kwa taarifa yako, it was too early kipindi kile kufanya hivyo, na criminal case huwa haifi. wangemkamata kipindi kile cha kampeni au uchaguzi au soon after election, hata wao walijua pasingetosha, wabaya toka ulaya na wa hapahapa nchini wangetafuta sababu ili machafuko yatokee. nakushaurini subirini hadi mwisho kesi itakapoisha na kwa namna inavyofanyika kwa uwazi, watanzania wote watakuwa majaji.
huwa tunawaita wakurupukaji kwasababu umeshaanza kuamua kesi kwamba hakuna ushahidi wakati hata kesi haijaisha, si usubiri mashahidi wote waletwe? kwani mnaogopa nini mashahidi wakiletwa wote, sasaivi prosecution bado hawajafunga kesi upande wao, na nakuambieni wale mawakili wenu pale wanafurahisha umati tu, hakuna wanachokifanya. ukiona mwanasheria amesifiwa na layman kwamba ndiye anajua sana, jua ni patupu, ila ukiona wanasheria wamaappreciate mwanasheria mwenzao hapo ndio uamini. ni wanasheria tu pale tunajua yapi ni makapi na ipi ni ngano. nyie ambao hamjawahi hata kuwa wanasheria ndio mmchambue ushahidi?