KERO Kero ya michango tunayokumbana nayo Wazazi wa Wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Mbagala Kuu

KERO Kero ya michango tunayokumbana nayo Wazazi wa Wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Mbagala Kuu

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Kero yangu inahusu shule ya sekondari Mbagala Kuu iliyopo Manispaa ya Temeke. Kila mara shule hii imekuwa ikiwataka wazazi kuchangia fedha kwa ajili ya mitihani ya majaribio.

Kwa mfano, wazazi tulichangishwa Shilingi 2,000 kwa ajili ya Mock Kidato cha pili, na sasa tumeombwa tena kuchangia Shilingi 2,000 kwa ajili ya mitihani ya Pre-NECTA kwa wanafunzi wa Kidato cha nne na cha pili.

Nimefuatilia shule nyingine za serikali zilizopo Temeke na kubaini kuwa wazazi hawafanyiwi michango kama hii. Naomba kufahamu kama uongozi wa shule hii una mamlaka ya kuanzisha michango hiyo bila ushauri au idhini kutoka mamlaka husika.

Pia, kuna malalamiko kuwa wanafunzi wanaoshindwa kutoa michango hiyo huadhibiwa kwa kuchapwa. Tunaomba mamlaka husika zifuatilie suala hili, kwani michango holela inaongeza mzigo kwa wazazi na inaweza kuathiri ustawi wa wanafunzi.

Serikali tayari imetenga fedha kwa ajili ya shughuli za kitaaluma; hivyo tunaomba matumizi ya fedha hizo yasimamiwe vizuri ili wazazi wasibebeshwe gharama zisizo za lazima.
 
2000 inakutoa roho. Hiyo mitihani wamefanya au hawajafanya? Huwa unahudhuria vikao vya wazazi shuleni?

Walimu wamejiongeza ili kumpatia mwanao ufaulu bora ziadi kwa kumuandalia mazoezi/mitihani mingi na ya mara kwa mara, as practice makes perfect.
 
Hiyo shule ilikuwa ya kwanza kiwilaya mitihani ya advance kama sikosei wakiwashinda hadi shule za private temeke kabla ya kulaumu tuwape maua Yao kwanza
 
Wazazi mna nongwa sana aisee.

Kwamba unahisi walimu wanaila na kuifaidi vilivyo buku mbili yako??

Je hiyo mitihani mwanao huwa anafanya au hafanyi?
Unafatilia maendeleo ya mwanao shuleni?
Buku mbili unataka mamlaka ziingilie kati, unaweza mnunulia mwanao kitabu cha 15k kweli??
 
Hivi kwa miaka ya sasa unadhani elimu ni rahisi kiasi hicho? Yaani elfu 2 unalalamika? Kwa akili hizi O-level utaweza kumnunulia vitabu vya elfu 30 mpaka 40 kwa kitabu kimoja?
 
Hamishia mwanao shule yenye hawachangishi michango.
 
Back
Top Bottom