Kero ya kusubirishwa kupisha msafara ya viongozi barabara za mikoani haivumiliki hakika viongozi mnatuumiza sana kwa hili

Kero ya kusubirishwa kupisha msafara ya viongozi barabara za mikoani haivumiliki hakika viongozi mnatuumiza sana kwa hili

Hili suala la viongozi kufunga barabara linaboa sana. Leo Kimara asubuhi masaa 3 na mchana huu masaa 3 tunasubiri kiongozi ambaye alikua na ziara zake huko kibaha.

Napendeleza yafuatayo

1. Serikali iwe inatoa taarifa siku moja kabla kwamba barabara itafungwa kwa muda wa masaa fulani ili wananchi wajue na watafute njia nyingine za kupita.

2. Watumie hata helkopta badala ya magari hasa kwa safari za mijini.

Baadhi ya watu leo hawaja fanya kazi kwa sababu ya kufungwa kwa barabara.
kiongozi gani huko kibaha wakati serikali yote iko kwenye mkutano Dodoma
 
Hakika huu ni UNYAPARA mambo leo!

Barabara za mikoani kila kuchwao zinapitiwa na kila aina ya binadamu;
  • Wenye afya na wagonjwa wote wanategemea barabara hiyo hiyo.
  • Wazima na maiti wote wanapitidhwa hapo
  • wenye haraka na wasiyo na haraka
  • Wenye bidhaa za kuoza na zisizo oza
  • Wenye pesa ya kula na wasiyo na akiba ya kula..
  • Madakitari na waganga
Kungandishana barabarani kupisha msafara wa viongozi hakika inaumiza sana!
  • Viongozi kwa hili Mnaharibu sana ratiba za watu,
  • mnaharibu sana bajeti za watu
  • Mnakwamisha matukio mengi sana ya watu
  • Mnapanda mbegu ya chuki pasiposababu ya msingi
  • Punguzeni Unyampara huu!
Pendekezo!
  1. Mnaonaje viongozi mkapanda ndege halafu magari yenu mkayakuta huko?
  2. Mnaonaje mkatoa japo taarifa siku moja kabila ili watu watafte mbadala wa safari?
  3. Mnaonaje mkatumia hata elkopita ili kuepusha acha kwa binadam wenzenu
Viongozi msichokijua ni hiki
Huenda sheria na kanuni za PSU/ task force zipo vizuri, lakini utekelezaji wa trafiki huko barabarani unafanyika kwa uoga ili kurinda kibarua!

Yamkini inatakiwa dakika 10-15 za kusubilia kiongozi! LAKINI TRAFIKI HUKO BARABARANI RTO/DTO huwa wanaamua kuwagandisha watu (2~3)hrs KWA HOFU TU ya kulinda kazi wakati kiongozi hata bado hajaamka!

EBU FIKILIENI
Kuna watu wanatoka mikoa ya mbali sana anapogandishwa 3hrs ni hasara kubwa sana.
(Mnachokifanya ni sawa na Uhujumu uchumi wa wanaichi wenu wenyewe)

Viongozi tambueni huko barabarani Kuna watu wanawahisha dawa za mgonjwa ambazo yamkini zikiwahi saa moja tu mgonjwa angepona, lakini hufariki kwa sababu ya misafara yenu!

Nitoe RAI kwa Viongozi na wale PSU fuatilieni zile ODA mnazowapa Trafiki wafunge njia! Hakikisheni Zinajali mda!

Wapeni updates ya misafara yenu matrafiki huko barabarani ili wafanye kazi kwa weledi! Kuna trafiki huko barabaranj huwa hata hawajui Exactly estimate ya msafara hadi hudiliki kutumia simu zao kupiga simu kwa wenzao!

Tunaomia ni RAIA! Viongozi na PSU tunaomba hili mliangalie Upya!
Mlipoamua kuwa magaidi hamkujua shida itawarudia nyie wenyewe, wananchi wa Tanzania mmekua watu wa hatari sana hamfai kuishi maeneo ya viongozi.
 
Uk.jpg
 
Back
Top Bottom