ni ushamba tu hata haisaidii kitu. binafsi huwa sipendi na huwa sifanyi hata kama maelekezo yatatolewa namna hiyo. mara tushikane mikono, siku moja mmama mmoja akanishika kwelikweli, kumbe alikuwa single mother na wife anamfahamu, nadhani ile kumshika alikuwa sijui ana siku nyingi sana, nikaona haachii mkono na anafurahia kwelikweli kuushika. wife alikuja akakaa upande wa pili akatutenganisha, na yeye akahama siti baada ya kuona wife hajafurahishwa. mnachotakiwa kujua, sio wote wanaenda makanisani wanafuata Neno la Mungu, wapo wengine wametumwa na shetani kabisa kwenda kuvuruga ibada (wachawi), wapo wengine wamejiuza sana mtaani huko wamechoka sasa pale wanajifanya wametulia ili wapate bwana wa kuzeeka naye, na wapo wale wanaomtafuta Mungu kabisa.
uzuri ni kwamba, Mungu huangalia moyo na wale wanaomtafuta kwa moto tu ndio huwa anaonekana kwao, wale wanaoigiza hurudi na maigizo yao na motoni wataenda. Biblia inasema nawapenda wale wanipendao na wale wanitafutao kwa bidii wataniona, pia inasema, nanyi mtanitafuta na kuniona mtakaponitafuta kwa mioyo yenu yote. Mungu hapatikani kirahisi rahisi tu mara ohh tushikane mikono tuombe sijui nini, tafuta Mungu kwa roho yako yote toka ndani ya kilindi cha moyo wako na chukia dhambi na kuikimbia, soma Neno la Mungu na uwe mtu wa maombi, hapo ndipo utakapo mwona.