Wakati niko shuleni tulipanga geto moja na mwanangu tukawa tuna-share. Nyumba ilikua iko freshi japo ilikua ipo katika mazingira ya kiuswazi.
Kulikua na wapangaji wengine ambao asilimia kubwa walikua ni wanawake.
Kiukweli wale mademu walikua wazuri walionekana kutokea familia zile zakishua sana. Changamoto kubwa tu ambayo inanifanya nisiukumbuke hata uzuri wao ni pale walipoweka ngazi za chooni kua kijiwe chao cha stori
Kile kitendo kilinifanya nione kodi yangu kama naibiwa vile maana ilifikia wakati nilikua sifurahii kuishi maisha kwa kujibana kiasi kile.
Nikawa naenda chooni kwa timing yani mchana hunioni kwenda chooni ila ikifika midnight pale saa 8 usingizi umechanganya nikiwa nauhakika kua kila mtu kalala hapo mkushi ndio naibuka nanyata mdogo mdogo kuelekea eneo la penalt box
Nikiwa naendelea ku-uploads files kabla sija delete browser history katika hari ya taharuki nikastukizwa mlango umegongwa sauti ya kike inasema "mbona mlango mgumu hivi" kwa wakati ule na giza lile hakuwaza kua kutakua na mtu atayeweza kwenda chooni muda ule, hakujua niko ndani na nimeupiga komeo ya ndani kwa emergency kama hizi
Nami nikawa nimekula buyu kwasababu akijua tu kua ni mimi itakua msala kesho sitamuangalia hata usoni. Basi zile purukushani zake kuhangaika na mlango nikaona anadalili za kuwaalika wenzake wamsaidie.
Nikasema bora nusu shari kuliko shari kamili ikanibidi nijikoholeshe nikijua atasepa. Nikasikia "hii si sauti ya Scars jamani?"
Nikawa nimeishatolewa kwenye mchezo concentration zangu zote zikawa juu ya hii aibu ambayo iko mbele yangu. Ikanibidi ni kohoe tena nikasikia vishindo vya miguu vikitoka pale mlangoni nikajisemea bora kasepa na kesho nikimuona namlia buyu na akiniuliza ntabisha kua sio mimi
Baada ya dakika kadhaa natoka sasa nakuta amesimama mlangoni halafu taa inanipiga usoni...moyoni nikasema potelea mbali kama inakua wacha iwe tu