairobi, mosi, rubani aliyekuwa amepangwa awali kajitoa dakika za mwisho ndipo akateuliwa mwingine (Madam Nancy Githuana) ambaye ndiye amekuja pata ajali na amefariki; pili miili ya waliokuwemo kwenye ndege imeungua haitambulikani, lakini pesa walizokuwa wamebeba kupeleka kwa fund raising hazikuungua kuteketea. Makubwa, lakini ndiyo hivyo, Prof George Saitoti, Naibu wake Orwa Ojode, walinzi wao wawili na marubani wawili wamefariki. Mwenyezi Mungu aweke roho zao mahali pema peponi.
View attachment 56013View attachment 56014
Poleni wafiwa na Wakenya wote..
RIP Saitoti