Kero za Wafanyakazi ambazo TUCTA wataziwasilisha mbele ya Rais Samia siku ya Mei Mosi 2023

Mkuu umeongea mambo ya msingi sana. Nchi hii ina fedha nyingi lakini bahati mbaya hazigawanywi kwa usawa.
 
Fao la KUJITOA?

Watu wachukuwe fedha zao zote wanapotaka kama zamani
Hili nalo ni neno mkuu. Aliyependekeza kufutwa fao la kujitoa mbinguni atapasikia tu.
 
Ndugu watanzania, Mei Mosi ni kesho. Sote tujiandae kuwasikiliza TUCTA wakitoa kero zao mbele ya Rais Samia kwenye maadhimisho haya yatakayofanyika kwenye uwanja wa Jamhuri Mjini Morogoro.
 
Nyonyaji kubwa la watumishi nchi hii ni vyama vya wafanyakazi.

Kukata 2% ya Mshahara wa mtu mwaka mzima halafu unampa T-shirt la elfu 10 Mara moja kwa mwaka, ni DHULMA NA WIZI.
 
Fao la kujitoa limeishia wapi?
 
Andiko zuri
 
Umeandika jambo zuri mkuu
 
Pointi unayo usikilizwe ila wafanyazi wa serikali mjiongeze jamani mitaji mnayo ya kutosha,fanyeni shughuli za ziada jamani hata biashara ,mkitegemea serikali mtazidi kufamaskini, serikali Haina Nia njema na nyinyi ila ni kukukamua mpaka utamu wako uishe Kisha kukutupa huko na 33% Tena ya pesa zako ulizowekeza Kwa miaka mingi,Kwa upande wa viongozi wa vyama vya wafanyazi makada ni wengi sana wa CCM,niwashauri tu wafanyakazi maslahimazuri yapo Kwa wanasiasa gombeeni jamani huko,na katiba iruhusu mgombea binafsi jamani.

Sent from my ZTE T1002 using JamiiForums mobile app
 
Kongole ndugu tpaul kwa andiko bora kabisa linalohusu wafanyakazi.

Mungu akubariki sana.
 
Kikokotoo nma fao la kujitoa ni tatizo kubwa kwa wafanyakazi lakini kwa kuwa TUCTA na serikali ya CCM lao moja huwezi kuwasikia wakiongelea jambo hili hata kidogo.
 
Imezikwa
 
hakuna mtu hathaminiwi katika hii nchi kama mtumishi wa umma na hii imesababisha hata utendaji mbovu kwenye sekta ya umma na wanufaika wa sekta ya umma watabaki kulia kila kukicha mpaka serikali itakapothamini hawa watu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…