TUNDU LISSU ANAMHOJI SHAIDI WAKE JOHN HECHE MAHAKAMANI.
SEHEMU YA 16.
Lissu: Sasa Shahidi, waeleze Waheshimiwa Majaji nilisema nini na Wadau juu ya harakati mbalimbali za kubadili mfumo huu wa Uchaguzi.
Heche: Waheshimiwa Majaji, alieleza kwamba harakati za kubadili mfumo huu wa Uchaguzi.
Harakati za Tume ya Jaji Nyarali mwaka 1991.
Tume ya Jaji Kisanga.
Tume ya Jaji Bomani.
Tume ya Jaji Joseph Sinde Warioba ya hivi karibuni.
Ambazo zote zina mapendekezo ya kubadili mfumo wa Uchaguzi.
Kuruhusu mfumo wa Kidemokrasia, uweze kufanya kuondoa huu mfumo wa chama kimoja.
Kuwapa nguvu Wananchi kuchagua nani awe Kiongozi wao.
Lissu: Naomba ufafanue hapo ukisema kuondoa mfumo wa Chama Kimoja una maana gani?
Heche: Waheshimiwa Majaji, mfumo uliopo sasa ni mfumo ambao umehodhiwa na Chama cha Mapinduzi.
Ambapo Mgombea wa CCM, ambaye yeye ndiye anaamua nani awe Mwenyekiti wa Tume, nani awe Mkurugenzi wa Tume, nani awe Mjumbe wa Tume.
Nani awe Commissioner wa Tume.
Na hata ngazi za Wilaya ni Wateule wake au wanafanya kazi chini ya Wateule wake.
Ambapo ni extension ya Urais.
Na wengi wao ni Wanachama wa Chama cha Mapinduzi.
Mfano ni Wilson Mahera, ambaye alikuwa Mkurugenzi wa Tume mwaka 2020, ila kwa sasa ni Mbunge wa CCM Jimbo la Butiama mwaka 2025.
Waheshimiwa Majaji, kwenye Uchaguzi Mkuu wa 2015, aliyekuwa Mkurugenzi wa Uchaguzi akaondolewa, Bwana Kailima, akaja Kipilimba.
Katikati ya mechi anaondolewa refa, analetwa mwingine, na Kailima ndiyo...
Vilevile, Katibu Mwenezi wa CCM, Bwana Omary Ramadhani Mapuri, sasa ni Kamishna wa Tume ya Uchaguzi.
Hii inaonyesha mfumo huu umehodhiwa na Chama Kimoja.
WEKA EMOJI KAMA UNASOMA
SHARE ZAIDI UJUMBE UFIKE MBALI.