Kero nilizokumbana nazo kwenye nyumba za kupanga

Kero nilizokumbana nazo kwenye nyumba za kupanga

Luqman mohamedy

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2016
Posts
899
Reaction score
1,231
Habari wanaJF,

Ama kweli ule usemi wa ukichoka kero za nyumba za kupanga jenga yako bado inaniumiza mpka leo kwa vitabia flani ivi vya kiswahili huku kwetu changanyikeni ambazo sizielewi.

Kwanza hapa naamini kuna watakaosoma hii article ni wapangaji wenzetu wenye tabia hizi.

(1)Utakuta wadada mnakaa kwenye mlango wa choo, na viti kabisa bila ata aibu mtu ukingia lazima uwapige vikumbo,na shughuli yako ndani unafanya kwa kujibana..ukizingatia hakuna bomba la maji chooni ambalo ungeweza kuzugia sauti kubwa kwa kulifungulia maji kwa kasi
Badilikeni jamani.

(2)Tabia ya kupiga story chini ya dirisha la mtu pia inanikera sana,mnatunyima faragha ndugu zetu wenye tabia hizo.

(3)Kuna watu ikifika zamu yao ya umeme wanarudi usiku mnene kimya kimya baada ya wapangaji wote kulala.

(4)Na wale wahuni mnaofungulia mziki kama viziwi mida mibovu tunaomba mtusamehe.

Wapo watakao ona kama hii ni misamiati hapo juu kwakuwa wanajifanya wakishua wamezaliwa masaki,wengine wamekulia bush na wengine mayahaya wanajifanya walishajenga..huku 70% hapa tumepanga[emoji28][emoji849]

Share kero zako mbili zilizowahi kukuta kwenye nyumba za kupanga..
 
Aisee namba 3 na 4 inakera sana...


Yaani suala la umeme linasumbua sana kuna watu ni wasumbufu mno kulipa hela ya umeme yaani ikifika zamu yao ni tafrani wanakulaza giza....

Alafu wafungua miziki nao ni shida unakuta mtu anafungulia mziki mnene usiku ukimfuata anakwambia yeye ndo starehe yake
 
Choo cha kulenga siyo poa ukidumbukiza lazima uruke hapa nikajiongeza niwe naenda kwa jiran mida ya usiku baada ya kama wiki mbili jamaa akashitukia kama kesho kutwa yake naenda nakuta kufuli daaa, nikaingia ndani nikapata akili nikachukua tissue nazitandika pemben ya tundu namalizia mzigo pembeni baada ya hapo nasindikiza na kiatu. jiran akabaki na kufuli lake.
 
Hilo swala rahisi sana mkuu jiulize kwenye familia yenu au nyingine unayoijua wapo wangapi na wangapi kati yao wamejenga?
Una marafiki wangapi wamejenga??
Na idadi ya nyumba za kupanga ni nyingi kuliko za binafsi..nyumba moja ina familia zaidi ya 5..hio 70 inaweza kuzidi mkuu.
Hiyo asilimia 70 umeipataje?
 
Kuna jamaa Kila akisex na Dem wake lazima tuzibe masikio maana demu NI full makelele mpaka mtaa wa 7 watajuwa Kama wanafanya mapenzi, mbaya zaidi wakimaliza wanafungulia sbufa mpaka bati linataka kung'oka, sometime huwa namhurumia jamaa mwenye watoto ambaye yupo jirani na chumba Cha huyo mpangaji
 
Wakati niko shuleni tulipanga geto moja na mwanangu tukawa tuna-share. Nyumba ilikua iko freshi japo ilikua ipo katika mazingira ya kiuswazi.

Kulikua na wapangaji wengine ambao asilimia kubwa walikua ni wanawake.

Kiukweli wale mademu walikua wazuri walionekana kutokea familia zile zakishua sana. Changamoto kubwa tu ambayo inanifanya nisiukumbuke hata uzuri wao ni pale walipoweka ngazi za chooni kua kijiwe chao cha stori

Kile kitendo kilinifanya nione kodi yangu kama naibiwa vile maana ilifikia wakati nilikua sifurahii kuishi maisha kwa kujibana kiasi kile.

Nikawa naenda chooni kwa timing yani mchana hunioni kwenda chooni ila ikifika midnight pale saa 8 usingizi umechanganya nikiwa nauhakika kua kila mtu kalala hapo mkushi ndio naibuka nanyata mdogo mdogo kuelekea eneo la penalt box

Nikiwa naendelea ku-uploads files kabla sija delete browser history katika hari ya taharuki nikastukizwa mlango umegongwa sauti ya kike inasema "mbona mlango mgumu hivi" kwa wakati ule na giza lile hakuwaza kua kutakua na mtu atayeweza kwenda chooni muda ule, hakujua niko ndani na nimeupiga komeo ya ndani kwa emergency kama hizi

Nami nikawa nimekula buyu kwasababu akijua tu kua ni mimi itakua msala kesho sitamuangalia hata usoni. Basi zile purukushani zake kuhangaika na mlango nikaona anadalili za kuwaalika wenzake wamsaidie.

Nikasema bora nusu shari kuliko shari kamili ikanibidi nijikoholeshe nikijua atasepa. Nikasikia "hii si sauti ya Scars jamani?"

Nikawa nimeishatolewa kwenye mchezo concentration zangu zote zikawa juu ya hii aibu ambayo iko mbele yangu. Ikanibidi ni kohoe tena nikasikia vishindo vya miguu vikitoka pale mlangoni nikajisemea bora kasepa na kesho nikimuona namlia buyu na akiniuliza ntabisha kua sio mimi

Baada ya dakika kadhaa natoka sasa nakuta amesimama mlangoni halafu taa inanipiga usoni...moyoni nikasema potelea mbali kama inakua wacha iwe tu
 
Back
Top Bottom