KERO Kero za MCT: Ada Kubwa, Huduma Mbovu, majibu ya mitihani na leseni hawatoi kwa wakati

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Kuna kero sana kwenye hii Medical council of Tanganyika(MCT), chama kinachosimamia madaktari wa nchi hii kila mwaka tunalipia leseni laki moja na elfu hamsini, lakini hakuna cha maana tunachopata

Sasa hivi mtu unalipia lakini wanashindwa kuhuisha leseni ukiwapigia simu hawapokei muda mwingine hawapatikani, wamefungua group la whatsapp kwamba watakuwa wanachukulia kero huko lakini unaeleza kero zako hakuna anaejibu wala kutatua

Mwaka jana watu wamefanya mtihani wa leseni mwezi wa kumi na moja majibu wamekuja kupewa mwezi wa tatu yaani miezi mitatu mbele na hapo ni baada ya watu kupiga kelele

Waliofanya mtihani wa leseni mwaka huu mwezi wa nne hawana matumaini matokeo yao yatatoka lini, ukiingia kwenye tovuti yao wanasema matokeo yatatoka baada ya mwezi ila hawajawahi kufanya,sijui hili baraza lina shida gani
 
Huu utaratibu wa leseni waupeleke pia kwenye kada nyingine ikiwemo ile ya ualimu. Hivyo basi Mwalimu atakayeshindwa kuhuisha leseni yake kwa sababu yoyote ile, basi serikali imuondoe kwenye mfumo wa ajira! Ila kwa sharti la kumpa mafao yake yote ili akapambane mbele ya safari.

Ikitokea hivi naamini walimu wengi watafurahi sana.
 
Leseni kila mwaka 150000 kuna mwalimu atakubali kulipia?
 
Huu utaratibu wa leseni waupeleke pia kwenye kada nyingine ikiwemo ile ya ualimu. Hivyo basi Mwalimu atakayeshindwa kuhuisha leseni yake kwa sababu yoyote ile, basi serikali imuondoe kwenye mfumo wa ajira! Ila kwa sharti la kumpa mafao yake yote ili akapambane mbele ya safari.

Ikitokea hivi naamini walimu wengi watafurahi sana.
Mbona hata huku Afya wapo wengi hawalipii hizo ada za kila mwaka,na hawajaondolewa kwenye utumishi. Mi mwenyewe nimelipia mara ya mwisho 2021.
 
Hapo kwa leseni wanakera sana lakin kwa majibu ni halali wasitoe kabisaa coz wakitoa majibu kwa wakati mtihani utavuja bora ungesema Matokeo ya mtihani.
 
Hapo kwa leseni wanakera sana lakin kwa majibu ni halali wasitoe kabisaa coz wakitoa majibu kwa wakati mtihani utavuja bora ungesema Matokeo ya mtihani
Nahisi amemaanisha matokeo ya mtihani(kwa maana ya results), kwenye tovuti yao wanasema ni siku 30 lakini watu wanasubiri kwa zaidi ya siku 90, ukiangalia huwezi kuomba kazi yoyote kama huna leseni
 
hii nchi watu walisha pandikizwa uoga mtu ananyonwa badala aseme kwa sauti kubwa anabaki kulia huku ameziba mdomo. Kenya tunawaona wajinga wanapoandamana kwa mambo kama haya lakini mwisho wa siku wanarekebishiwa. Kama hapa kwa kuwa sio yeye peke yake ilikua waamke wote hadi huko kiamani hadi kieleweke. Lakini kwa style hii tutaishi maisha ya kulalamika hadi tuzeeke ndugu yangu.
 
Kuna kero sana kwenye hii Medical council of Tanganyika(MCT), chama kinachosimamia madaktari wa nchi hii kila mwaka tunalipia leseni laki moja na elfu hamsini, lakini hakuna cha maana tunachopata

Sasa hivi mtu unalipia lakini wanashindwa kuhuisha leseni ukiwapigia simu hawapokei muda mwingine hawapatikani, wamefungua group la whatsapp kwamba watakuwa wanachukulia kero huko lakini unaeleza kero zako hakuna anaejibu wala kutatua

Mwaka jana watu wamefanya mtihani wa leseni mwezi wa kumi na moja majibu wamekuja kupewa mwezi wa tatu yaani miezi mitatu mbele na hapo ni baada ya watu kupiga kelele

Waliofanya mtihani wa leseni mwaka huu mwezi wa nne hawana matumaini matokeo yao yatatoka lini, ukiingia kwenye tovuti yao wanasema matokeo yatatoka baada ya mwezi ila hawajawahi kufanya,sijui hili baraza lina shida gani
Wapo kwa ajili ya kupiga pesa za kuhuisha leseni pamoja na full registration. Ila nasikia wafanyakazi wa MCT hapo kambarage towel Dodoma wana hela sana unakuta mtu tu wa reception ana miliki ndinga yenye cc zaidi ya 2000. Nilitegema kwa pesa wanayoipata MCT wawe na office zao na hata wawe wanatoa scholarships kwa members. Anyway kila mtu anakula kulingana na urefu wa kamba yake ilimradi usile hadi uvimbiwe.
 
Mimi ni daktari wa Binadamu! Kero zangu nazielekeza kwa Baraza la madackari Tanganyika ( medical council of Tanganyika) Utaratibu wao wa kuhuisha leseni Kila MWAKA ni aina ya wizi uliojificha! Inafikirisha mabaraza na taaluma nyingine zinazohusisha leseni, leseni zao Zina kipindi.

Mfano leseni ya udereva miaka 5, leseni za wa uguzi miaka 4, leseni za Biashara nazo Zinamuda lakin madactari wao Kila MWAKA walipie tena wanafanya kazi isiyo ya kibiasharA.

SSerikali iliangalie na kuingilia kati hilli jambo.

Suala lingine la MITIHANI yao ni Nyonyaji. MITIHANI yao haipimi uwezo wa dactari anayoka tarajali na kupewa leseni.. elimu yetu ni shule endelevu... Kama wanaona ni chanzo Cha mapato ni Bora waseme KULIKO kufelisha wanafunzi

Jingine MITIHANI yao ililetwa na ushindani wa Walimu wa Muhas na Udom inapelekea vyuo vingine kukandamizwa

Screenshot_20260525-131707.png

images.jpeg
 
Back
Top Bottom