Kesi ya Dr. Slaa inaendelea Mahakamani bila yeye kuwepo

Kesi ya Dr. Slaa inaendelea Mahakamani bila yeye kuwepo

Kwa ufupi, kisheria, kuendesha kesi ya jinai bila mtuhumiwa kuwepo mahakamani ni ukiukwaji wa haki za msingi za mtuhumiwa na kanuni za utawala bora. Mtuhumiwa ana haki ya kuwepo mahakamani ili kujitetea na kushiriki kikamilifu katika mchakato.

Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai (Sura ya 20 ya Sheria zilizorekebishwa) Kifungu cha 225(1): Kinamtaka hakimu kuhakikisha kwamba mshtakiwa yuko mahakamani wakati wa kusikiliza kesi.
 
Kama mtuhumiwa aligoma kwenda mahakamani? Ama alitoa ruhusa ya uwakilishi je? Mahakamani hakuna wajinga wa kuendesha kesi tu ilimradi. Muwe mnaweka habari kamili, sio hujamuona tu slaa mahakamin basi inakuwa habari.
Bado naendelea kusisitiza tu; kiwango cha UJINGA nchini kinatisha mno, ni ngumu sana kupambana na majirani zetu kwa akili hizi; hizo assumption zako kama ni za kweli, imekuaje mawakili wa serikali wasijue? Askari magereza waliokuwepo hapo je?
 
Hii ni mpya kabisa, haijawahi tokea, inakuwaje kesi iendeshwe bila mtuhumiwa kuwepo? Only in my country!

---
Wakili Peter Madeleka anayemwakilisha Dk. Wilbord Slaa kwenye kesi Na.993 ya mwaka 2025 ya kuchapisha taarifa za uongo kwenye mtandao wa X ameiomba mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuuwajibisha upande wa Jamhuri kwa kutomfikisha mahakamani hapo mtuhumiwa (Dk. Slaa).

Madeleka amedai mahakamani hapo kuwa upande wa Jamhuri ndio uliowasilisha zuio la dhamana ya Dk. Slaa kwa madai ya usalama wake "ikiwa haonekani upo wapi uhakika wa usalama wake"
https://x.com/Mwanahalisitz/status/1878721492923371937/photo/1
Soma: Dkt. Slaa afikishwa mahakamani Kisutu kwa Shtaka la kusambaza taarifa za Uongo
Wamuache aozee jela, na dawa sake za sukari na presha wasimpe
 
Kifungu cha 225(1) cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai kinahakikisha haki ya kusikilizwa kwa mtu anayedaiwa kufanya kosa la jinai. Hapa kuna baadhi ya vipengele muhimu vinavyohusiana na haki hii:

1. Haki ya Kusikilizwa: Kila mtu anayo haki ya kusikilizwa kwa haki na kwa wakati muafaka katika mchakato wa kesi yake.

2. Utaratibu wa Haki: Kifungu hiki kinaelekeza kwamba mchakato wa kesi unapaswa kufanywa kwa njia ya haki, ambayo ina maana ya kutoa fursa kwa mtuhumiwa kujitetea na kuwasilisha ushahidi wake.

3. Uwazi katika Mchakato: Kusikilizwa kwa kesi kunapaswa kuwa wazi, ambapo wahusika wote wanapata nafasi ya kutoa maoni yao na kuwasilisha ushahidi.

4. Haki za Mtuhumiwa: Kifungu hiki kinatoa kipaumbele kwa haki za mtuhumiwa, kuhakikisha kwamba hawatendewi kwa njia isiyofaa au ya ubaguzi.

Kwa ujumla, kifungu hiki kinajikita katika kutafuta usawa na haki katika mchakato wa kisheria, ili kuhakikisha kwamba kila mtu anapata haki ya kusikilizwa kwa wajibu. Ikiwa unahitaji ufafanuzi zaidi au mfano, tafadhali nijulishe!
 
Back
Top Bottom