Wacha kunichekesha nimekumbuka siku moja nilikuwa Airport wakati wa ugakuguzi ile tunaingia ndani, mbele yangu alikuwepo mkaka sijawahi ona alikuw na vifu vifuatavyo,
1: simu kubwa 2 na tablet kuubwa mkono jumla tatu
2: shingoni sasa micheni kama minne hivi, kuzidi ile ya harmonise.
3. Peteee jamani vidole vyote 10 nadhani viwili ndo havikuwa na peteee
4. Bonge la saa mkono wa kushoto
5. Mkono wa kulia kama kibangili cha gold
6, kavaa simple tu nguo
7. Na begi moja la wastani.
Nyie watu yule kaka kuvua vile vitu kuviweka kwenye kile ki sahani na kuzunguka kule mbele kuvipokea ilichukuwa nusu saa almost.
Hiyo siku ndo nilijuwa kwa nini Airport waliweka masaa mawili ya ku report kabla ya kuondoka.
Kila mtu kwenye line pale alichungulia mbele kuona kwanini watu hawasogei? Mkaka kabebelea mavitu kuzidi hata sisi wanawake? Hapana ni kerooo.