KERO Kero ya kuunganishiwa Umeme REA Igonyamu, Mbeya DC

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Naomba kuwasilisha kero yangu inayohusu kuunganishwa kwa umeme wa REA Kijijini kwetu IGONYAMU KATA YA IWINDI MBEYA DC.

Baada ya mda mrefu wa kusubiri kuunganishiwa umeme kijijini kwetu na wanakijiji kujitolea kuchimba mashimo na kubeba na kusimika nguzo kwa umbali mrefu kwa nguvu ya wanakijiji.

Kinachoshangaza baadhi ya kaya zinaachwa bila kuwekewa nguzo kwa karibu ili kuvuta umeme
Mkandarasi amekuja na nguzo chache kwanini.?

Naomba utusaidie kupaza sauti kuhusu hili jambo.
 
Habari, ndugu mteja.

Kwanza, tunaomba radhi kwa kuchelewa kukupatia mrejesho kuhusu suala lako.

Tunaomba utupatie muda ili tufanye ufuatiliaji wa changamoto yako na kukupatia mrejesho sahihi haraka iwezekanavyo.

Tunaomba uvumilivu wako wakati tukilifanyia kazi suala hili.

Asante. ^CM
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…