Kero hii ya kutofikishwa kileleni

Kero hii ya kutofikishwa kileleni

Unapoona kwenye mahusiano watu wanagombana lakini hawaachani jua hao wanapendana sana na hutimiziana haja zao mubashara kabisa! Hufikishana kileleni!!!

Mahusiano mengi yamevunjika kutokana na tatizo sugu la kutofikishana kileleni hakika hii ni Kero kubwa mno
Elimu ina pande mbili, unaweza kusoma na ukafaulu mitihani lakini usielimike na mwingine anaweza asisome elimu rasmi lakini akaelimika na kuwa mtu bora kabisa

Ni katika hilo la elimu kuna utashi utayari kujituma kuelewa na kiwango cha IQ pia! Kuna watu kwa njia za ajabu kabisa wamepata mafanikio yanayoliliwa na wengi lakini kwakuwa kiwango chao cha ufahamu ni kidogo sana wamejikuta wanaangukia pua na kufeli kabisa

Kwenye mfumo wa taa za magari kuna taa inawaka sana inaitwa spotlight...hii haiwashwi hovyo! Dar es salaam ni spotlight ya nchi kuna tofauti kubwa sana kati ya rc wa Kigoma na rc wa Dar

Chochote kinachofanywa Dar kinakuwa kama mwongozo wa kwingine kote
Mtu ambaye anabamba sana kwasasa kwenye mijadala ni bwana Makonda (bashite?) vyovyote iwavyo kati ya wengi wanaomponda wengine ni kutokana tu na wivu na kijicho! U-rc wa Dar si nafasi ndogo ati pesa hata kama huitaki itakufuata tu na ukiikataa basi unahitaji kupimwa akili

Tumjadili rc kwa hulka yake ya kutotimiza yale anayoyaanzisha. Hili halina tofauti na ile Kero ya kutofikishwa kileleni
Hulka hii mbaya ni sawa na chumba kile cha mahututi gereza la fikra
Haya yameishia wapi?

Vitambulisho maalum vya walimu ili wapande bure
Dar tuitakayo
Operation Ondoa ombaomba
Kero za wanadarisalama
Na operation nyingine nyingi zilizifeli kabisa

Shida ni moja maandalizi na kushirikishana hakuna. Lakini Dar ni jiji lenye wataalam na wasomi wa kila kaliba iweje hakuna kujadiliana kwanza?
La dawa za kulevya ndio bye-bye tumeachwa na hamu zetu hatujafikishwa kileleni tunachafuliwa tu kila wakati

Kama ukiamua kuwa banditu baki hivyohivyo usiwe kama mkate mgumu mbele ya chai
Mwanaume kakaa mahabusu siku zaidi ya 100 lakini katoka na tabasamu wewe Leo kuombwa tu kuonyesha vyeti unamwaga michozi hadharani! Nini maana ya kuwa kiongozi?
Andiko zuri
 
daaha hapo kwa mwanaume kakaa jela siku 100 katoka na tabasamu ,lakini jombii ya daslam kuombwa vyeti kalia kweli,nadhani tunatakiwa ku assess uanume wa huyu mkuu wa mkoa wa daslam maana ujinga anao ufanya ni tofauti na maisha aliyopitia nilitegemea angekuwa strong maana kama manyanyaso na masimango ameyapitia sana maana kalelewa sana na watu baki katika maisha yake..!!binasfi na mashaka na uanume wake
Acha ujinga wewe, kwani kipimo cha Uanaume wa mtu ni kutokulia? Kwa wale wanaotumia Biblia na hata wale wasioitumia ila wanauelewa juu ya biblia wanaweza kuwa na jibu sahihi, PETRO mwanafunzi wa YESU, aliitwa MWAMBA na YESU mwenyewe na kuahidiwa kwamba Juu ya Mwamba huo atalijenga Kanisa. Lakini baada ya Petro kumkana Yesu mara tatu alilia huku akimuomba MUNGU msamaha, Je, Petro nae tumweke katika kudi gani?
 
Dah, wewe Mshana ni Noma, huu utakimbiliwa na wapenda ngono zaidi, hii itatoa uhuru wa mawazo. Kuliko heading ingekua " Rc..... Hajawahi kutufikisha kileleni". Hapo lingekuja povu la ajabu sana.
Mie mwenyewe nilivyoona heading nimekimbia mbio kuwahi kufika nikajua ni mambo yetu yaleeeeeeeeeeee
hahhahahahahah
 
Acha ujinga wewe, kwani kipimo cha Uanaume wa mtu ni kutokulia? Kwa wale wanaotumia Biblia na hata wale wasioitumia ila wanauelewa juu ya biblia wanaweza kuwa na jibu sahihi, PETRO mwanafunzi wa YESU, aliitwa MWAMBA na YESU mwenyewe na kuahidiwa kwamba Juu ya Mwamba huo atalijenga Kanisa. Lakini baada ya Petro kumkana Yesu mara tatu alilia huku akimuomba MUNGU msamaha, Je, Petro nae tumweke katika kudi gani?
sinakumbukumbu katika biblia kama petro alienda kulia mbele ya hadhira??alafu Petro alikiri kuwa kweli alimkana Yesu je Bashite amekiri kuwa aliiba vyeti,sikatai kuwa mjinga ila nakushangaa wewe zwazwa unaetetea upumbavu
 
sinakumbukumbu katika biblia kama petro alienda kulia mbele ya hadhira,alafu Petro alikiri kuwa kweli alimkana Yesu je Bashite amekiri kuwa aliiba vyeti,sikatai kuwa mjinga ila nakushangaa wewe zwazwa unaetetea upumbavu
kama hauna kumbukumbu kaa kushoto unasumbua Watu.
 
sinakumbukumbu katika biblia kama petro alienda kulia mbele ya hadhira,alafu Petro alikiri kuwa kweli alimkana Yesu je Bashite amekiri kuwa aliiba vyeti,sikatai kuwa mjinga ila nakushangaa wewe zwazwa unaetetea upumbavu
Alikr wap...mbele ya hadhira.. Duuuh...biblia na vya kaisal n kama mlenda na kamasi
 
"Lakini Dar ni jiji lenye wataalam na wasomi wa kila kaliba iweje"Mshana nimekipenda sana kisehemu hiki....yeye anatuhumiwa kuiba vyeti na yupo mstari wa mbele kuwapiga vita hawa "wataalam na wasomi" ambao kimsingi sio wa kaliba yake.....
 
sinakumbukumbu katika biblia kama petro alienda kulia mbele ya hadhira??alafu Petro alikiri kuwa kweli alimkana Yesu je Bashite amekiri kuwa aliiba vyeti,sikatai kuwa mjinga ila nakushangaa wewe zwazwa unaetetea upumbavu
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
INGENJA huna Hisia ndo maana unamshangaa mwanaume kulia. Wengine hulia kwa sababu ya hasira mbona hayo mambo ni ya kawaida mtaani, ndugu yangu.
 
Hahaha ninesoma na kuelewa vizuri sana. Hoja ni nzuri na inayotaka utendaji madhubuti juu ya kiongozi wetu.
 
INGENJA huna Hisia ndo maana unamshangaa mwanaume kulia. Wengine hulia kwa sababu ya hasira mbona hayo mambo ni ya kawaida mtaani, ndugu yangu.
mwanaume analia kama simba ndani ya moyo tena peke yake usiku wa manane alikwambia Banana zoro,ni udahifu mkubwa sana mwanaume kulia mbele ya umma alafu sababu ikiwa ya kijinga tu kusakamwa kisa vyeti
 
Dah, wewe Mshana ni Noma, huu utakimbiliwa na wapenda ngono zaidi, hii itatoa uhuru wa mawazo. Kuliko heading ingekua " Rc..... Hajawahi kutufikisha kileleni". Hapo lingekuja povu la ajabu sana.
🙄🙄🙄
 
Dah, wewe Mshana ni Noma, huu utakimbiliwa na wapenda ngono zaidi, hii itatoa uhuru wa mawazo. Kuliko heading ingekua " Rc..... Hajawahi kutufikisha kileleni". Hapo lingekuja povu la ajabu sana.
KWELI. KWA AGE YANGU,HII POST NIMEACHA KUIFUNGUA TANGU JANA. NILIJUA CONTENTS ZA HEADING HAZINIHUSU! DUU, UANDISHI MAHIRI SANA.
 
Kila mpango anaouanzisha unaishia kuwa kama cheti chake
Kitambulicho cha mwalimu F
Shisha F
Sensa ya vijana wasio na kazi F
Madawa F
Yani ni fafafa
 
Back
Top Bottom