Kesi baina ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC na Rwanda kusikilizwa Leo 12 na 13 Februari katika Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu

Kesi baina ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC na Rwanda kusikilizwa Leo 12 na 13 Februari katika Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu

Joined
Jun 26, 2024
Posts
16
Reaction score
16
Kesi baina ya Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo, DRC na Rwanda kuanza kusikilizwa leo Februari 12 na 13, 2025 katika Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu.

Kesi hiyo iliwasilishwa mahakamani hapo Agosti 21, 2023 dhidi ya Rwanda kwa madai ya ukiukwaji wa haki. Tuhuma za Congo dhidi ya Rwanda zinahusiana na mzozo uliokumba eneo la mashariki mwa nchi hiyo tangu 2021, ambako vikosi vyake vimekuwa vikikabiliana na waasi wa M23 wanaodaiwa kuungwa mkono na Rwanda.

Hoja itakayosikilizwa katika kesi hiyo ni pamoja na kuhusu mamlaka ya mahakama hiyo na uwezo wake wa kusikiliza ombi iliyowasilishwa na DRC.

Kulingana na taarifa iliyotolewa na Mahakama hiyo yenye makao yake mjini Arusha Tanzania, Congo inadai kuwa mzozo huo umesababisha mauaji, uvamizi wa maeneo yake, na watu 520,000 kulazimika kuyahama makazi yao, kuzuka kwa ugonjwa wa kipindupindu na uharibifu wa shule na hivyo kusababisha watoto 20,000 kukosa elimu.

Kupitia kesi hiyo DRC anaiomba Mahakama:
  • Kuiamuru Rwanda kuondoa majeshi yake kutoka DRC na kusitisha mara moja aina zote za msaada kwa M23, ili kukomesha ukiukwaji wa haki za binadamu;
  • Kuiamuru Rwanda kufidia ipasavyo uharibifu uliosababishwa na ukiukwaji huo, kwa taifa na wananchi wake ;
  • Kutoa uamuzi kwamba Mahakama itasikiliza na kuamua swala la fidia.

Kesi hii inasikilizwa siku chache baada ya Marais wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, EAC, na Jumuiya ya Maendeleo ya Mataifa ya Kusini mwa Afrika SADC, kukutana jijini Dar es Salaam Tanzania, kutafuta ufumbuzi wa mzozo huo.
 

Attachments

Back
Top Bottom