Kesi ya Elizabeth Michael (Lulu), Mke wa Dk. Slaa ahitajika kufika mahakamani kutoa ushahidi

Kesi ya Elizabeth Michael (Lulu), Mke wa Dk. Slaa ahitajika kufika mahakamani kutoa ushahidi

Nimezoea kuona kesi za watu maarufu kupigwa kalenda mara kwa mara, pengine husikilizwa siku moja tu kisha kupigwa kalenda.... Lakini hii ya lulu karibu wiki Sasa inasikilizwa
usipofuatilia mambo mengi yanayohusu nchi yako..utashindwa kuelewa mengi tu yanayotukia.
na pia hii kesi imeanza alhamis ilopita ya tar 19.
 
Kiiiruuuuu!! Haka katoto mambo yanaweza kubalika masikini kakaenda kule "chuo cha mafunzo ya kurekebisha tabia", halafu hii kesi mbona inaenda mbio sana au kwa kuwa zingine sikuwa nazifuatilia?!
 
20171024105115.jpg

Kesi ya kuua bila kukusudia inayomkabili muigizaji wa filamu bongo Elizabeth Michael, (Lulu) imeendelea leo katika mahakama kuujijini Dar es salaam, ambapo upande wa utetezi umeshindwa kuendelea kutoa ushahidi wake kwa kukosekana shahidi mwingine .

Shahidi huyo aliyetajwa kuwa ni mke wa aliyekuwa katibu mkuu wa CHADEMA, Dk. Wilbroad Slaa, Bi. Jacqueline Mushumbusi ambaye yuko nje ya nchi, ushahidi wake umekataliwa kupokelewa na mahakama mpaka awepo mwenyewe au askari ambaye aliandika maelezo yake afike mahakamani kutoa ushahidi huo.

Hapo jana wakili wa mshtakiwa Peter Kibatala aliiomba mahakama iruhusukupokelewa kwa ushahidi utakaotumwa na Bi. Mushumbusi, lakini mahakama imekataa ombi hilo ikisema upande wa utetezi hauwezi kusoma ushahidi huo na kutoa uamuzi wake wa kutaka shahidi awepo mwenyewe au askari aliyeandika ushahidi huo.

Kesi hiyo imeghailishwa mpaka kesho Oktoba 25, ambapo inatarajiwa askari aliyeandika ushahidi wa Bi. Jacquline Mushumbusi, kuwasili mahakamani hapo na kutoa ushahidi wake.
MKE WA DR.SILAA AITAJIKA KUTOA USHAIDI KESI INAYOMKABILI LULU.

Mke wa Padre Slaa anaitwa Josephine na siyo Jacquline, hawa ni watu wawili tofauti.
 
maraa paaaaaaaaaaaaaaap na Dr. anakuja Tanzania "kumsindikiza my wife wake" maana anajua akija peke yake kuna wakora humu wanaweza "kumchapia"
 
Kesi ya kuua bila kukusudia inayomkabili muigizaji wa filamu bongo Elizabeth Michael, (Lulu) imeendelea leo katika mahakama kuu jijini Dar es salaam, ambapo upande wa utetezi umeshindwa kuendelea kutoa ushahidi wake kwa kukosekana shahidi mwingine ambaye ni mke wa Dr. Slaa

slaa.jpg

Shahidi huyo aliyetajwa kuwa ni mke wa aliyekuwa katibu mkuu wa CHADEMA, Dk. Wilbroad Slaa, Bi. Jacqueline Mushumbusi ambaye yuko nje ya nchi, ushahidi wake umekataliwa kupokelewa na mahakama mpaka awepo mwenyewe au askari ambaye aliandika maelezo yake afike mahakamani kutoa ushahidi huo.

Hapo jana wakili wa mshtakiwa Peter Kibatala aliiomba mahakama iruhusu kupokelewa kwa ushahidi utakaotumwa na Bi. Mushumbusi, lakini mahakama imekataa ombi hilo ikisema upande wa utetezi hauwezi kusoma ushahidi huo na kutoa uamuzi wake wa kutaka shahidi awepo mwenyewe au askari aliyeandika ushahidi huo.

Kesi hiyo imeghailishwa mpaka kesho Oktoba 25, ambapo inatarajiwa askari aliyeandika ushahidi wa Bi. Jacquline Mushumbusi, kuwasili mahakamani hapo na kutoa ushahidi wake.

EATV
Daah... kumbe Kibatala anajali hela tuu sio haki. Bongo muvi yetu imekuwa km mwathirika wa UKIMWI alokosa dawa za kupunguza makali kwa sababu ya Lulu. Kuanzia leo simuheshimu tena Kibatala
 
Daah... kumbe Kibatala anajali hela tuu sio haki. Bongo muvi yetu imekuwa km mwathirika wa UKIMWI alokosa dawa za kupunguza makali kwa sababu ya Lulu. Kuanzia leo simuheshimu tena Kibatala
Anasimamia haki ya mtuhumiwa.
Hata kama akikutwa na hatia lakini haki zake za msingi na kila mtuhumiwa ana haki ya kutetewa.
Watu mna mahaba hadi yanafunika reasoning.
Yani hiki mnacholalamika hapa hakina tofauti na viongozi wa serikali kusema mawakili wawekwe ndani kisa wameenda polisi kutetea wale inaowatuhumu na kuamini ni waharifu wakiwemo wanasiasa waliokamatwa.
 
Back
Top Bottom