Kero za Wabara (Tanganyika) wakiwa Zanzibar

Kero za Wabara (Tanganyika) wakiwa Zanzibar

and 300

JF-Expert Member
Joined
Jun 27, 2012
Posts
26,398
Reaction score
36,406
Ikiwa wewe umezaliwa Tanganyika basi ukifika hapa kisiwani jiandae na kero zifuatazo.

1. Kudaiwa leseni ya udereva Zanzibar (hata kama unayo ya huko kwenu).

2. Kukosa Uhuru wa kutumia NYAMA PENDWA na kilevi hadharani.

3. Kukosa fursa ya kumiliki ARDHI.

4. Bullying "name calling" (kuitwa CHOGO).

5. Uhuru wa kuabudu mashakani (ref. Uchomaji Moto nyumba za ibada)

NB: ukifika Zanzibar epuka wahuni wanaojificha kwa kuvaa kanzu.
 
Attachments

  • yunusrashidmkomange_1671482304297236.mp4
    4.1 MB
Huwa sioni faida ya muungano huu wa Zanzibar na Tanganyika.

Kama ukienda kununua vitu kwa bei rahisi huku wanakucharge tena ushuru, ardhi huwezi miliki. Ni hasara tupu

Mwenye kujua faida za huu Muungano kwetu wabara azitaje nijue labda kwa chama cha CCM.
 
Ikiwa wewe umezaliwa Tanganyika basi ukifika hapa kisiwani jiandae na kero zifuatazo;
1. Kudaiwa leseni ya udereva Zanzibar (hata kama unayo ya huko kwenu).
2. Kukosa Uhuru wa kutumia kilevi hadharani,
3. Kukosa fursa ya kumiliki ardhi.
Ila wao wakija huku wanataka Kila fursa. Ni ngumu sana ata ukiwa mtu wa bara kuajiriwa zanzibar
 
Hata upande wa ajira ikitokea kuna nafasi zipo kule basi kwa sehemu zilizo nyingi lazima waandike mwombaji lazima awe na kitambulisho cha Mzanzibari mkazi ambapo hapo ni kama wameamua ajira wapaeane wao kwa wao tu lakini ukija huku bara hamna mambo hayo.

Inasikitisha sana yaani.
 
Hata upande wa ajira ikitokea kuna nafasi zipo kule basi kwa sehemu zilizo nyingi lazima waandike mwombaji lazima awe na kitambulisho cha Mzanzibari mkazi ambapo hapo ni kama wameamua ajira wapate wao kwa wao tu lakini ukija huku bara hamna mambo hayo.

Inasikitisha sana yaani.
Sasa nini maana ya kusema Zanzibar ni Tanzania visiwani?
 
Huu Muungano ni janga na si kero.

Kero ni neno dhaifu unapouzungumzia Muungano.Mkeo au mwanao anaweza kukukera na bado akawa mkeo na mwanao.

Kero kwa hakika maana yake halisi ni vitu au mambo madogo madogo mfano ukienda kukata ticket unavamiwa na wapiga debe kumi hiyo ni kero.

Kero unaweza kwenda dukani kununua soda ya Tsh 700 unatoa note ya Tsh 10,000 muuza duka anatumia dakika 10 kukutafutia Tsh 9,300 hiyo ni kero.

Kero ni pale Msukuma ambaye haenda shule (Secondary) sasa ni Dr Msukuma.

Kero ni maudhi madogo madogo ambayo unaweza kumudu kuyavumilia na maisha yakaendelea.

Neno sahihi unapozungumzia Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ni Janga.

Hili neno kero limeletwa na CCM ili kutupumbaza waTanganyika tuone matatizo ya Muungano na mambo madogo madogo.

Ngongo kwasasa Kibanda maiti.
 
Ndo hata na mimi nabakiaga kushangaa.
Siku akija rais mwenye mawazo kama yangu, vile visiwa vitakuwa ni moja ya mikoa ya Tanzania huku sheria ikiwa ni moja kila mahali! Yani itakuwa mtu anayetoka Zanzibar ni sawa na aliyepo Mbeya Arusha Dar es Salaam, Morogoro nk... Vivyo hivyo na anayetoka Tanzania Bara itakuwa sawa.

Nchi moja hii kwanini tugawanywe kwa mafungu?
 
Sema kwa namna ipo ni ngumu sana kulibadilisha hilo.
 
Kitimoto kipo?

Back
Top Bottom