Njiani Kuna vituko sana
Miaka ya nyuma niliwahi kupangiwa siti na dada mmoja sister du kinoma sema alikua Pisi sana maringo mengi, kwenye kutafta siti namuona ndo kaka kiti Cha pembeni nikasema mambo si ndo haya, ebana ile nampa salamu dada kanikata jicho Wala hakuitika akatoa ipad yake(kipindi hicho 2nd generation) akaweka earphones Wala hakunisemesha, nikafadhaika nikasema poa tu
Njiani kufika ile sehem ya chakula nikavuta sambusa zangu na soda take away nikarudi zangu kwenye gari, sister du kaja na chips kavu nyama choma na kachumbari ya kutosha ( big big mistake) ๐๐
Sasa sijui ile kachumbari ilikua imelala au vipi, aisee baada ya muda safari kuendelea sister duh tumbo likavuruga, kama usiwahi pata tumbo la kuhara najua Kila mtu anaelewa mziki wake, sister du akaanza kuomba kujisaidia maporini, konda akawa anamkubalia anampa na maji ya kujisafisha Yale ya emergency kwenye madumu kwa ajili ya kupooza rejeta, anaingia porini anafanya yake anarudi, tumbo nalo halina adabu ukikaa tu ndo linachanganya zaidi๐๐
Akapiga trip kadhaa abiria wakaanza kua wakali gari linasimama Kila muda, mi hapo Sina habari na mi nikatupia earphones zangu... Kuja mwangalia huyu sister du aisee anataka kulia anajinyonga nyoga sio poa nikaingiwa na Imani nikamzingua konda pale na abiria kadhaa wakisimama akatoka tena, maji yashaisha anapewa zile hand tissues, aisee huyu sister du sijui nguvu zilimuishia au alikua ashavurugwa yaani akawa haendi porini tena, akishuka tu anavua nguo anaachia mzigo karibu na gari kabisa, watu wanafanya Kuona aibu kumtazama wanaangalia pembeni....
Kuna mama akamstiri kanga maana nguo ilishaanza kulowana kwa nyuma, tukafika Kijiji kimoja nikaongea na konda pale nikashuka nikaenda pharmacy Kuna dawa nikamchukulia na maji, Mungu saidia tumbo likatulia mpaka tunafika.... Alikuja kuniomba namba mwenyewe kwa aibu
Wahenga sio watu nilikuja kupita nae kimasahara na mpaka Leo tunawasiliana mara moja Moja ana maduka tu makubwa ya electronics kariakoo aliotea kuolewa na jamaa kibopa hatari
,