Kero za Muungano: Ni wakati muafaka kwa Wazanzibari kufanya Referendum

Kero za Muungano: Ni wakati muafaka kwa Wazanzibari kufanya Referendum

MkamaP

JF-Expert Member
Joined
Jan 27, 2007
Posts
8,146
Reaction score
3,235
Nafikiri niwakati sasa umefika Zanznibar wafanye referendum kwamba wanataka muungano Ndio/Hapana. Baada ya hapo ndo tutakuwa na jibu sahihi la kupata ufumbuzi wa kudumu wa hiki tunachoita muungano.
 
Muungano ukivunjika, Tanganyika itasambaratika. Lukuvi alishasema.

Nafikiri niwakati sasa umefika Zanznibar wafanye referendum kwamba wanataka muungano Ndio/Hapana. Baada ya hapo ndo tutakuwa na jibu sahihi la kupata ufumbuzi wa kudumu wa hiki tunachoita muungano.

Referendum hufanywa kwa kitu kilichokubalika kabla . Huu si muungano bali ni UVAMIZI uliopewa jina la muungano.

La msingi ni Tanganyika iondoe majeshi yake ya kivamizi , nchi ikalie kiti chake kwenye UN ambacho hakijaondoshwa na baadaye kama nchi huru ndio watu waulizwe ikiwa wanataka kuungana na nchi yoyote iwe Tanganyika , Kenya au kokote
 
Muungano ukivunjika, Tanganyika itasambaratika. Lukuvi alishasema.

Kama itasambaratika , kwa nini waliomba uhuru ?? au waivamie Zanzibar ili isisambaratike ?? Hizi ndizo akili za viongozi wa kiafrika ni Zerro.

Kwa hivyo kwa nini wasimwombe Muingereza au Mjerumani akaja kutawala mpaka hapo watakapojiona hawawezi kusambaratika ndio waombe uhuru ??
 
Nafikiri niwakati sasa umefika Zanznibar wafanye referendum kwamba wanataka muungano Ndio/Hapana. Baada ya hapo ndo tutakuwa na jibu sahihi la kupata ufumbuzi wa kudumu wa hiki tunachoita muungano.
Zanzibar iliungana na Tanganyika kufanya Jamhuri ya Muungano wa nchi hizo mbili tajwa, kwa maana hiyo referendum haiwezi kuwa na maana kwa Zanzibar pekee bila Tanganyika kufanya pia referendum.

Watanzania wote wapitishiwe referendum kuhusu huu muungano. Nina hakika kwa kufanya hivyo muungano utaimarika zaidi au nyufa zitaonekana wazi na hivyo kuzikarabati kama kero za muungano.
 
Nafikiri niwakati sasa umefika Zanznibar wafanye referendum kwamba wanataka muungano Ndio/Hapana. Baada ya hapo ndo tutakuwa na jibu sahihi la kupata ufumbuzi wa kudumu wa hiki tunachoita muungano.
Ni wazo zuri lakini kwa nini wazanzibari peke yao? Watanganyika nao waulizwe. Muungano uendelee pale tu pande zote zikiukubali. Upande mmoja ukiukataa tugawane fito.

Amandla...
 
Zanzibar iliungana na Tanganyika kufanya Jamhuri ya Muungano wa nchi hizo mbili tajwa, kwa maana hiyo referendum haiwezi kuwa na maana kwa Zanzibar pekee bila

Tanganyika kufanya pia referendum.

Watanzania wote wapitishiwe referendum kuhusu huu muungano. Nina hakika kwa kufanya hivyo muungano utaimarika zaidi au nyufa zitaonekana wazi na hivyo kuzikarabati kama kero za muungano.

Zanzibar ilivamiwa Na Tanganyika. Kuna nchi iliyovamiwa ikafanya referendum ya kuwauliza watu Kama waendelee Na kuvamiwa?

Haya yanaendelezwa kwa sababu bado Wazanzibari hawajawa Na nguvu Za kijeshi kuanzisha japo gorilla war. Ikiwa hali inaendelea hivi ,siku itafika
 
Wengi naona wameuliza kwanini isiwe Tanganyika, ni vyema pia Tanganyika kufanya zoezi hilo lakini Zanzibar ndo naona ni muafaka zaidi kwa sababu malalamiko mengi yanatoka huko na pia kuzuia wizi wa kura za referendum.

Nimechukulia tu kama Scotland, referendum haikufanyika kwa UK nzima bali sehemu tu moja ambayo inalalamika sana na manageble kwa kura. Naamini Zanzibar wapewe huu wasaa wa kupiga hii kitu, haina maana ya muungano kama kuna kero. Kero hufutwa kwa kurudi tena ktk ubao wa wananchi wenyewe kuridhia.
 
Scotland ni tajiri ila Zanzibar ni maskini wa kutisha
Zanzibar ni tajiri kama Scotland ilivyo "in relation to.."
Hivyo wapewe referundum na baada ya hapo tuandike katiba sawia. Mie ktk jicho jingine naona hakuna umhimu sana wa kuandika katiba mpya ndani ya nchi ambayo ina kero za muungano.
 
Nafikiri niwakati sasa umefika Zanznibar wafanye referendum kwamba wanataka muungano Ndio/Hapana. Baada ya hapo ndo tutakuwa na jibu sahihi la kupata ufumbuzi wa kudumu wa hiki tunachoita muungano.
Mi naunga mkono hoja ila maoni yasiwe ya upande mmoja tu. Ifanyike nchi nzima, na kama upande mmoja ndio hawataki, tuanzie hapo kutafuta njia ya kuuondoa muungano.
Zanzibar pekee hawawezi kuwa na jukumu la kuamua hatma ya muungano
 
Ni jambo jema basi tufanye referendum kila upande uwe na kura zake binafsi zisichanganywe kuhesabiwa pamoja. Maana ni ngumu kuandika katiba mpya na kutatua changamoto bila kwanza kushughurika na matatizo rahisi kabisa yaliyopo ambayo tunayafanya kuwa magumu. Changamoto zote za muungano zinatatuliwa na referendum tu.
 
Kuna mtu hajui kama yeye ni Mzanzibari au nani, sababu anacho kitambulisho cha Mzanzibari mkaazi na siyo kitambulisho cha raia au taifa.
 
Ni jambo jema basi tufanye referendum kila upande uwe na kura zake binafsi zisichanganywe kuhesabiwa pamoja. Maana ni ngumu kuandika katiba mpya na kutatua changamoto bila kwanza kushughurika na matatizo rahisi kabisa yaliyopo ambayo tunayafanya kuwa magumu. Changamoto zote za muungano zinatatuliwa na referendum tu.
Huu muungano ilikuwa kwamba tukishazoeana pande zote mbili matatizo haya madogo madogo yangekwisha na tukaendelea kuwa nchi moja. Waasisi walikuwa na matumaini hayo, lakini walichosahau ni kwamba baada ya wao kutoweka kwenye ulingo, hapakuwepo tena warithi wa nafasi zao wenye uwezo wa kuupalilia muungano ili uwe imara zaidi. Badala yake kukajitokeza wasiotaka muungano na kuongeza mafuta, hasa upande wa Zanzibar. Hawa walikuwepo toka mwanzo, lakini nguvu zao hazikuweza kufurukuta kupinga ushawishi wa kuwepo kwa muungano.
Hawa wamekuwa taratibu wakifanya kila njia ya kuudhoofisha muungano, wakaanza na bendera, nadhani hata katiba na mambo mengine mengi.
Wanaotetea muungano huwasikii tena wakieleza chochote, bali iliyobaki ni kutumia mabavu tu, kwa mfano kwenye chaguzi za viongozi.

Tumefika mahali inafaa sasa tutambuane kwa usahihi. Kama Zanzibar na kuwa mZanzibari ni bora zaidi kuliko kuwa mTanzania, basi, ni vizuri tutambuane hivyo kuliko kuendelea kudanganyana na kupeana rushwa ili kuwavuta watu wapende uTanzania. Hili haliwezekani kabisa.
 
Back
Top Bottom