KERO: Masanja Mkandamizaji kutumia Ulokole kinyume na maadili ya Kipentekoste

KERO: Masanja Mkandamizaji kutumia Ulokole kinyume na maadili ya Kipentekoste

Kama kinachoangaliwa ni roho sio mavazi,basi roho itakiwayo ndo ikae nje,na mavazi yakae ndani ili yasionekane,,kwani mavazi huiwakilisha roho
 
Kama kinachoangaliwa ni roho sio mavazi,basi roho itakiwayo ndo ikae nje,na mavazi yakae ndani ili yasionekane,,kwani mavazi huiwakilisha roho
Wee jamaa' kuna kitu kinaitwa wearing code
Kwann padri havai bukta?
Au sister kimini??
 
Gwajima hana kosa siasa na dini huwezi kuvitenganisha,ndo maana hata wanasiasa wanaombewa na na wachungaji
 
Unaweza ukavaa suruali bwaga kama gunia la mashineni lakini kama moyoni hakuna Mungu ni buree.
Ifact kuvaa milegezo na kusuka kweli inaweza ikatia mashaka ila kuvalia kama hapo kwenye picha sijaona sana ubaya
" Chakula ni kwa tumbo na tumbo ni kwa chakula lakini roho ni kwa Bwana"
waambie vijana waache ushamba, we live in the era of improvised generation, vitu kama hivyo ni kawaida, ulokole upo moyoni japo mavazi au tabia mbovu ni kumuaibisha Mungu wetu tuliembeba.

Masanja mbona anavaa kawaida sana....sijui kama mtoa mada amemuona K.Franklin aisee hasa akiwa jukwaani.

dunia inabadilika jamani.
 
waambie vijana waache ushamba, we live in the era of improvised generation, vitu kama hivyo ni kawaida, ulokole upo moyoni japo mavazi au tabia mbovu ni kumuaibisha Mungu wetu tuliembeba.

Masanja mbona anavaa kawaida sana....sijui kama mtoa mada amemuona K.Franklin aisee hasa akiwa jukwaani.

dunia inabadilika jamani.
4dd24e5c189affc3d759648738cccfb9.jpg


Tamaduni za wazungu tusizilete tusizilete huku, ki ukweli massanja mkandamizaji analichafua sana kanisa la Mungu, hivi mchungaji wa kondoo kweli anavaa hivyo?????? jamani tuacheni utani kwa Mungu.
 
mbona kavaa kawaida sana ,asee shetani anapambana
 
A
Leo nimeona picha ,yuko kwny ndege na binti mmoja,sasa jamaa akaanza kumhusisha mungu kweny mambo yake,anamsifia yule binti ni mzuri,na anamshukuru aliyepanga seat za ndege,huyu jamaa ni jipu
Anaenda kuhubiri kwa kswahili Marekani kila wiki na nyie hamjiongezi.Masanja piga kazi na mbavu zao zikikusogelea piga nazo na sembe kama kawa
 
MMEKUBALI KUTUMIKA ALIYEKUAMBIA MASANJA NI MCHUNGAJI NI NANI.YEYE YUPO HAPO KUENDELEA NA ZE COMEDY YAKE! KWANI WATOTO WAKIIGIZA KAMA BABA NI KWELI BABA.HAPO ANAIGIZA KAMA MCHUNGAJI NA NYIE MAZUZU MNATOA KIINGILIO BILA YA KUJUA KWA MOYO MWEUPE.YEYE HANA KOSA LOLOTE!!
Habari ya mda Huu..

Asilimia kubwa ya watu duniani wanaamini uwepo wa Mungu, na uwepo huu wa Mungu umeleta Imani tofauti tofauti za ambazo binadamu huziishi. Na Imani hizi zinaheshimiwa, wapo wenzetu waroma, wakatholiki, wapentekoste, kila imani inataratibu zake na miiko yake inayoheshimiwa na kila muumini wa dini hiyo.


Kwa upande wa wapentekoste, sote twajua namna miiko yao ilivyo hasa katika mavazi, tumeona kwa waroma tumeona kwa waanglikana, zaidi sana hata kwa wenzetu waislamu.Uwepo wa dini hizi umekuwa msaada sana kwa jamii hasa kuibadilisha jamii na hasa vijana kuwa na miiko na heshima.

Lakini siku za hivi karibuni, kumekuwepo na wimbi la vijana wanaokimbilia ulokole lakini matendo yao hayaendani na miiko ya kilokole, bika kupepesa pepesa kumekuwa na celebrity huyu anayefahamika kama "Massanja mkandamizaji" ama "Emmanuel Mgaya" huyu amekuwa akijiita PASTOR.

Kumekuwa na malalamiko mengi hasa toka wa vijana wakilokole wakilalamika mienendo ya celebrity huyu na mavazi yake yasiyoendana na miiko ya kilokole, ki ukweki kuna wakati ukimwona ni kama kijana mwingine tu wa mitaani, kuvaa mlegezo, kusuka nywele, kofia kuvalia nyuma, hivi haviendani na miiko ya kikristo.

Kwenye jamii inaonyesha picha kuwa Anajifichia kwenye mwamvuli wa kipentekoste ili hali si mpentekoste...sasa unamdanganya nani massanja? hata moyo wako ukushuhudie kuwa UNACHOKIFANYA HAKIENDANI NA MAADILI YA KIPENTEKOSTE, KUMBUKA WEWE NI KIOO NA NI MAARUFU, HIVYO EITHER UBADILI NAMNA UNAVYOVAA AU UACHE KUTUMIA ULOKOLE KAMA KIVULI CHA MAOVU!


Unaharibu Taratibu za kipentekoste!


Ujumbe huu ukufikie mahali pote ulipo
92395f03f88a62a17fe2ae4374070d17.jpg
 
Yaani hujaelewa kweli kilichoandikwa au unajitia kichwa ngumu? Ukiambiwa wazinzi hawataingia mbinguni maana yake ni kwamba asiye mzinzi ni mbinguni direct?
Mkuu nafkiri wewe pia unataka kuchanganya mafaili! Sijaelewa concern hasa ya swali lako kwangu,na cjui pia ni wapi nlipomaanisha hicho unachokisema!
 
Back
Top Bottom