kuna kitu huelewi. prosecutor ndio mwenye mamlaka ya nani ashitakiwe na nani asishitakiwe. Mahakama haina mamlaka kumlazimisha prosecutor amshitaki mtu asiye mtaka kumshitaki hata kama wewe unaona amefanya makosa, yeye prosecutor anaweza kuwa na sababu zake ambazo sio lazima akwambie. wakati wa ukamataji suspects kuna watu wengi huwa wanakamatwa, lakini upon scrutinizing evidence in the file unachambua, nani akipelekwa ushahidi wake ni mzito na nani anatakiwa asishitakiwe ila awe shahidi. mnaweza kukamatwa watu wanne, wengine kati yenu wakageuka mashahidi wako. kuwepo pamoja mahabusu hakutumiki kuamua kesi kama una kosa au la, ila ushahidi. kama Ling'wenya alisema kuwa walikuwa wote mahabusu basi chote anachokisema Urio ni cha kweli.
na wakati mwingine ili kujua kilichopo moyoni mwa mtu, watu kama hao wanaweza hata kutumwa kabisa wakunasishe, kwani pccb huwa wanafanyaje? si wanaandaa kabisa hela ya kumpa mtu uliyemwomba rushwa na hela hizo wameweka alama, ukipokea tu kwa akili yako unafikiri labda na yule aliyetoa rusha mtashitakiwa naye, kume ndio anakuwa shahidi wako. akili zenu sijui mnapelekaga wapi cdm. Tundu Lisu anawadanganya sana na amewapoteza sana kwa hasira zake dhidi ya serikali, yeye yupo ulaya anabwia wine wenzake waliopo gerezani anapigilia msumari wasitoke. na kwa taarifa yako kwa ushahidi wa aina hii, mbowe anafungwa na hata wazungu wataappreciate kwamba kweli kume kulikuwa na kitu.
kitu kikubwa ambacho chadema wanashindwa kuelewa ni kwamba, pamoja na yoote hayo, ushahidi wa jana umeanza kufumbua macho kuonyesha kuwa kumbe ni kweli mbowe alikuwa anawasiliana na hao watu, mwanga umeanza kuja sasa watu wanaelewa. ushauri ulio mzuri ilikuwa mbowe na chama chake wasijifanye wajuaji wakati wanajua kabisa wamefanya makosa, serikali ingeshawasamehe, kwani kusamehe shilingingapi?, lakini wao na kina Tundu Lisu wameamua kuidhalilisha serikali kwama mbowe hatakiwi kusamehewa kwasabau hana kosa, sasa itabidi prosecution watoe ushahidi wote kuwaonyesha kwamba alikuwa na kosa, na mwisho wa siku atafungwa kwasababu alichezea bahati. unafanya kiburi wakati huna lolote. huu ndio ukweli.
inaonyesha wazi mbowe alikuwa anaamini anaweza kuspy vyombo vya serikali kupitia watumishi wa serikali ambao sio waaminifu, bila kujua kuwa wenzake wamekula kiapo cha maisha. alikuwa negligent sana.