KERO: WAKAZI WA MBALIZI HATUNA MAJI: TUNAOMBA UFAFUNUZI KUTOKA IDARA HUSIKA.

KERO: WAKAZI WA MBALIZI HATUNA MAJI: TUNAOMBA UFAFUNUZI KUTOKA IDARA HUSIKA.

Travis_Kitengo

JF-Expert Member
Joined
May 19, 2021
Posts
329
Reaction score
919
Habari wana JF,

Bila kupoteza muda sisi wakazi wa mbalizi centre mitaa yake hadi huku Ifisi tuna changamoto kubwa sana ya maji!

Kabla ya ziara ya Mheshimiwa Makamo w Raisi tulikaa takribani mwezi mzima hakuna hata tone la maji kutoka Idara ya Maji. Siku moja kabla ya Ujio wa Mheshimiwa maji yalianza kutoka na yaliendelea kutoka siku zote ambazo Mheshimiwa Makamo wa Raisi alikuwepo hapa jijini.

Baada ya Mheshimiwa kuondoka shida ikaanza tena kama kawaida!

Kama wananchi tunauliza hawa Idara ya Maji, Kipindi Mheshimiwa amekuja Mbeya yale maji mliyotoa yalitoka wapi kama mnasingizia kuna Ukame? Au kuna sehemu mnayapeleka kwa wenye nacho sisi walala hoi mnatuacha tujifie na ukame ?

Kama kuna upungufu wa maji kwa nini msiweke ratiba ya magao wa maji kwa mitaa ili kama yapo machache tushare hayo hayo machache yaliyopo?

Je, wakuu wa vitengo idara ya maji mnahisi mnastahili kuwepo kwenye ofisi zetu za umma?

Inasikitisha sana kutoka 1961 mpaka leo hii 2026 tunahangaika na shida ya maji!
 
Back
Top Bottom