Kero gani umewahi kukutana nayo kutoka kwa abiria mwenzio wakati unasafiri?

Kero gani umewahi kukutana nayo kutoka kwa abiria mwenzio wakati unasafiri?

Kuna dada tumefika Nzega akanunua nyama za kuku na chipsi zinazouzwa sted na nikamuonya hizi chips sio nzuri achana nazo hakusikia dk20 likanitapikia . DAAH SITASAHAU NA SIKUWA NA NGUO ZA KUBADIRISHA
 
Lile mama la kisukuma:
1. Kuweka kuku wanne chini ya Siti
2. Kusafiri na watoto Watatu alafu akaniomba Mimi nimpatate toto lake lenye miaka sita😡
3. Kuwanunulia watoto vyakula Kila gari likisimama huku akijua kuwa watoto wake wanatapika kwenye gari
Hapo namba mbili,kama ulimpakata huyo mtoto wewe ni muoga sana
 
Lile mama la kisukuma:
1. Kuweka kuku wanne chini ya Siti
2. Kusafiri na watoto Watatu alafu akaniomba Mimi nimpatate toto lake lenye miaka sita😡
3. Kuwanunulia watoto vyakula Kila gari likisimama huku akijua kuwa watoto wake wanatapika kwenye gari
Uwa nakataa kumpakata mtoto wa mtu ila mdada akiwa na kitoto kidogo cha miaka 2 au 3 napenda kucheza na hicho kitoto uwa nakichikua na kumsaidia.
 
July 3, 2016 natoka Dar naenda zangu Nzega Tabora, nlipanda city boy ya kahama(hii kesho yake wakati inarudi Dar ilikula mzinga pale maweni uso kwa uso na city boy iliotoka Dar ) tunakaribia singida stendi hali ya hewa ndani ya chombo ikachange ghafla, harufu kali vibaya mno, wenye watoto wakaanza kuwakagua kama wamejisaidia lakini hamna kitu, chombo kikafika stendi singida akashuka mafia mmoja kajifunga sweta kiunoni kachafuka mbaya, kulikua na wasukuma ndani ya basi wakawa wanamzomea (nyelaga,nyelaga) tulimuacha palepale singida yule mwamba
 
Asubuhi midomo inatema usiombe mtu aongee na simu hadi mkifika chimba dawa angalau akila kitu.
Pia watu ulala sana wanaachia sana harufu kubwa sababu ya kulewa usingizi
 
Umepanda kwenye daladala umekaa kwenye siti unachati af mtu anachungulia + abiria wa pembeni kusinzia af akuegemee!
 
Habari ya konda kubaki na shilling . Mia au hamsini yangu huwa sipend na siwi na amani kabisa katika safar
 
Back
Top Bottom