Kero: Mahari sasa yageuzwa chanzo cha kipato

Kero: Mahari sasa yageuzwa chanzo cha kipato

Mwanadamu hawezi kubakia salama kwa kuongozwa na hisia peke yake kwani hisia zinaziba nafasi ya akili kufanya kazi......ndio maana aliyezama kwenye mapenzi anafanya mambo anayoyaona ya kawaida lakini walio nje ya penzi wanamuona amerukwa na akili......

Kitu pekee kinacho mtenganisha mwanaume na mvulana ni matumizi sahihi ya akili badala ya emotions.......
Huyo kijana akifikia kwenye hatua ya UANAUME akili zitamjia na kujiona mjinga sana....

maamuzi ya huyo kijana yameegemea kwenye emotions pekee na ndio maana nafsi yake ikashindwa kuhimiri presha za jambo hilo......akija kwenye uhalisia atajikuta amefanya maamuzi yasiyoendana na uhalisia wa uchumi wake......na hilo jambo litazaa majuto makuu siku za usoni.........

NB;
Ukiona jambo la khiyari unatumia nguvu kulifanikisha......achana nalo....
Kabisa, umeongea ukweli mtupu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ni kijana wa Miaka 25, shahada ya Ualim, ila hakubahatika kupata ajila rasmi.

Amejiajili Kwa kufungua twisheni za mitaani na kabahatika kupata mchumba ambae ni binti wa Miaka 21 ( Ila tayar ana mtoto wa Miaka 3).

Amedumu kwenye mahusiano na binti kwa mwaka mmoja tangu desemba 2020 na Sasa na mwezi januari 2021 alishika ujauzito wake.

Ambapo kwa Sasa anamimba yenye miez 5, kijana akaona afanye mchakato wa kuanza Kuishi rasmi pamoja na binti.

Kaandika barua ya uchumba ukweni imepelekwa na imekubaliwa, majibu yamerudishwa vimeorodheshwa vitu kadhaa na pesa taslim ambazo ukijumlisha inakuja jumla ya 4,600,000 (million 4 na laki 6)

Kijana akazungumza na mshenga kua icho kiwango Ni kikubwa na hawez kabisa kukimudu, mshenga kamshauri asiogope Ayo yanazungumzika na kitapunguzwa Sana watakapoenda kutambulishwa.

sikU ya kutambulishwa maongezi ya punguza yanaendelea, ila Mwisho kabisa wazazi na Ndugu wa MKE wakaishia milioni 2 taslimu
(million 1 kwa ajili ya mahali na million 1 Ni faini ya uchafuzi- kuzalisha kabla ya kuoa )

Na mkaja wa mama laki 5 na vitu mchanganyiko vinavyogharimu laki 7.
Jumla vyote unapata million 3 na laki 2.

Kijana kasema yeye icho kiwango Hana na hawezi kupata kabisa kwa sasa, kwa KAZI anayofanya haimruhusu kabisa kupata kiasi icho.

Akasema
Yeye alijiandaa kwa million 1 na laki 5 kwa Mambo yote.

Mshenga akaliwasilisha kwa Wazee, Wazee wakasema
"ilo haliwezekani kijana maana Kwenye ukoo wetu hamna mtu ameolewa chini ya million 2 mahali na vitu vyetu, iyo umependelewa kutokana na uchumi Wako Kama alivyotuambiwa na binti yetu"

Kijana akakubali ila akomba alipe kwa awamu, 1.5million afu baadae atamalizia 1.7million.

Wazee Nalo wakakataa kata kata kua hamna Cha kupunguza hapo, labda akajipange KWANZA akiwa tayar aje.

Kijana amepanik,
Ameondoka amemuacha binti kwao na anazunguka uku na kule Anaomba akopeshwe pesa ili akamilishe zoezi.

Kaja KWANGU kwetu Kama watu wake wa karibu tumsaidie kwa Hali na mali kakamilisha zoezi lake ili alilokwisha lianza.

Kaniomba nimsaidie au nimkopeshe kiasi icho,
Kiukweli nafsi yangu imegoma kabisa na nimemwambia kabisa kua yeye Ni rafki yangu ila kumchangia suala Hilo maana naona anajitwika mzigo mkubwa wkt uwezo wake ni mdogo.

Kuna vipaumbele vingi vya Ela ila sio kwa ilo, ila Kama uwezo anao apambane mwenyewe tutamsapoti kwa vingine.

Kijana
Amepambana kwa kuuza baadhi ya vitu vyake vya ndani Kama laptop, dressing table na stendi ya viatu. Jumla vyote kauza kapata laki 5 na 50.

Amepambana tena ameenda Kwenye taasisi flani izi za mitaani ya kukopesha fedha,
ameweka bond kiwanja alichaochiwa na marehem mama ake mzazi kwa ajili ya mkopo wa 1.3 million kwa miezi 6.

Kaniomba nikamdhamini, na kiroho Safi nimemdhamini na mkopo kapata chap kaenda kumaliza zoezi lake.

Ila baada ya kijana kUondoka NIMEBAKI NA MASWALI YAFUATAYO KICHWANI:

1. Mahali Ni malipo ya shukrani kwa wazazi kwa kumtunza vema binti yao.
-Inakuaje kijana alazimishwe kulipia mahali kubwa kwa binti ambae alimkuta bila bikra?
Kibaya Zaid binti alishazalishwa kabla.

2. Inakuaje kijana atozwe faini ya uchafuzi wakati binti mwenyewe tayar alikua keshazalishwa hapo awali na binti tayar alikua na mtoto mkubwa?
Maana Ake iyo mimba ya jamaa inakua ni mimba ya pili kwa uyo binti?

3. Wazee inakuaje wang'ang'anie binti yao hawezi kuolewa na kijana bila kumaliza kabisa mahali wakati wanaona kabisa kijana uwezo wake kiuchumi Ni mdogo?

4. Wamechukua hatua gani kwa kijana aliemzalisha binti yao hapo kabla ya kulipa mahali?

5. Wazee, je Binti yao amegeuka bidhaa ya kuuzwa kiasi kwamba lazima awekewe kiwango maalum Cha gharama za kuolewa rasmi, na isipofikiwa Basi haiwezekani?
Yaani eti "Hakuna binti yetu yoyote ameolewa kwa mahali chini ya mil 3"

6. Kijana anajiskiaje anapokua na mke ndani ambae ameingia madeni na gharama za kuuza vitu vyake kwa hasara ili mradi amuoe?
Yaan una MKE ambae umepata kwa gharama,madeni na Maumivu makali sana?

7. Itakuaje endapo atashindwa kurejesha Deni ndani ile miez 6 na kiwanja Cha urithi kichukluliwe kisa Ela ya ule mkopo ulienda kulipia mahali ya kuoa MKE?

8. Binti alishindwa Nini kusimama na mwanaume wake kusimama na yeye pamoja kumtetea dhidi ya Wazee wenye tamaa ya Ela ya mahali?

Kiukweli,
Ili suala limeniacha na sintofahamu nyingi kwa jamii zetu hizi kuhusu ustaarabu na mtizamo wao Kwenye suala Zima la Utoaji wa MAHALI.

Sent using Jamii Forums mobile app
Huyo Kijana Hana akili kabisa. Wanawake wamejaa anahangaika na single mother kiasi hicho . Hana akili huyu Kijana kabisa . Angemuacha na hiyo mimba akamsusa kabisa ili wale wazee wabakie na binti Yao
 
Huyo Kijana Hana akili kabisa. Wanawake wamejaa anahangaika na single mother kiasi hicho . Hana akili huyu Kijana kabisa . Angemuacha na hiyo mimba akamsusa kabisa ili wale wazee wabakie na binti Yao
Mapenz upofu, mapenz ni kama giza.

Yaan mapenz ya baadh ya watu ni ngumu Sana kuyaelewa.

Kijana anaonekana anampenda Sana binti Kia's kwamba sidhan Kama angeweza kumuacha.

Maybe Kuna kitu special alichokua nacho binti, ambacho Mimi na wewe hatukijui.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mapenz upofu, mapenz Ni Kama giza.

Yaan mapenz ya baadh ya watu ni ngumu Sana kuyaelewa.

Kijana anaonekana anampenda Sana binti Kia's kwamba sidhan Kama angeweza kumuacha.

Maybe Kuna kitu special alichokua nacho binti, ambacho Mimi na wewe hatukijui.

Sent using Jamii Forums mobile app
Ni kutojielewa tuu au ni mgeni kwenye mapenzi . Kwahiyo anaendeshwa na hisia lakini sio akili.
 
Kuna baadhi ya Makabila kipengele cha Mahari huwa hairuhusiwi kutolewa yote, kama waliandika mahari ni milioni 1 unaweza kutoa nusu na inakubalika. Wanadai ukilipa mahari yote ni sawa umemnunua Binti yao na haruusiwi kurudi kwao. Ila hivyo vikolokolo vingine vyote (Faini, Mkaja wa Mama etc) huwa vinalipiwa ela yote au upeleke vitu husika vilivyoandikwa kwenye barua. Hii inahitaji umpate mshenga mzuri wa kuongea na kupanga hoja.

Huyo mwalimu tayari ameshapachika ujauzito, hawakustahiki kumfanyia hivyo kwa kuwa pia tayari alishazalishwa na mtu mwingine hivyo thamani yake nayo imepungua.

Ningekuwa mimi kwenye hali ya namna hiyo tayari ana ujauzito wangu, ningewaachia Binti yao kisha nawaambia tutarudi mwakani tunaenda kujipanga upya halafu sirudi tena maana vitu vingine vinatia hasira.

Aisee!. Binti tayari ameshakuwa Singo Mother halafu wanataka kumuongezea tatizo lingine.
Mi pia najuaga hivyo kwamba mahari haiishi, nilidhani ni desturi ya kitanzania kumbe kuna makabila ni lazima ulipe cash. Aisee mi ningekua huyo jamaa ningeingia mitini tutalea mtoto akiwa huko huko kwao. Yaani 1.5 million kwa single mother wanaikataa.
 
Back
Top Bottom