KERO: Masanja Mkandamizaji kutumia Ulokole kinyume na maadili ya Kipentekoste

Ujue hadi sasa sijaona hayo maadili ya kipentekoste ktk bibilia, naomba msaada jamani
 
Swala la kuwakwaza wengine sio zuri ....
Tunafundishwa kuwa nakiasi ...tunaambiwa tusikae sana miongongoni na wenye mizaha
 
Acheni kutumika vibaya Mtumishi wa Mungu Masanja mbali ya uchungaji kazi yake nyingine ni msanii wa Commedy kwa hiyo msichanganye mambo. Sidhani hayo mavazi mnayoyalalamikia kama ni kweli lkn huwa anayavaa kanisani, mi ninachokiona wengi wenu hapa mnawivu na mafanikio yake, kwa sababu watu wa kwanza kulalamika kama kweli anakosea wangekuwa viongozi wake wa dini, wala sio nyie. kwa hiyo kwa ushauri wangu acheni majungu kama kweli nyie mmeokoka.
 
kuhusu utajiri wake sina shida kabisa naye, nina shida naye kwenye mavazi na mienendo yake, haiendsni na miiko ya Kikristo kabisa,na ni kama kajifichia kwenye ukristo li afanye yake. kiufupi anawaharibia walokole.


jamaa kaongea point ila kuna watu wanachukulia poa mavazi ni sehemu ya kuonesha heshima na uaminifu.

Huyo jamaa analima mpunga mbarali, na analima kibiashara sio kwa mazoea
 
wivu tena, au nawe ni mmoja wao?
 
Hakuna kitu kinaitwa mungu.

Amani ni fursa kwa wale wanaoujua ukweli kuwa hakuna mungu. Na ukiona unaitwa kwenye fursa basi jua wewe ndo fursa yenyewe
 
Mjasiliamali huyo.....anachangamkia fursa tu, kwenye vichekesho, uimbaji, kuhubiri, biashara, siasa kote yuko.....anatumia fursa!!
 
masanja kwa level za kuwa pastor/mchungaji inabidi kumchukua miaka mingi sana ili abadilike kwa sababu hata ukisikiliza mahubiri yake yamejaa vijembe, sasa watumishi wa Mungu kazi yao kubwa ni kuwaunganisha watu wawe jamii moja ya taifa la Mungu. lakini huyu jamaa utasikia akihubiri then anamchana mtu mala hata kwenye account huna hata sent mala hata marekani hujawahi kufika

hivyo basi anahiji mentorship kwa mda mrefu ili yale maumivu ya ndani aliyonayo yaishe kwa sababu ukisikia mahubiri yake unajua tu huyu ana maumivu ya ndani
 
Pale unapotafuta amani kwenye mavazi ya watu na sio kutoka kwa Mungu. Mnataka avae kizee na yeye ni pastor kijana?
 

Mbona kama una chuki binafsi vile. Lete mstari wa biblia unaoonyesha sheria za mavazi hasa ukiwa mlokole. Binafsi nilimuona mchungaji anavuta sigara. nikamuuliza mwanini anavuta sigara? Akanijibu hata kwenye biblia inasema fuata maneno yangu usifuate matendo yangu” nikaishiwa pozi.
 
ila masanja utajiri wake una ukakasi mwingi ngoja siku watamtolea uvivu

Jamani hivi mnjua biashara ngapi anafanya mashanja? Vijana fanyani kazi. Masanja ana mashamba ya mpunga kivao huko vijijini, ana kampuni ya ulinzi hapo Dar na vimgahawa hapo Dar plus na sadaka[emoji16] na alinza biashara kitambo
 
Yaani hujaelewa kweli kilichoandikwa au unajitia kichwa ngumu? Ukiambiwa wazinzi hawataingia mbinguni maana yake ni kwamba asiye mzinzi ni mbinguni direct?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…