Kero ya kuripoti kazini baada ya kupangiwa ajira na sekretarieti ya ajira, halafu unaambiwa urudi nyumbani mpaka upigiwe simu kuitwa!

Kero ya kuripoti kazini baada ya kupangiwa ajira na sekretarieti ya ajira, halafu unaambiwa urudi nyumbani mpaka upigiwe simu kuitwa!

Naomba nieleweke: Mimi sikatai mtu kuambiwa asubiri taratibu za ajira zikamilike na aingizwe kwenye pay roll ya saerikali. Ninachokataa ni mtu kutokulipwa gharama ya nauli aliyotumia kuitikia wito wa kuripoti ndani ya siku 14, na pia kutokulipwa nauli ya kurudi nyumbani akasubirie taratibu za kukamilisha ajira. Hiyo imesababisha watu wateseke mjini!! Safari ya kuitikia wito ni rasmi lazima ilipwe kikamilifu kwa mujibu wa taratibu za serikali!! Huko nyuma hata kuja kwenye usaili ilikuwa unarudishiwa nauli na posho ya siku angalau mbili kwenye kituo cha usaili. Sisemi ifanyike hivyo sasa lakini hata la kuitikia wito rasmi wa ajira mtu asilipwe!!! Hapana huu ni uhuni!!
 
Taratibu za serikali nazijua sana!! Mimi ni mumishi wa umma mstaafu!! Niliajiriwa katika utumishi wa umma mwaka 1986 baada ya kuhitimu chuo kikuu cha Dar, na nimestaafu mwaka 2019!! Kinachofanyika sio taratibu za utumishi wa umma bali uhuni. Taratibu za utumishi wa umma zinaongozwa na Government standing orders toleo la 2009 na marekabisho yake ya mwaka 2011!! Huo utaratibu wa mtu kuripoti kazini kwa wito rasmi halafu unarudishwa nyumbani bila kuhudumiwa kwa lolote ni uhuni wa watu!! Naomba unukuu hapa waraka wowote rasmi wa serikali unaoelekeza hivyo!!
Embu nukuu wewe hiyo standing order tuisome hapa wote...
 
Ukisharipoti ni ajira imekamilika. Hizo ni taratibu tu.
Ilipaswa kumpa hata barua kuwa ameripoti na sasa wanakamilisha taratibu nyingine arudi tarehe fulani.
😂😅 sasa mbona unajichanganya mwenyew tena... Unapewa vipi barua wakat tayar ulipata barua ya ajira... Halafu sasa ukitaka twende kwa utaratibu basi yeye ndiye alipaswa kuandika barua ya kukiri kufika kituoni na kuruhusiwa kurudi nyumban kusubiri taratibu nyingine za kikazi... Vijana msi complicate mambo ya kiserikali hayahitaji papara, by the way hakuna wa kuwazurumu stahiki zenu...
Zamani watu walikua wanaripoti kituoni na wanalipwa stahik za muhimu kama nauli na pesa za mizigo kusafirisha utokapo, tatizo likaja kuonekana wengi hawarudi tena... Anyways all in all kuweni wapole
 
Haiwezekani kukubaliana na uonevu eti kwa kuwa tu umepata ajira!! huu ni utumishi ni utumishi wa umma na haikubaliki watu kujifanyia utaratibu unaonyanyasa na kutesa watu!! Mtu aliitwa kwa vitisho kuwa ukichelewa nafasi yako atapewa mwingine! lakini alivyoripoti bado anazungushwa, hilo halikubaliki!
Kukiwa hakuna ajira kelele mkipata kelele. Mama kanyaga twende
Hujitambui
 
Ukipata placement kitu Cha muhim ni kwenda kuripoti kituo Cha KAZI. Taratbu za vyeti zikiisha inabidi urudi ulikotoka na uendelee kutafta pesa zako had utakapopigiwa simu. Kuna watu hikaa hata mwez mzma na sehm Kisha ndo wanapigiwa simu.

Na huo ndio mfumo ulivo.
 
Mimi nadaigi ela yangu ya kujikimu mpk leo na sina matumaini ya kulipwa na nikifanya over price wananishikia bango wakati mm najitafutia pesa yangu ya kujikimu ambayo sijalipwaga
 
Embu nukuu wewe hiyo standing order tuisome hapa wote...
Naona naongea na mtu anayedai anajua taratibu kumbe hata standing order zinazoongoza kwenye utumishi hana habari nazo na hajui mahali pa kuzipata!
 
Naomba nijibu kama ifuatavyo....unakuwa bado hujaingizwa kwenye mfumo, na mpaka uingizwe kwenye mfumo anaweza kuchukua mwezi au ndani ya miezi miwili ili upate mshahara wako, ili upate mshahara wako inabidi utumishi wa approve taarifa zako, kwa kuzikagua kiundani ili tusipate udanganyifu......kwa kuwa hakuna bajeti Yako ya kujikimu kwa mda ule,ndio maana tunakwambia kuwa kakae kwanza nyumbani mpaka tukupigie simu....jamani sio kwa ubaya,maana hakuna wa kukulisha hapa mjini.....kama hamuamini kawaulize walimu wanavyopata ajira,wanakaa zaidi ya mwezi ndio wanaingiziwa mshahara wao..muda wote huwa wanahudumiw na wakuu wa shule mpaka wanapopata mishahara Yao kwa mara ya kwanza.....alisikika HR mmoja wa michango.
Kumbe alisikika mpumbavu mmoja HR; nlifikiri n ww ulokuwa unaongea pumba.
 
Nimwombe mama Samia alifuatilie hili maana ni mateso makubwa wanayoyapitia waajiriwa wapya usione wamekaa kimya!!
Bora hata tumseme waziri husika, hivi mama/rais atafanyia vitu vingapi vidogo vya namna hii, hata km rais ni taasisi, lakini mengine yanapswa kuishia wizara husika.
 
Ukipata placement kitu Cha muhim ni kwenda kuripoti kituo Cha KAZI. Taratbu za vyeti zikiisha inabidi urudi ulikotoka na uendelee kutafta pesa zako had utakapopigiwa simu. Kuna watu hikaa hata mwez mzma na sehm Kisha ndo wanapigiwa simu.

Na huo ndio mfumo ulivo.
Mfumo wa wapi huo?. Subsistance allowance inakuwa inafanya kazi gani au ni kutokana na kutokuelewa kanuni za utumishi wa umma hivyo unataka kuaminisha umma kuwa ndivyo ilivyo?.
 
Nchi wa wasiojitambua hii Mambo ya kukaa online eti una hakiki Sasa una hakiki Jambo gani? It about outodated regime
 
Inawezekanaje watu wapange utaratibu ambao siyo rafiki kwa waajiriwa wapya? Iko hivi: Ukipangiwa ajira na sekretarieti ya ajira kwa maana ya kufaulu usaili, unapewa barua ya kuripoti kazini ndani ya siku 14 vinginevyo nafasi yako atapewa mwingine! Hii inmfanya mwajiriwa atafute nauli hata kwa kukopa toka huko aliko na kusafiri hadi kituo alichopangwa. Akifika huko wanakagua vyeti vyake halisi, na kujaza taarifa zake binafsi kisha huambiwa RUDI NYUMBANI NA TUKIKAMILISHA TARATIBU ZA AJIRA TUTAKUITA KWA SIMU!! Hapo wameshamaliza na unatoka ofisini bila hata senti moja! Hawajali utalala wapi na utakula wapi na usalama wako ni upi! na utasafiri vipi na utarudi tena vipi!! Niliposikia kwa mara ya kwanza kwa mtu aliyekuwa amepangiwa halmashauri moja huko tabora sikuamini kuwa huo ndio utaratibu!! Nilifikiri ni roho mbaya tu ya wahusika huko halmashauri ya tabora!! Juzi juzi kuna dogo alipata nafasi katika moja ya manispaa za Dar. Naye aliporipoti alipokelewa na kukaguluiwa vyeti vyake na kujaza fomu za personal particulars na kuambiwa arudi hadi atakapopigiwa simu! Ni wiki nimepita sasa na bado hajapigiwa simu na anajibanza tu kwa watun na hajui hadi lini!! Huu utaratibu una usumbufu sana!! Ninachofahamu watu huitwa wakati serikali imeshafanya maandalizi tayari ya kuwapokea na kuwahudumia!! Yaani kijana amesota na interview kibao kwa gharama kubwa sana ya nauli, malazi na chakula, sasa ameitwa kwenye ajira bado anasoteshwa! Niwaulize nyie mnaowafanyia hivyo wenzenu mnajua masaibu wanayopambana nayo wanaposubiria? Wengine wanalala kwenye vituo vya mabasi kwa kukosa pesa za gesti na nauli ya kurudi tena nyumbani hawana! Tafadhali angalau siku wanaporipoti wapeni zile posho za kujikimu zilizopo kisheria ili ziwalinde wanaposubiria!
Mimi yalinikuta kwenye ofisi Moja za mamlaka Fulani nilipo riport TU wakaniambia tutakuita baada ya week Moja ,ukapita mwezi nikaenda na suruali nyeusi na shati zuri la chama Cha mapinduzi na kofia,nilipowauliza na majibu hayaeleweki nikaenda office za CCM mkoa nikaonana na mwenyekiti wa ccm.Kesho yake nilipigiwa simu ni riport mapema na nilionyeshwa ofisi yangu nikapiga miaka 4 nikapata internal transfer .
 
 Kawafungulie mashtaka kwenye ofsi za kazi zipo Kika wilaya.
 
Inawezekanaje watu wapange utaratibu ambao siyo rafiki kwa waajiriwa wapya? Iko hivi: Ukipangiwa ajira na sekretarieti ya ajira kwa maana ya kufaulu usaili, unapewa barua ya kuripoti kazini ndani ya siku 14 vinginevyo nafasi yako atapewa mwingine! Hii inmfanya mwajiriwa atafute nauli hata kwa kukopa toka huko aliko na kusafiri hadi kituo alichopangwa. Akifika huko wanakagua vyeti vyake halisi, na kujaza taarifa zake binafsi kisha huambiwa RUDI NYUMBANI NA TUKIKAMILISHA TARATIBU ZA AJIRA TUTAKUITA KWA SIMU!! Hapo wameshamaliza na unatoka ofisini bila hata senti moja! Hawajali utalala wapi na utakula wapi na usalama wako ni upi! na utasafiri vipi na utarudi tena vipi!! Niliposikia kwa mara ya kwanza kwa mtu aliyekuwa amepangiwa halmashauri moja huko tabora sikuamini kuwa huo ndio utaratibu!! Nilifikiri ni roho mbaya tu ya wahusika huko halmashauri ya tabora!! Juzi juzi kuna dogo alipata nafasi katika moja ya manispaa za Dar. Naye aliporipoti alipokelewa na kukaguluiwa vyeti vyake na kujaza fomu za personal particulars na kuambiwa arudi hadi atakapopigiwa simu! Ni wiki nimepita sasa na bado hajapigiwa simu na anajibanza tu kwa watun na hajui hadi lini!! Huu utaratibu una usumbufu sana!! Ninachofahamu watu huitwa wakati serikali imeshafanya maandalizi tayari ya kuwapokea na kuwahudumia!! Yaani kijana amesota na interview kibao kwa gharama kubwa sana ya nauli, malazi na chakula, sasa ameitwa kwenye ajira bado anasoteshwa! Niwaulize nyie mnaowafanyia hivyo wenzenu mnajua masaibu wanayopambana nayo wanaposubiria? Wengine wanalala kwenye vituo vya mabasi kwa kukosa pesa za gesti na nauli ya kurudi tena nyumbani hawana! Tafadhali angalau siku wanaporipoti wapeni zile posho za kujikimu zilizopo kisheria ili ziwalinde wanaposubiria!
Taasisi nyingi ukiripoti ndo wanachukua vyeti vyako wanapeleka necta kuhakiki.. baada ya hpo ndo uingizwe kwenye payroll.. so taasisi hiz muda huu wanapenda kukuambia urudi watakuita hadi watakapoona tayari umeingizwa Kwa payroll na uhakiki umekamilika... Taasisi zenye uwezo wanaweza kukuretain ubaki huku wakikusuprt kidogo, zingne wanaona huo ni mzigo so nenda tutakuita.. ni vizuri Pia kuomba maelezo kwanin urudi nyumbani wakati ndo umeripoti???usikae kimyaaa
 
Back
Top Bottom