Gazeti la Raia Mwema limeandika kuwa kesi iliyofunguliwa na kina Mdee na wenzake 18 itafungua boksi ambalo limeficha siri kubwa la ‘vigogo’ waliohusika na sakata zima la wabunge 19 wa viti maalumu waliokuwa wanachama wa Chadema.
Gazeti hilo linasema mchakato mzima unaihusisha Ikulu, vigogo kutoka Tume ya Uchaguzi akiwemo Mkurugenzi wa NEC Mahera, vigogo kutoka Bunge akiwemo Spika na katibu wa bunge, vigogo kutoka ofisi ya Msajili wa vyama vya siasa.
Kwa upande wa Chadema wao wanasema wamefurahi kesi hii kufunguliwa kwa sababu wanazo nyaraka za kutosha watakazoziwasilisha mahakamani na kwa umma ambazo zitaishangaza dunia, wanaujua mchezo wote nani alihusika nani aliandaa hayo majina 19, nani aliandika removal order ya Nusrat na nani yuko nyuma yao kwa sasa. Kikosi cha mawakili wa chama kiko tayari kitawaanika wote waliohusika kwa vile wao kama chama hawana cha kupoteza.
Kwa habari zaidi soma gazeti la leo la Raia Mwema.