Kero: Tabia ya kurundika/kumiliki vitu vingi kuzidi uwezo wa kuvimudu au kuvitunza

Fuata ushauri wa daktari hivi Ina maana gani una ndoo za plastiki hamsini, majaba kumi mapipa matano familia ya watu sita na kisima cha maji unacho ebu badilika bwana๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚
Ni ushamba tu kufuatilia maisha ya wengine. Ulijuaje yalioko nyumbani kwake kama sio umbea na kufuatiliana.

Majirani wenyewe tunaonana kwenye vikao vya mwisho wa mwezi vya ulinzi, napata wapi muda wa kuhesabu ana ndoo ngapi na majaba mangapi, NI USHAMBA NA KUKOSA LA KUFANYA KUNAKUSUMBUA.
 
Huyu jamaa ana akili sana. Miaka 20 mbeleni huko, ukitaka kumuona lazima uombe kibali kwanza cha kumuona.
Hicho kiwanja kimoja atakuja kuuza hata milion 60.
Kipindi hicho utakuwa unawaambia watu huyu jamaa tulikuwa naye tunahangaika naye.
Kama una hela nunua hata viwanja 100. Usiwaze kimasikini ndugu
Njoo hapa mtaani kwangu kuna jamaa kila nikipita naye mahali utasikia na hiki ni kiwanja changu. Badala amalize kuendeleza kiwanja kimoja yeye amekazana tu kuongeza vingine, sasa kamahia kununua mashamba.
 
Mtoa uzi ndiyo wale watu wakiingia kwako wakakuta radio 3, anaomba moja.
Kuwa na vitu vingi raha sana. Una simu 3, moja ikipasuka kioo, unabeba nyingine na siyo unaanza kuhangaika kwenda kwa fundi au kununua simu nyingine.
Katika vitu ambavyo napenda ni muziki, kwahio ukikuta nina redio 3 ndani mwangu kaa kwa kutulia๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚
 
Umewaza kimasikini sana. Huyo jamaa ana akili sana. Baada ya miaka 20 mbeleni hautaweza hata kupiga naye story.
Duh! Hii hatari sana, inaweza kufikia kipindi akashindwa kuvimudu ata kupalilia majani.
kitu muhimu ni kuwekeza nguvu kwenye kuvimalizia halafu ndio aongeze viwanja vya ziada.
 
Nitajitahidi nipunguze๐Ÿ˜‚
 
Hawa hayo majaba
 
Hii hapa siku hizi tumepunguza sana maana gharama za ujenzi zimeongezeka bila kiasi.

Tumeshaelewa kwamba watoto wakiondoka nyumbani basi linabaki behewa tu ambalo siku hizi hata ndugu wa vijijini huwa hawaji tena kulijaza.
 
Aiseee

Ila kila mtu aishi aonavyo inamfaa
 
Embu funguka kidogo mbona mimi nagawa nguo zangu kila kukicha? Zingine natuma kijijini maninti wanao msaidia mama anawagawia? Nguo nyingine nawatumia wifi zangu. Watoto wa ngugu zangu wa kike almost wote washavaaga nguo zangu embu funguka kidogo maana ninahisi kuna kitu hakiko sawa.
 
Na pia kuna hili la kuhifadhi vitu vya marehemu hata kama havitumiki.

Hii ni hasa kwa wale waliofiwa na baba/mama zao, huwa wanahisi wakivitupa/kuuza au kugawa marehemu atajiskia vibaya.
 
Kuna wale wanamiliki simu nne...nyingine kaziweka chumbani tu..
na hao naona wapitie uzi huu
Wacha kunichekesha nimekumbuka siku moja nilikuwa Airport wakati wa ugakuguzi ile tunaingia ndani, mbele yangu alikuwepo mkaka sijawahi ona alikuw na vifu vifuatavyo,

1: simu kubwa 2 na tablet kuubwa mkono jumla tatu
2: shingoni sasa micheni kama minne hivi, kuzidi ile ya harmonise.
3. Peteee jamani vidole vyote 10 nadhani viwili ndo havikuwa na peteee
4. Bonge la saa mkono wa kushoto
5. Mkono wa kulia kama kibangili cha gold
6, kavaa simple tu nguo
7. Na begi moja la wastani.

Nyie watu yule kaka kuvua vile vitu kuviweka kwenye kile ki sahani na kuzunguka kule mbele kuvipokea ilichukuwa nusu saa almost.
Hiyo siku ndo nilijuwa kwa nini Airport waliweka masaa mawili ya ku report kabla ya kuondoka.

Kila mtu kwenye line pale alichungulia mbele kuona kwanini watu hawasogei? Mkaka kabebelea mavitu kuzidi hata sisi wanawake? Hapana ni kerooo.
 
Bora unaewapa ndugu,mi watu Baki walinijibu vibaya
 
Mtoa uzi ndiyo wale watu wakiingia kwako wakakuta radio 3, anaomba moja.
Kuwa na vitu vingi raha sana. Una simu 3, moja ikipasuka kioo, unabeba nyingine na siyo unaanza kuhangaika kwenda kwa fundi au kununua simu nyingine.
Na hio inasaidia sana mkuu, juzi nimepigwa Iphone nimepekua kabati nimeibua ka Sony kangu ka mwaka 2017 nakatumia now ๐Ÿ˜…๐Ÿ˜…๐Ÿ˜…
 
Ungetuambia kilichokupata nasi tuchukue tahadhari mkuu. Mimi bado ninagawa nguo kwa ndugu zangu lakini.
 

Sisi bado ni wajima. Ndiyo maana nyumba nyingi hazipendezi hata kama ni ya kisasa. Hatujui kufanya nyumba ipendeze.
Wenzetu huko mbele hadi wana kampuni maalumu za kurudisha makazi katika ubora wake. Mtu akishazidiwa na mikorokocho anawakodi jamaa. Utaona hata vitu vya mitumba, si kwamba wanatuhurumia saaana bali ni kusafisha makazi yao. Sisi ndiyo jalala lao. Imagine tunaletewa hadi vyombo vya jikoni na vya kulia vya mtumba. Sasa unavinunua,unajaza home kwako.
Mada hii iendane na ununuzi wa vitu rahisirahisi mradi tu kujaza nyumba. Mfano,mavyombo ya plastiki kibao. Hii ni akili mbovu.

Asante kwa mada nzuri
 
Tatizo kubwa tunafanya vitu kwa tamaa!
Ukiona mtu X ana masofa unataka nawewe uwe na sofa kama hizo. Ukiona kochi zuri na we unataka kununua.
Mwisho wa siku unakua na vyote, rangi tofauti nyumba inakosa mvuto.
Nyumba inatakiwa iwe mahali pa kuleta faraja baada ya purukushani za siku nzima.
Unakua na fenicha ambazo hazina kazi maalumu, zinajaza nafasi na kukuongezea gharama ya kuzitunza.
Ukiwa na dada wa kazi unataka afanye usafi wa kila kitu, dada kuanzia asubuhi yuko busy majukumu yanakua mengi sana. (Madada wengi wanakimbia sababu ya mazingira ndani ya nyumba).
Mpangilio wa nyumba ukiwa mbaya ata shughuli zako zitakua hazikai sawa.
Kuna uhusiano mkubwa kati ya mpangilio wa nyumba na umakini wa kufanya vitu.
 
Unaweza kuta mleta mada ni jinsia me na tabia ni jinsia ke.

Iweje ukwazike kwa mali alizotafuta mwenzako kama anarundika hana kazi navyo muache ni mali zake hajaiba hajakuomba wala hakupunguzii kitu yeye kumiliki vitu asivyotumia.

Nasikitika kuona watu wanacomment kuhusu umiliki wa ardhi wakati ardhi ni mali haiozi na hata asiooweza kuiendeleza haina madhara kwakua ni yake atajua atafanyia nini anaekosoa mtu kuwa na ardhi au viwanja vingi basi huyo hana hata uchochoro anaomiliki
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn moreโ€ฆ