- Thread starter
- #61
We
Unawashauri wafanye kufukuza watu?? Unategemea kitu gani kitokee upande wapili wa shilingi? e.g NCCR-Mageuzi au ACT-Wazalendo
Je itakuwa sawa Watanzania wakasema tuwafukuze wawekezaji Uchwara kwa sababu wanakwepa kulipa kodi, kodi ambayo ni haki ya Mtanzania? Kwa sababu wapo watu wa namna hiyo au?
Ni dhuluma zipi hizo, Kwamba kashindwa Uchaguzi kwahiyo ni dhuluma?
??
Kulikuwa na kawimbo:
"Nyerere yupo ukiona kundi la wapigania haki na yeye yupo."
Kina Che Guevara walikuja kupigania haki hadi DRC. Wakafia ugenini Cuba huko, kama mashujaa.
Chadema ni movement ya haki. Wa nini wasioamini kwenye haki?
Odinga hana rundo la wapumbavu. Ana wachache waliodhamiria na kazi inaendelea.
Odinga ana agenda zake zinazokubaliwa na wakenya. Agenda hizo si za kikabila kama zinavyodaiwa na wapuuzi wa kwetu. Agenda zake kwao wanazitambua kuwa ni za haki ndiyo maana anaungwa mkono.
Tunazo zetu za haki tunazozipigania kupitia chadema. Mbinu za kupigania haki ni zile zile kote duniani.
Hupiganii haki na wasio waumini wa haki.
Hapo ndipo tunapokwama sisi.
Tuna wajumbe mizigo baina yetu. Hawa ni heri kuwafurusha kuliko kuwa nao.