Kero ya kuripoti kazini baada ya kupangiwa ajira na sekretarieti ya ajira, halafu unaambiwa urudi nyumbani mpaka upigiwe simu kuitwa!

Naomba nieleweke: Mimi sikatai mtu kuambiwa asubiri taratibu za ajira zikamilike na aingizwe kwenye pay roll ya saerikali. Ninachokataa ni mtu kutokulipwa gharama ya nauli aliyotumia kuitikia wito wa kuripoti ndani ya siku 14, na pia kutokulipwa nauli ya kurudi nyumbani akasubirie taratibu za kukamilisha ajira. Hiyo imesababisha watu wateseke mjini!! Safari ya kuitikia wito ni rasmi lazima ilipwe kikamilifu kwa mujibu wa taratibu za serikali!! Huko nyuma hata kuja kwenye usaili ilikuwa unarudishiwa nauli na posho ya siku angalau mbili kwenye kituo cha usaili. Sisemi ifanyike hivyo sasa lakini hata la kuitikia wito rasmi wa ajira mtu asilipwe!!! Hapana huu ni uhuni!!
 
Embu nukuu wewe hiyo standing order tuisome hapa wote...
 
Ukisharipoti ni ajira imekamilika. Hizo ni taratibu tu.
Ilipaswa kumpa hata barua kuwa ameripoti na sasa wanakamilisha taratibu nyingine arudi tarehe fulani.
😂😅 sasa mbona unajichanganya mwenyew tena... Unapewa vipi barua wakat tayar ulipata barua ya ajira... Halafu sasa ukitaka twende kwa utaratibu basi yeye ndiye alipaswa kuandika barua ya kukiri kufika kituoni na kuruhusiwa kurudi nyumban kusubiri taratibu nyingine za kikazi... Vijana msi complicate mambo ya kiserikali hayahitaji papara, by the way hakuna wa kuwazurumu stahiki zenu...
Zamani watu walikua wanaripoti kituoni na wanalipwa stahik za muhimu kama nauli na pesa za mizigo kusafirisha utokapo, tatizo likaja kuonekana wengi hawarudi tena... Anyways all in all kuweni wapole
 
Kukiwa hakuna ajira kelele mkipata kelele. Mama kanyaga twende
Hujitambui
 
Ukipata placement kitu Cha muhim ni kwenda kuripoti kituo Cha KAZI. Taratbu za vyeti zikiisha inabidi urudi ulikotoka na uendelee kutafta pesa zako had utakapopigiwa simu. Kuna watu hikaa hata mwez mzma na sehm Kisha ndo wanapigiwa simu.

Na huo ndio mfumo ulivo.
 
Mimi nadaigi ela yangu ya kujikimu mpk leo na sina matumaini ya kulipwa na nikifanya over price wananishikia bango wakati mm najitafutia pesa yangu ya kujikimu ambayo sijalipwaga
 
Embu nukuu wewe hiyo standing order tuisome hapa wote...
Naona naongea na mtu anayedai anajua taratibu kumbe hata standing order zinazoongoza kwenye utumishi hana habari nazo na hajui mahali pa kuzipata!
 
Kukiwa hakuna ajira kelele mkipata kelele. Mama kanyaga twende
Watu wateseke wasiseme au?. We waweza kuwa n miongoni mwa watesaji wa vjana wa watu!. Wapeni vjana wa watu posho zao zikawasaidie kuanza maisha.
 
Kumbe alisikika mpumbavu mmoja HR; nlifikiri n ww ulokuwa unaongea pumba.
 
Nimwombe mama Samia alifuatilie hili maana ni mateso makubwa wanayoyapitia waajiriwa wapya usione wamekaa kimya!!
Bora hata tumseme waziri husika, hivi mama/rais atafanyia vitu vingapi vidogo vya namna hii, hata km rais ni taasisi, lakini mengine yanapswa kuishia wizara husika.
 
Mfumo wa wapi huo?. Subsistance allowance inakuwa inafanya kazi gani au ni kutokana na kutokuelewa kanuni za utumishi wa umma hivyo unataka kuaminisha umma kuwa ndivyo ilivyo?.
 
Nchi wa wasiojitambua hii Mambo ya kukaa online eti una hakiki Sasa una hakiki Jambo gani? It about outodated regime
 
Mimi yalinikuta kwenye ofisi Moja za mamlaka Fulani nilipo riport TU wakaniambia tutakuita baada ya week Moja ,ukapita mwezi nikaenda na suruali nyeusi na shati zuri la chama Cha mapinduzi na kofia,nilipowauliza na majibu hayaeleweki nikaenda office za CCM mkoa nikaonana na mwenyekiti wa ccm.Kesho yake nilipigiwa simu ni riport mapema na nilionyeshwa ofisi yangu nikapiga miaka 4 nikapata internal transfer .
 
 Kawafungulie mashtaka kwenye ofsi za kazi zipo Kika wilaya.
 
Taasisi nyingi ukiripoti ndo wanachukua vyeti vyako wanapeleka necta kuhakiki.. baada ya hpo ndo uingizwe kwenye payroll.. so taasisi hiz muda huu wanapenda kukuambia urudi watakuita hadi watakapoona tayari umeingizwa Kwa payroll na uhakiki umekamilika... Taasisi zenye uwezo wanaweza kukuretain ubaki huku wakikusuprt kidogo, zingne wanaona huo ni mzigo so nenda tutakuita.. ni vizuri Pia kuomba maelezo kwanin urudi nyumbani wakati ndo umeripoti???usikae kimyaaa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…