KERO Kero kuhusu mchakato wa zabuni katika baadhi ya halmashauri za Mkoa wa Kilimanjaro.

KERO Kero kuhusu mchakato wa zabuni katika baadhi ya halmashauri za Mkoa wa Kilimanjaro.

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua

fanuel daniel

New Member
Joined
Oct 7, 2026
Posts
1
Reaction score
1
Naomba nitoe kero kuhusu mchakato wa zabuni katika baadhi ya halmashauri za Mkoa wa Kilimanjaro.

Kuna taasisi ambazo, kwa madai yangu, hutangaza zabuni lakini mchakato wake unaonekana kuelekezwa kumpendelea mzabuni fulani. Mzabuni mwingine anaposhinda badala ya yule anayependelewa, zabuni hiyo hufutwa bila kutolewa maelezo ya wazi kuhusu sababu za kufutwa kwake.

Katika uchunguzi wangu mdogo, nimebaini kuwa baadhi ya wazabuni wanaopewa zabuni wanadaiwa kuwa na uhusiano wa karibu na wakuu wa shule au taasisi husika. Pia, nimeona baadhi ya bei zinazowekwa kwenye zabuni hazilingani na bei halisi za bidhaa sokoni. Kwa mfano, mboga zinazoainishwa kwa bei ya Sh100 kwa kilo, hali inayozua maswali kuhusu uhalisia wa bei hizo.

Serikali na PPRA, tunaomba suala hili lifanyiwe kazi ili kuhakikisha taratibu za ununuzi wa umma zinafuatwa kwa haki, uwazi na ushindani wa kweli. Ni muhimu pia kuwe na uwajibikaji pale zabuni zinapofutwa, pamoja na kutolewa kwa sababu zinazoeleweka kwa wazabuni walioshiriki.

Je, ni wazabuni wangapi wanaweza kushinda zabuni ikiwa hawafahamiani na wakuu wa vituo au taasisi zinazotangaza zabuni?

Tunaiomba Serikali ichunguze malalamiko haya katika baadhi ya halmashauri za Mkoa wa Kilimanjaro na kuhakikisha kuwa kila mzabuni anapata fursa sawa, bila upendeleo wala mianya ya vitendo visivyo vya haki.
 
Back
Top Bottom