KERO Kero ya Wanafunzi kulazimishwa kusoma tuition shule za Serikali

KERO Kero ya Wanafunzi kulazimishwa kusoma tuition shule za Serikali

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Habari wana Jamii Forums,

Naomba kuwasilisha hii kero kwa umma na taarifa hizi zifike TAMISEMI na Wizara ya Elimu.

Kuna utaratibu mbovu sana kwa wanafunzi wanaosoma shule ya msingi Tandika iliyoko wilaya ya Temeke mkoa wa Dar Es Salaam. Wanafunzi wamekuwa wakilazimishwa kusoma masomo ya tuition.

Wanafunzi wanakuwa wanalalamika kupigwa na waalimu wao wa darasa husika hasa darasa la kwanza wakilazimishwa kusoma tuition.

Kuna wakati mtoto alikataa kwenda shule nilipomuuliza sababu ya kukataa akasema mwalimu amekuwa akimpiga asipopeleka fedha ya tuition, nikalazimika kwenda na mtoto shule kujua ukweli wa jambo hilo nilipofika shuleni nikamkuta mwalimu wake nikamuuliza sababu ya kumuadhibu mwanafunzi, akajibu kwa kejeli kwamba mwanafunzi huyo ni mzito, nikamuuliza uzito gani unaomaanisha akasema ni mzito kujifunza.

Lakini mwanafunzi huyo anasoma darasa la kwanza na anajua kusoma, kuandika na kuhesabu kwa ufasaha kabisa.

Nilichogundua ni kuwa walimu huwa wanaanza kufundisha wanafunzi masomo ya tuition nyakati za asubuhi kwa wale wanafunzi waliolipa fedha za tuition na wanatengwa darasa tofauti na wale ambao hawajalipa. Na hii imekuwa ni kero kwa wanafunzi wengine ambao hawajalipa fedha ya tuition kwasababu wanakosa haki ya kufundishwa kama wanafunzi wengine hadi pale watakapotoa fedha hizo.

Jambo hili limekuwa ndiyo utaratibu wa shule hii, naomba taarifa hizi zifike kwa mamlaka husika kwa hatuna zaidi.

Asante naomba kuwasilisha.
 
Back
Top Bottom