Kesi ya Lissu Septemba 10, 2026: IGP Wambura, DCI Kingai na CDF Mkunda waitwa kutoa ushahidi

JAJI ANASOMA UAMUZI KUHUSU MASHAIDI WA TUNDU LISSU SAMIA SULUHU SAMIA NA WENZAKE.

SEHEMU YA 3.

Hoja za msingi za upande wa Mashitaka zilikuwa 6, kwanini wanapinga:

1. Kifungu cha 281(1)

Inatokana na Kifungu cha 281(1), kwamba wakati shauri linatoka Mahakama ya chini, kinaeleza kwamba mashahidi watapewa wito wakati wa kutajwa wakati wa Committal Proceedings.

Kwa kuwa hakuwataja, basi mashahidi hao hawawezi kuitwa kwa sababu hakuwataja.

Akasema kutajwa kwa mashahidi hawa wakati huu hakutibu makosa ya Mahakama ya Hakimu Mkazi.

Na Kifungu cha 314(2) kinaeleza kwamba Mahakama itawaita pale ambapo itaona wana uwezo na wanahitajika, na ushahidi wao uendane na shauri husika.

Wakasihi Mahakama isiwaite.

2. Kuhusu Samia Hassan Suluhu, Philip Isidory Mpango na Kassim Majaliwa

Wakasema ushahidi wa Samia Hassan Suluhu, Isidory Mpango na Kassim Majaliwa hauhusiki.

Na kwamba wameshatoa ushahidi kupitia baadhi ya mashahidi ambao ni watumishi wa umma.

Na kwamba kuwaalika mashahidi hao ni kwamba Mshtakiwa atakuja kuuliza maswali ya dodoso kwa maswali ambayo ameshauliza.

Mshtakiwa akisema anataka waje ili kuthibitisha kama walitishika.

Kifungu cha 209 cha Mwenendo wa Makosa ya Jinai

Kifungu cha 209 cha Mwenendo wa Makosa ya Jinai kuhusu dodoso.

3. Kifungu cha 9 kuhusu Presidential Affairs Act

Kwamba Rais halazimiki kuitwa kuja kutoa ushahidi Mahakamani.

4. Kifungu cha 24 cha Sheria ya Huduma ya Usalama wa Taifa

Kilikuwa mahususi kupinga ombi la kumuita Mkurugenzi wa Usalama wa Taifa.

Ni kinyume cha sheria kwa taarifa za vyombo vya usalama kutolewa Mahakamani.

Na kwamba shahidi siyo material, kwa hiyo Mahakama isimuite.

Share zaidi

Weka emoji
 
JAJI ANASOMA UAMUZI KUHUSU MASHAIDI WA TUNDU LISSU SAMIA SULUHU HASSAN NA WENZAKE.

SEHEMU YA 4.

Baada ya Upande wa Mashitaka kutoa hoja hizo, Mshtakiwa alijibu hoja hizo.

Na kwamba hao ni mashahidi muhimu katika mashitaka haya kwa ajili ya fair trial.

Mahakama hii ilishapokea orodha ya hawa mashahidi.

Akaeleza kwamba wakati wa Committal Proceedings, isipokuwa Mahakama ya Hakimu Mkazi ilikataa kuchukua orodha ya mashahidi wake.

Kwa kuwa hapo Mahakama ilisharidhia mashahidi wake, Mahakama hii haiwezi kurudi nyuma na kuanza kujadili Kifungu cha 281 na 314 cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai.

Ni mashahidi ambao wana ulazima.

Kimsingi, kila mmoja ni shahidi isipokuwa kama sheria inazuia.

Akaeleza Mahakama kwamba hakuna sheria inayomtoa Rais, Makamu wa Rais, Waziri Mkuu na Mkuu wa Polisi kutokuja Mahakamani.

Sheria ya masuala ya Rais inasema kwamba Rais hatolazimishwa.

Sheria hiyo imeeleza namna ambavyo Mahakama inaweza kumfikishia wito Rais.

Sheria inasema Rais ataamua yeye kuja au kutokuja.

Lakini haizuii Mahakama kutoa wito.

Rais na hao viongozi watatu, ushahidi wao ni ushahidi muhimu.

Shitaka lililopo Mahakamani ni kutishia Serikali.

Na kwamba suala la kutishia Serikali linamgusa Rais.

Na kwamba hao wengine, ushahidi wao ni muhimu sana.

Mashahidi hao watakuja kuisaidia Mahakama endapo kosa hilo limefanyika.

Sheria haimzuii Mkurugenzi wa Usalama wa Taifa kuja kutoa ushahidi Mahakamani.

Akaeleza kwamba hata katika shauri la Khatibu Ghandi imeeleza kwamba ushahidi wa shahidi hautoki, usitolewe katika Mahakama ya wazi.

weka emoji

Share zaidi
 
Hapa kwenye examination in chief Kila mtu anatiririla lakini inapokujankwenye cross examination jamaa anajuankucheza na logic ambayo haisomewi darasani anawatega kiulaini wanaingia kingi mazima, wamekariri kujibu short answers wanakuja kuongizwa kingi wazima wazima. Wingi wa Mashahidi huaribu kesi hasa wa upande wa defence bado wale viongozi alliowaorodhesha kama Mashahidi wake wakija wakati wa cross examination Wana mmnaliza. Tatizo wanadhani jukwaa la kwenye siasa za mikutano ya hadhara wanapozungumza upande mmoja ni sawa na jukwaa la kwenye mimbari ya sheria anapoachwa uropokee wewe halafu inakuja kubanwa kuhusu ulichoropoka. Katuga anajichulia tuu point kwa kuwasulubisha wanaojiita makamanda wakati hata mgambo hawajacheza. Wanaomba MAJI ya kunywa
 
Bora ungenyamaza kuliko huu ujinga!
 
JAJI ANASOMA UAMUZI KUHUSU MASHAIDI WA TUNDU LISSU SAMIA SULUHU HASSAN NA WENZAKE.

SEHEMU YA 5.

Na kwamba wengine wameshatoa ushahidi kwa niaba ya watu wengine. Hakuna sheria inayoruhusu mtu kutoa ushahidi kwa niaba ya mtu mwingine.

Upande wa Mashitaka walitaka Mahakama izingatie Kifungu cha 281 na 314.

Mahakama, baada ya kupitia hoja za pande zote mbili, ikaangalia hoja ya msingi kama pingamizi lina mashiko au la.

Sheria inasema kwamba Mshtakiwa ataleta orodha ya mashahidi ambao waliorodheshwa katika Committal Proceedings.

Katika Mahakama ya Kisutu haikuorodhesha mashahidi wake, kweli.

Na kwamba ni kweli Hakimu Mkazi Kisutu hakuorodhesha mashahidi wake.

Mahakama yenye mamlaka inalazimika kuorodhesha mashahidi.

Kuorodheshwa au kutoorodheshwa siyo lazima kwa sababu sheria ipo hivyo; ni wakati gani wanatakiwa kuorodheshwa.

Tunajubaliana na Mashitaka kwamba kuorodheshwa siyo jambo la msingi.

Hoja ya msingi ni kwamba Mahakama inaweza kuita mashahidi wakati wowote wakati wa shauri kusikilizwa.

Pale ambapo Mahakama imepewa discretion, Mahakama inatakiwa kuitumia kwa upande wa haki.

Sasa Mahakama inaangalia hapa mashahidi:

1. Samia Suluhu Hassan
2. Isdory Mpango
3. Kassim Majaliwa

Hoja ya msingi, Mahakama inaangalia kama mashahidi hao ni relevant.

weka emoji

Share zaidi
 
Huna hata hela ya kulipia host una host free trial NameCheap, Inc., Wadanganye wajinga wenzako wa CDM
View attachment 3667778

View attachment 3667779

View attachment 3667781
Kwenye upande wa namna gani website inafanya kazi sio kazi yangu ni ya developer wa website hiyo na admin wake kwenye kilicho ndani ndicho ninachoitaji ukisogelee, yaani hicho kilicho ndani ya website.

Pia hakuna free wala trial kwa Hiyo Namecheap labda unajichanganya mwenyewe.

Mwisho naomba uelewe kwamba, Sifungamananishwi na chama chochote cha siasa, siko hapa kwa niaba ya chama chochote na wala sintokuwa mmoja wa hayo kamwe.
 
JAJI ANASOMA UAMUZI KUHUSU MASHAIDI WA TUNDU LISSU SAMIA SULUHU HASSAN NA WENZAKE

SEHEMU YA 6.

Mshtakiwa alisema anawaita kwa sababu anataka kujua kama kweli walitishika na shtaka.

Kwa upande wa Rais, sheria imesema kwamba siyo shahidi anayelazimika.

Na sheria kuwa ni wanaothibitisha upande wa Mashitaka.

Kutoitwa kwa upande wa Mashitaka, kuwaita waje kuthibitisha, basi ni jukumu la Upande wa Mashitaka kuwaita.

Upande wa Utetezi hauna ulazima wa kuwaita kuja kuthibitisha.

Hati iliyopo mbele yetu, Mashitaka alitengeneza nia ya kutisha.

Hati ya Mashitaka haijasema aliwatisha, bali akitengeneza nia.

Kwa hiyo, hoja ya walitishika au hawajatishika siyo hoja, kwa sababu siyo hoja ya msingi.

Kwa hiyo, kama siyo hoja ya msingi, ushahidi wao hauna mashiko.

Baada ya kutoka hao viongozi watatu, hoja iliyobakia ni Mkurugenzi wa Usalama wa Taifa.

Kila shauri kitaamuliwa kwa mazingira yake.

Shauri la Khatibu Ghandi, Mkurugenzi wa Usalama wa Taifa alienda kutoa ushahidi kwa upande wa Mashitaka.

Na kwamba shauri hili hajaitwa na upande wa Mashitaka.

Na sheria inasema mtoaji wa taarifa za Usalama wa Taifa ni Rais pekee, ndiye anatakiwa kujua taarifa za usalama.

Hatuwezi kumuita Mkurugenzi wa Usalama wa Taifa kwa sababu ya katazo la sheria na utofauti wa shauri lililopo.

weka emoji

Share zaidi
 
Toa pesa achana na vitu vya bure. Nyie ndio scammers. Unapiga kelele huna hata pesa za kulipia host
 
JAJI ANAMALIZA KUTOA UAMUZI AMEMLINDA SAMIA KAMA MAMA YAKE

Na mashahidi ambao hatujawagusa ni:

1. Mkuu wa Jeshi la Polisi
2. Mkurugenzi wa Mashitaka
3. Mkuu wa Majeshi

Summons zitolewe kwa ajili ya kuleta ushahidi upande wa Utetezi.

Shauri linaahirishwa hadi kesho asubuhi.

Jaji Ndunguru: Inatarajiwa Shahidi namba 5 amalize kutoa ushahidi wake.

Lissu: Kimya, hajibu.

WEKA EMOJI

SHARE
 
Toa pesa achana na vitu vya bure. Nyie ndio scammers. Unapiga kelele huna hata pesa za kulipia host
Tovuti hiyo inaendeshwa na Admin wa website hiyo na pia hipo auto-Renew 7 Years kwaiyo mimi sio mtaalamu wa maswala ya development ya website na administration, kitu pekee ninachokijua ni kile kilicho ndani ya website hiyo. Yaani Pendekezo la katiba ambalo ndilo naitaji huje na hoja kulihusu sio kupiga kelele
 
Nimejua kwanini mahakama haikutaka kupokea video.
Inajua huu mchezo, nikutaka kumpotezea tu lisu muda ili huyo mubibi awe na ahueni
Hawa watu hapa chini wanataka kutupiwa Zigo la october 29 ili Samia achomoke, ndiko tunako elekea maana wanajua kwamba Lissu atawakaanga vilivyo..,
1. Mkuu wa Jeshi la Polisi
2. Mkurugenzi wa Mashitaka
3. Mkuu wa Majeshi
 
Heche kakiwasha balaa ,mpende msipepe Lissu atakua rais wa nchi hii , mara sijui mtandao ,hakuna cha mtandao hapa, hii kesi ya lissu itatumika kama reference kwa wanasheria wengi kwa miaka ijayo
 
Acha uongo. Utakuwa umepigwa pesa wewe:
Registered On: 2026-07-15
Expires On: 2027-07-15

NameCheap ni host ya bure. Mwambie akurudishie pesa yako aliyekupiga

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…