Salaam Wakuu,
Leo tarehe 11/11/2021 yanatolewa maamuzi ya kesi ndogo Mwenyekiti wa CHEDEMA Freeman Mbowe.
Kujua jana kesi ilipoishia, soma: Yaliyojiri Mahakama Kuu kesi ndogo ya Mbowe, Superitendent Jumanne Malangahe atoa Ushahidi
Ungana nami katika uzi huu ili kujua kila kinachojiri Mahakamani.
Picha: Watu mbalimbali waliohudhuria Mahakama kuu leo 11/11/2021
UPDATES;
Jaji ameingia Mahakamani Sasa Saa 5 Na Dakika 15 Kesi namba 16 ya Mwaka 2021 Khalfani Bwire, Adam Kasekwa, Mohammed Ling'wenya na Freeman Mbowe inatajwa.
Wakili wa Serikali Robert Kidando anatambulisha Jopo la Mawakili wa Serikali
1. Pius Hilla
2. Abdallah Chavula
3. Jenitreza Kitali
4. Nassoro Katuga
4. Esther Martin
5. Tulimanywa Majige
6. Ignasi Mwinuka
Wakili Peter Kibatala anawatambulisha jopo la Mawakili wa Utetezi:
1. Jeremiah Mtobesya
2. Paul Kaunda
3. Fredrick Kihwelo
4. Dickson Matata
5. Iddi Msawanga
6. John Mallya
7. Alex Massaba
8. Khadija Aaron
9. Evaresta Kisanga
10. Maria Mushi
-
Jaji anawaita washtakiwa wote wanne, na wanaitika kwamba wapo.
Wakili wa Serikali: Mheshimiwa Jaji Shauri linakuja Kwa ajili ya kusikiliza Uamuzi wa Mahakama, sisi tupo tayari Wakili Peter Kibatala: Nasi pia kwa Ruhusa yako tupo tayari Kupokea Uamuzi na Kuendelea na Kesi.
- Jaji anaandika Kidogo
Jaji: Jana nilisikikiza Pingamizi la Upande wa Utetezi, Na baada ya Kusikiliza Pande zote Mbili, Maamuzi yapo tayari Jana wakati Shahidi akitoa Ushahidi alieleza Kwamba Baada ya Kupewa Maelekezo ya Kumwandika Maelezo Mshtakiwa namba tatu
Jaji: Na baada ya kupitia Nyaraka hiyo Shahidi alisema anaitambua na baada ya hapo aliomba Mahakama Ipokee Nyaraka hiyo kwa ajili ya Utambuzi, Kitu ambacho Mawakili Wa Washtakiwa wote wanne walipinga Vikali
Jaji: Inapaswa Shahidi ajenge Misingi Kwamba Kwa namna Gani Kielelezo Kimemfikiaje Mahakamani, Na Mawakili Wakasema Kinachotolewa Mahakamani ni Register siyo Entry Kwa Mfano Ingekuwa na Features ambazo zinaonyesha Register hiyo Inatumika Central tu na siyo Mahala Pengine popote
Na Pale ambapo Shahidi ametoa Ushahidi wake anaweza Kufafanua, Wakaomba Mahakama Ione Kielelezo Kilichopo Mahakamani shahidi anaweza Kutoa Ushahidi Wake, Wakaeleza tarehe 07 August 2020 namba alivyo fika Saa 11 Alfajiri na Jinsi ambavyo Shahidi aliweka Entry na aliweza Kukitambua
Jaji: na hicho ndicho kimezua shaka. Na Upande wa Mashtaka Walipata nafasi Ya Kujibu kwa Kuwakilishwa na Abdallah Chavula na Pius Hilla Walisema Kwamba Mapingamizi hayana Mashiko, Wakaja na Kesi ya DPP VS SHARIF Authentication ya Mahakama Inapaswa Kufanywa na Ushahidi Wa Shahidi.
Wakaomba Mahakama itofautishe Kesi ya DPP VS SHARIF ATHUMAN kwamba kesi ile Kielelezo Kilikuwa Gari na Kwenye Kesi hii Kielelezo ni Nyaraka, Wakarejea Kesi ya CHARLES GAZILABO dhidi Ya Jamhuri Kwamba Kesi hiyo iliweka Mambo Matatu ya Relevance, Competence na Shahidi Husika
Wakasema Kwamba Kwa namna ambavyo Shahidi alikuwa anatoa Ushahidi Wake ni Competent. Wakasema Kwenye Kesi Ya CHARLES GAZILABO Kwamba Mtu anaye weza Kuelezea Kielelezo NA kukitambua, Kitu ambacho Shahidi alifanya.
Shahidi alieleza Kwamba alifika kituo cha Polisi Kati Dar es Salaam, Hiyo inathibitisha kwamba Shahidi anaweza Kufanya Utambuzi na wakaomba Mahakama Itupilie mbali, Upande wa Utetezi Walipata tena nafasi ya Kujibu na Kuona Bado Mapingamizi yao yanayo Sababu
Jaji: Na wakaendelea Kusema Kwamba Suala Zima la Chain of Custody, Mahakama Imeshatolea Maamuzi Kwamba Chain of Custody Inaweza Kujadiliwa Mwishoni, Wakasema Shahidi alijitahidi Kueleza Kwamba aliweka Entry na hilo pekee ndiyo lina fanya Shahidi aonekane anaweza Kukitambua.
Jaji: Kwenye kesi Ya SHARIF ni kwamba wanaona Kanuni inaweza Kutumika Kwenye kesi yoyote, Na Kwamba Shahidi ameeleza Entry na a siyo Kielelezo Chenyewe na Kwamba Suala la Authentication halijaweza Kukidhiwa, Na swala Zima la Kuamua Chain of Custody Wali endelea Kusema Swala La Kupinga Kielelezo ni Jukumu lao Kupinga Wakati Wa Uchukuliwaji, Upande wa Mashtaka wamekosa Hoja za Msingi kuhusiana na Mapingamizi yao.
Na Kwamba Hakuna Features Mahususi Kuhusiana na Kielelezo hicho ili Kutofautisha Detention Register na Detention Register zingine zinazotumika katika Vituo Vingine.. Na suala la Chain Of Custody haijaelezwa Vizuri ni wapi Walipo toa Kielelezo hicho, Kwamba kwa Kumbukumbu zilizopo bado Kielelezo Kipo Chini ya Mahakama. Huo ndiyo ulikuwa Mwisho wa Muhtasari. Sasa twende kwenye maamuzi.
Jaji: Identification of EXHIBIT, Establishing Chain Of Custody, Identification of Objects. Haya siyo Maneno yangu ni Maneno ya Maamuzi ambayo nimeyanukuu hapo juu. Lengo la Chain Of Custody wanapaswa Kueleza Kielelezo Wamekitoa wapi.
Na Kuhusiana na Competence ya Shahidi imeelezwa Kwenye kesi ya CHARLES GAZILABO, KHAMIS ADAM Kwamba Mtu ambaye amekifanyia kazi Kielelezo siyo tu anaweza Kukitolea Ushahidi Bali anaweza za Pia Kukitolea Maelezo
Jaji anasoma maamuzi ya kesi hiyo aliyonukuu
MAAMUZI
JAJI: Tunakubaliana kwa pamoja Kwamba Pingamizi linapinga ipokelewaji wa Vielelezo na Siyo Jambo geni Mahakamani, Na Maamuzi Yamefanywa na Mahakama zetu katika Upokeaji wa Vielelezo Mahakamani. Maamuzi yameonyesha Taratibu, Kanuni na Muongozo.
Kufuatia Maamuzi ya SHARIF MOHAMMED na wenzake Mahakama ya Rufani Ilitoa Maamuzi Kwamba tunao Ushahidi Wa Namna Nne Uhalisi, Testimonial, Documentary Evidence, Na Kwamba Mahakama inaweza Kupokea Ushahidi Mahakamani Wakati wowote.
Mahakama Ijiridhe Kama Ushahidi ni Relevance, Material na Competence, Na Katika Maamuzi yake wamejadili kwa kina kuhusu Ushahidi Halisi. Nimesema Mpaka Mwisho Sijaona Kwamba Vigezo ambavyo vinatumika Katika Real Evidence haitakiwi Kutumika katika Kupokea Documentary Evidence.
- Jaji amemaliza kusoma Maamuzi ya Shauri hilo kama Rejea yake,
Jaji: Kimsingi hayo ndiyo maamuzi ya mahakama ya Rufaa.. Kwa sababu hiyo sasa ilikupima Competence ya Shahidi, Na Kwa Kesi hii Shahidi ameeleza Vizuri kuhusu Kielelezo hicho ambacho alikotumia Kuweka ENTRY ili Kumtoa.
Shahidi Kwenda Kumchukua Mtuhumiwa Maelezo yake. Kwa Maana hiyo anayo Competence. Kuhusiana na Relevance ni Ukweli kwamba Kipo Relevance sababu inadaiwa ndiyo walitumia Kielelezo hicho Kumtoa Mtuhumiwa
Kuhusiana na Materiality ni kweli kabisa kwamba kitasaidia Mahakama Kufanya Maamuzi, ikiwemo Katika Pingamizi Kwamba Mshitakiwa hakuwa hi Kuwepo Katika Kituo hicho cha Polisi. Mahakama hii inaona kwamba ni sahihi kabisa kuendelea kutumika.
Jaji: Imebakia suaala la Chain Of Custody, Ni kweli Shahidi namba Moja ameeleza Kwamba anaweza Kutambua Kielelezo hicho Kwa Majina yake na Sahihi Yake na Majina ya Mtuhumiwa, Ukweli ni kwamba ameweza Kukitambua, Ingawa Mr. MTOBESYA amepinga Kwamba Features zilizoelezwa ni za Entry na siyo Register Yenyewe.. Lakini Mahakama yenyewe inaweza Kutambua kuwa Kielelezo hicho huwezi Kutenganisha Entry na Register. Na Kuhusiana na Chain Of Custody Shahidi hajeleza Chain of Custody Kwamba ni Kwa namna gani Kielelezo hicho Kimemfikia.
Jaji: Ni kweli Kwamba hajaeleza ametoa wapi, Ni kweli Kwamba Kielelezo Kipo Kwenye Kumbukumbu ya Shauri Lingine, Ili Mahakama ione kama kilifuata Utaratibu kilipaswa kionekane kwamba ni kweli Kilifuata Utaratibu wa kiutawala kutoka Mahakamani.
Na Kwa namna hiyo Kielelezo kinajifuta Chenyewe kwa sababu Shahidi hakuonyesha namna gani kilimfikia, Assumption ni kwamba Kielelezo Kipo Kwenye Chumba cha Mtunza Kielelezo Cha a Mahakama, Hakuna Ushahidi Kwamba Shahidi alikipataje kuja Mahakamani.
Jaji: Kwa sababu hiyo mahakama inakikataaaaa kielelezo hiki natoa amri.
- Mawakili wa pande zote wanasimama na kuinama kuonyesha kukubaliana na uamuzi wa Jaji.
Jaji: Shahidi wenu yupo wapi tuendelee
Jaji: Shahidi nakukumbusha Upo chini ya Kiapo ambacho Ulikiapa wakati Unatoa Ushahidi Wako
Wakili wa Serikali Robert Kidando ameanza kuuliza maswali
Wakili wa Serikali: Shahidi Ulisema Kwamba Siku ya Tarehe 07 August 2020 ulimchukua Mohammed Ling'wenya Kwenda Kumchukua Maelezo, Eleza Siku hiyo alikuwa na hali gani
Shahidi: Wakati na chukua Mohammed Abdilah Ling'wenya alikuwa Mwenye Afya Njema na Hakuwa na Tatizo lolote
Wakili wa Serikali: Baada ya Kumchukua Ulimpeleka wapi
Shahidi: Nilimpeleka Pembeni Kidogo Kwenye Chumba Kwa ajili ya Mahijiano na Mtuhumiwa huyo
Wakili wa Serikali: Elezea Baada ya Kukaa Pamoja nini Kiliendelea
Shahidi: Nikijambulisha Kwa Majina Kwamba Mimi ni ASP JUMANNE MALANGAHE, Na Mtuhumiwa akajitambulisha kwa Majina yake Kwamba anaitwa Mohammed Abdilah Ling'wenya alimaarufu kama DOYI
Wakili wa Serikali: Elezea Ni kitu gani sasa Ulifanya Baada ya Kujitambulisha
Shahidi: Nilimuonya Kwamba anatuhumiwa kwa Makosa ya Kula Njama za Kutenda Matendo Ya Ugaidi, Nilimueleza kwamba Katika tuhuma hizo alazimiki kueleza Chochote isipokuwa kwa hiari yake Mwenyewe chochote atakachokieleza kinaweza Kutumika kama Ushahidi Mahakamani, Vilevile anayo Haki ya Kuwepo Mwanasheria Wake, Ndugu yake, Jamaa yake, Rafiki ili ashuhudie Wakati Maelezo hayo yakiandikwa, Baada ya Hatua hiyo, Mimi Nilisaini na Mtuhumiwa alisaini ilikuonyesha nilimuonya.
Shahidi: Baada ya kumaliza Hatua hiyo Mtuhumiwa Mohammed Abdilah Ling'wenya alimaarufu DOYI alijibu Onyo hilo.. Kwamba yeye Mohamed Abdilah Ling'wenya Alimaarufu DOYI ameonywa na Mimi ASP JUMANNE MALANGAHE anatuhumiwa kwa Kosa la Kula Njama kutenda Vitendo Vya Ugaidi Chini ya Sheria namba 24 ya Sheria ya Kupambama na Ugaidi, Kwamba alazimishwi Kusema Lote isipokuwa kwa hiari Yake Mwenyewe. Chocolate atakachoandika Linaweza Kutumika aka Ushahidi Mahakamani.
Na pia anaweza Kuwepo Mwanasheria Wake, Ndugu yake, Jamaa yake, au Rafiki ili ashuhudie Wakati Maelezo yake yakiandikwa. Baada ya Mtuhumiwa kuulizwa Onyo hilo kama Yupo Tayari Kutoa Maelezo yake, Mtuhumiwa akajibu Ndiyo Nipo tayari, Nilimuuliza nani awepo Wakati anatoa Maelezo yake, Mtuhumiwa alijibu yeye Mwenyewe anatosha Wakati wa Kutoa Maelezo yake, alisaini na Mimi nikasaini, baada ya hapo akawa tayari Kutoa Maelezo Yake, Saa 2 na Dakika 20 nilianza kuandika Maelezo Ya Mtuhumiwa,
Wakili wa Serikali: Wewe Ulifanya nini baada ya yeye Kusema yupo tayari Kutoa Maelezo
Shahidi: Nilimuuliza Mtuhumiwa Ushiriki wake Kuhusu tuhuma nilizomueleza
Shahidi: Nilimueleza kila anapohusika na ambapo yeye alikiri
Wakili wa Serikali: Wewe baada Kueleza ulifanya nini
Shahidi: Nilikuwa na andika Kwenye Karatasi, Fomu kile alichokuwa ananieleza
Wakili wa Serikali: Kilikuchukua amuda gani?
Shahidi: Muda wa Masaa 2 na Dakika 42
Wakili wa Serikali: baada ya Kumalizia Kuandika Ulifanya nini?
Shahidi: Nilimpatia Maelezo ayasome, ilikuweza Kuongeza, Kupunguza au Kufanya Marekebisho kwa yake aliyiyasema
Wakili wa Serikali: Baada ya Mtuhumiwa Kusoma Maelezo hayo akasemaje
Shahidi: Ameridhika na hana cha Kupunguza wala Kuongeza
Wakili wa Serikali: Ulifanya nini baada ya kuandika
- Kibatala: OBJECTION anachofanya Wakili anajua Hakiruhusiwi
Wakili wa Serikali: Baada ya kumaliza Kuandika Ulifanya nini?
Shahidi: Alisaini na Mimi nikasaini, na baada ya hapo nikaandika Uthibitisho wangu mimi Mwenyewe.
Wakili wa Serikali: Baada ya akumaliza Kuandika Uthibitisho huo Ulifanya nini
Shahidi: Niliandika Muda wa Kuandika Maelezo
Wakili wa Serikali: baada ya Kumalizia Kuandika Maelezo Ulifanya nini na Mtuhumiwa
Shahidi: Nilimchukua na Kumrejeaha Chumba cha Mashtaka
Wakili wa Serikali: Maelezo ya Mshitakiwa Mohammed Abdilah Ling'wenya uliyapeleka wapi
Shahidi: Kwa Assistant Inspector Swila
Wakili wa Serikali: Ilikuwa ni Lini?
Shahidi: Ilikuwa ni Siku hiyo hiyo
Wakili wa Serikali: Elezea Baada ya Shughuli hiyo Ulikutana wapi tena na Mtuhumiwa
Shahidi: Niliondoka Kwenda Kufanya Majukumu Mengine kwa Kadri nilivyokuwa naelekezwa na ACP kingai, Siku ya tarehe 08 August 2020 Majira ya Saa 5 Asubuhi Tukiwepo na Inspector Mahita, Tulielekezwa na Afande Kingai Kumuhamisha Mtuhumiwa na Kumpeleka Kituo cha Polisi Mbweni.
Wakili wa Serikali: Wakati Mlielekea Mbweni Ni kitu gani Kiliendelea
Shahidi: Hakuna Kilichoendelea, Tulipofika Tukiwakabidhi watuhumiwa, Na Kwenda Kuonana na Kiongozi wetu ACP KINGAI kwa Upelelezi wa watuhumiwa Wengine
Wakili wa Serikali: Elezea Baada ya hapo Ulionana naye wapi?
Shahidi: Sikuwahi Kuonana tena na Mtuhumiwa huyo..
Wakili wa Serikali: Kwa Ufahamu Wako Vituo ambavyo Mohammed Abdilah Ling'wenya aliweza Kufikishwa ni Vingapi?
Wakili wa Serikali: Unasema Siku Mnampeleka Kituo Cha Polisi Mbweni hakuna Kilichofanyika zaidi ya kumkabidhi pale, Sababu hasa ni nini?
Shahidi: Sababu zilikuwa za Kiupelelezi, Sababu Kuna Mwingiliano Wa watuhumiwa wengi wanaingia na Kutoka ni wengi.. Tulihofia Taarifa zinaweza Kufika Kwa Watuhumiwa ambao bado tunawatafuta Kwa urahisi.
Wakili wa Serikali: Siku unaandika maelezo ya Mtuhumiwa pale, unasema ulimpa Inspector Swila, Je Inspector Swila alipeleka wapi? -
- Mtobesya: OBJECTION Mheshimiwa Jaji huyo siyo Swila na hawezi Kujibu kwa niaba ya Swila
Wakili wa Serikali: Ngoja Nirudie Swali
Wakili wa Serikali: Ulipompa Swila hizi Karatasi, alifanya nini na Hizo Karatasi
Shahidi: Ndiyo tulikuwa tunampa Nyaraka zetu, Kwa hiyo alizochukua akaenda Kuweka kwenye Jalada
- Mtobesya: OBJECTION Mheshimiwa Jaji hizo ni hearsay
Jaji: Jiande uje kumuuliza labda walikuwa naye.
Shahidi: Swila amuda Mwingi tulikuwa naye, alienda Kuweka kwenye Jalada la Upelelezi
- Kibatala: OBJECTION Mheshimiwa Jaji Wakili anahama Eneo, Je ulichokiandika Siyo HearSay
Wakili wa Serikali: Sisi Bado hatuoni tatizo, huyu Mohamed Abdilah Ling'wenya amepinga Maelezo ya Onyo kwamba hakuwahi Kufika Kituo cha Polisi Kati Dar es Salaam na ajawahi Kuandika Maelezo hayo..
Shahidi: Siyo Kweli, Mimi Mwenyewe ndiyo Niliyempeleka Pale, Nikaenda Kumchukua Mimi Mwenyewe Kutoka Kwenye Chumba Cha Mashtaka Nikiwa Pekee yangu bila Uwepo wa Askari Mwingine yoyote akiwa na hali Nzuri, na Mimi Niliondoka nikiwa nje ya Kituo na yale maelezo, Nikampigia Assistant Inspector Swila yale achukue yale maelezo ili aweke kwenye Jalada la Kesi.
Wakili wa Serikali: Wewe una utbitisho gani kwamba uliandika Hayo Maelezo siku ya tarehe 07 August 2020
Shahidi: Alikuwepo Askari aliyekuwepo pale Chumba cha Mashtaka. Na baada ya kumaliza Kuandika Maelezo Askari huyo huyo alimpokea na Kumrudisha Lockup.
Wakili wa Serikali: anachosema ni kwamba ulimtishia kwa Bastola ilikutoa Maelezo
Shahidi: Siyo Kweli, Sikuwahi Kumtishia Mtuhumiwa huyo Kwani alikuwa na Ushirikiano, Sikuwa na Sababu hiyo
- Kibatala: OBJECTION, huyu labda hajasikia Vizuri Mapingamizi, nayasoma tena kwa sauti ayasikie
Wakili wa Serikali: Sawa Ngoja Nirudie, Ulimtishia Kwamba Asipo Saini Ile Karatasi ya Maelezo basi yale Mateso Mliyompatia Moshi Mtayarudia
Shahidi: Si kweli Sikumtishia kwa sababu sikuwa na sababu hiyo.
Wakili wa Serikali: Maelezo ya Mohammed Abdilah Ling'wenya ukiyaona unaweza Kuyatambuaje
Shahidi: Naweza Kuyatambua Kwa Majina Yangu, Sahihi yangu, Uwepo wa Majina ya Mtuhumiwa na Sahihi zak na Yote aliyo I eleza Nikaandika kwenye Karatasi ya Maelezo.
Wakili wa Serikali: Samahani Mheshimiwa Jaji tunaomba tumpatie Nyaraka Kwa sababu ya Utambuzi
- Shahidi anamkabidhiwa Nyaraka
Wakili wa Serikali: Angalia Nyaraka hiyo Kama Umeitambua na Useme ni Kitu gani?
Shahidi: Ndiyo nimeitambua Nyaraka hii Kama Maelezo Niliyoaandika kutoka kwa Mohamed Abdilah Ling'wenya Maarufu Kama DOYI,
Wakili wa Serikali: Umeitambuaje?
Shahidi: Kwa Majina Yangu, Sahihi Yangu Pamoja na Saini zake pamoja na aliyoyaeleza
- Kibatala: OBJECTION kwa Stage ya Utambuzi anatakiwa asifike kwenye aliyoyaandika Sababu ni Content
Wakili wa Serikali: Sisi hatuoni tatizo
Kibatala: Kwa Stage ya Utambuzi, aliyoyaandika ni Content
Jaji: content yake hatuingii, anaishia Kusema ameyaona
Wakili wa Serikali: Ungependa Mahakama ifanye nini katika Hayo Maelezo uliyoandika kutoka Kwa Mohammed Abdilah Ling'wenya alimaarufu kama DOYI
Shahidi: Ningependa Mahakama Iyapokee kwa Utambuzi
Mtobesya: Hatupingi Upokelewaji wa Maelezo haya Kwa niaba ya Mshtakiwa wa Kwanza Sababu ni Zifuatazo Naomba Iwe on record Kwamba Mahakama inayajua hayo Maelezo lakini Mshtakiwa wa tatu Amekataa hayo Maelezo Kutokupinga huku Hakumaanishi Kwamba Mshtakiwa anakubaliana na Content.
Wakili wa Serikali S Pius Hilla: OBJECTION Mheshimiwa Jaji natafakari kwamba hupingi lakini kwa conditions kwamba lazima sababu zieleweke, Kama hupingi, Lakini unapoongezea Vitu Vingine inamaana hukubaliani, Tunatengeneza Record gani kwa Mahakama. Kama kuna Jambo it's better akapinga tu hadharani..
Wakili wa Serikali Robert Kidando: kwa Kuongezea tu, hili zoezi la Trial Within Trial na Hii Conditions alizo +toa hapa hairuhusiwi.
Mtobesya: Mheshimiwa Jaji Sijui Kwanini Wenzangu Wamesimama, Wenzangu Waniambie Kwamba Ni Sheria gani inakataza Ninaposema sipingi siruhusiwi Kuongeza Maneno.. Sijui Wenzangu Wanahofu gani labda.. Wakasome Kesi ya Martha Weja sisi Kama Utetezi tunaruhusiwa Kuhoji content.
Jaji: katika Kesi yoyote Mahakama haijui chochote, Bila nyinyi Kueleza Mahakama, Mahakama Imeelekezwa Kwamba Isiyapolee yanayo Vunja Sheria yoyote, Sioni Tatizo Kwa Mtobesya Kuzungumza alichozungumza na huwezi kujua atakitumia wapi.
Mtobesya: naomba nikumbushwe niliishia wapi
Jaji: uliishia Mheshimiwa Jaji
Mahakama: Kicheko
Jaji: Unakubaliana na Mahakama Kupokea Lakini Hukubaliani na Content..
Mtobesya: naomba niishie hapo
- Anasimama Wakili Paul Kaunda...
PAUL KAUNDA: kwa niaba ya Mshtakiwa wa Pili tunaomba kufunga Mkono kilichozungumzwa na Wakili wa Mshtakiwa Wa Kwanza Fredrick Kihwelo: Tunakubaliana na Uwepo wa Nyaraka hii lakini hatukubaliani na Kilichopo Ndani
Kibatala: Kwa niaba ya Mshtakiwa wa Nne na sisi Hatupingi, Tunategemea Kuitumia Nyaraka hii katika Kuhoji Dodoso katika kesi hii Ndogo
Jaji: Yaliyosemwa na Mtobesya Mnalolote la Kujibu (Mashtaka) WS Wanateta Kidogo napokea kama ID namba 1
- Wote wanakubali.
Wakili wa Serikali Robert Kidando: Naomba Dakika Mbili Nishauriane na Wenzangu Kuhusu Hoja ya Mtobesya kama Kuna la Kumjibu..
Wakili wa Serikali: Off Record Kwanza, Kuna Jambo la Mtobesya Kwamba Kwenye kesi ya Martha Weja, Tukasema tunaomba tujiridhishe kwanza.
Mtobesya: Kwa haki tuwaache wajiridhishe tu, Ni Kesi ambayo Imeripotiwa Kwenye TANZANIA LAW REPORT ya Mwaka 1982 Ukurasa wa 35..
Kibatala: nawakumbusha kwamba wenzetu wazingatie na muda kwa sababu leo tumeamza Saa tano na shahidi ana siku mbili kizimbani.
Jaji: Siku 3 labda kwenye kesi Ndogo ndiyo Siku 2..
Wakili wa Serikali: Mheshimiwa tupewe tu Muda wa Kutosha kwa sababu hatuna hapa na hatuwezi Kupata ipo Ofisini
Jaji: Mtobesya ametaja Mpaka Kurasa labda anayo hapo.
Mtobesya: Hapana sina hapa ni kesi ya siku nyingi lakini tunatumia sana, Naweza kuiomba na Mimi ofisini Wakascan wakanitumia
Jaji: Natoa Hairisho la Dakika 45, tutarudi Saa 8 Jaji anatoka.
Zinapigwa kelele za kooooooortiiiiiii