Kesi ya Lissu Septemba 10, 2026: IGP Wambura, DCI Kingai na CDF Mkunda waitwa kutoa ushahidi

Kesi ya Lissu Septemba 10, 2026: IGP Wambura, DCI Kingai na CDF Mkunda waitwa kutoa ushahidi

TUNDU LISSU ANAMHOJI SHAIDI WAKE JOHN HECHE MAHAKAMANI

SEHEMU 11.

Lissu: Sasa turudi kwenye tarehe 03 April mwaka jana.

Umeiambia Mahakama kuwa mkutano wa 03 April mwaka jana ulikuwa wa kuwafahamisha watia nia kuwa bila mabadiliko gani mlikuwa mnayataka?

Heche: Waheshimiwa Majaji, ni mabadiliko ya Kikatiba na kisheria yanayoongoza uchaguzi.

Katiba, hasa kifungu cha 74, kinachounda hiyo.

Uwepo wa Katiba mbovu.

Lissu: Shahidi, kama nimekusikia sawasawa, kuwa msimamo huu wa “No reforms, No election” ulitolewa na kikao cha tarehe 03 December 2024.

Baada ya msimamo huo nini kilifuata?

Heche: Waheshimiwa Majaji, msimamo huo ulitangazwa hadharani na Mwenyekiti wa wakati huo, Freeman Mbowe.

Baada ya kuwa tumetoka uchaguzi, kwamba hata wale wachache walioshinda hawakutangazwa.

Kwa hiyo Mbowe akatangaza kwamba uchaguzi hauwezekani kwa njia hizi za kawaida.

Waheshimiwa Majaji, hilo tamko lilitolewa tarehe 10 December 2024.

Lissu: Baada ya Tanzania kutamka hilo azimio, kitu gani kilifuatia?

Heche: Waheshimiwa Majaji, tulikutana Kamati Kuu tarehe 19 December 2024.

Lissu: Kamati Kuu ya tarehe 19 December ilijadili kitu gani?

Heche: Waheshimiwa Majaji, miongoni mwa mambo mengi yaliyoazimiwa, Kamati Kuu iliazimia kupeleka huo msimamo katika Baraza Kuu la tarehe 20 January 2025.

Lissu: Waeleze Waheshimiwa Majaji, kitu gani kilitokea katika hilo Baraza Kuu la tarehe 20 January?

Heche: Waheshimiwa Majaji, Baraza Kuu la tarehe 20 January lilipokea ajenda hii na kuunga mkono azimio hilo.

Heche: Waheshimiwa Majaji, nikisema Kamati Kuu ya chama namaanisha Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo.

Na nikisema Baraza Kuu la chama namaanisha Baraza Kuu la Chama cha Demokrasia na Maendeleo.

Lissu: Unamaanisha nini?

Heche: Kamati Kuu ni chombo cha utendaji wa chama, na Baraza Kuu ni chombo cha utungaji wa sera na usimamizi wa chama.

Lissu: Eleza kitu gani kilitokea katika huo Mkutano Mkuu.

Heche: Mkutano Mkuu ulipitisha azimio la “No Reforms, No Election” na ulimchagua Mwenyekiti Tundu Antipas Lissu, Makamu Mwenyekiti Bara John Wegesa Heche na Makamu Mwenyekiti Zanzibar Said Mzee Saidi.

Lissu: Specific kuhusu “No Reforms, No Election”, Mkutano Mkuu uliamua nini?

Heche: Kuandaa mpango wa utekelezaji, kuwaelimisha wanachama na wananchi juu ya kwanini tumefikia uamuzi wa “No Reforms, No Election”.

Lissu: Waeleze Waheshimiwa Majaji, baada ya Mkutano Mkuu kuamua hivyo, Kamati Kuu iliamua nini?

Heche: Waheshimiwa Majaji, Kamati Kuu iliyofanyika Bagamoyo ikaazimia maazimio ya Mkutano Mkuu yatekelezwe.

Kwa maana kwamba Mwenyekiti Tundu Antipas Lissu, Makamu Mwenyekiti Bara John Wegesa Heche, Makamu Mwenyekiti Zanzibar Said Mzee Saidi, Katibu Mkuu John Mnyika, Manaibu wote wa Bara na Zanzibar, pamoja na wenyeviti wa kanda 10 za kichama, tukutane na viongozi wa taasisi mbalimbali.

Viongozi wa kitaifa wakutane na viongozi kwenye level ya kitaifa.

Tukutane na viongozi wa dini, kwa maana ya dini zote.

Tukutane na mabalozi (Diplomats) wanaowakilisha nchi zao hapa Tanzania.

Wazee maarufu, NGOs (Asasi za Kiraia).

Kuwaeleza msimamo wetu huo, kuwaomba waunge mkono huo msimamo na uchaguzi ufanyike huru na wa haki.


WEKA EMOJI KAMA UNASOMA

SHARE ZAIDI UJUMBE UFIKE.
 
Sio wote, sema machawa wote wa muuaji Samia. Hadi hapo kwenye hii kesi imeshaonyesha mahakama haziko huru, na upuuzi wote wa serekali dhidi ya cdm uko wazi kama uchi wa mbuzi.
Dogo acha kujipendekeza kila comment yangu.
 
Heche is out of context - Anatakiwa kuleta ushahidi kwamba Lissu hakuhamasisha uasi
lissu alijitetea kwa kusema "Kesi hii ni ya kisiasa, kiuonevu na yenye lengo la kudhoofisha upinzani nchini", so mbona hii kwenye sheria hipo sahihi wao Jamhuri wanathibitisha uhaini, yeye anajitetea kwa kusema huu sio uhaini bali ni hila za kisiasa na anatoa ushaidi wa ukandamizaji wa kisiasa kiasi Mahakama ione je Ushaidi wa Jamhuri licha ya sehemu kubwa ulishakataliwa na mahakama kama vile hile video ya ushaidi, Masahidi wa vificho D's .

Pia PW's wameandika ushaidi wao wamesaini wao, na kuwalazimisha D's kuwa mashaidi wakati walikuwa waalifu waliofanya uharifu baada ya kushawishiwa na maneno ya lissu aliyowaikuyatoa and at the same time hapo hapo maneno hayo yamekataliwa maakamani kwa vielezo videos..
 
TUNDU LISSU ANAMHOJI SHAIDI WAKE JOHN HECHE MAHAKAMANI

SEHEMU YA 12.

Lissu Sasa Shahidi shitaka linalo nikabili linase sema nimesema neno lenye maudhui kiaini

Naomba Uwaeleze Majaji Kuhusu Waandishi wa habari

Heche: Miongoni mwa waru nilio wataja ni Jukwaa la Waharii.

Lissu: Sasa Shahidi katika hao wote ulo wataja kamati pamoja na hao wadau nataka mimi na wewe tulikwepo pamoja

Heche:
Tulimtembelea Balozi Wa Marekani
Tulimtembelea Mzee Warioba / alikuwa pamoja na Butiku

Lissu ni nani..?

Heche: Butiku ni Mwenyekiti wa
Mwl.Nyerere foundation

Lissu Wengine

Heche Tulimtembelea Rais wa Baraza la katoliki Tanzania ( Askofu pisa)
Legal and Human Rights center.

Hizo ni ambazo mimi na Mwenyekiti tulishiriki.

Lissu Kwa Sababu tulikuwa Pamoja Waeleze Waheshimiwa majaji naji alikuwa Kiongozi na msemaji Mkuu wa ujumbe wetu !.

Heche Msemaji wa Ujumbe wetu alikuwa Mwenyekiti wa chama cha Demokrasia na Maendeleo Tundu Antipas Lissu

Lissu Waeleze Waheshimiwa majaji kwa kumbukumbu zako au ufahamu wako

Kuhusu Mimi Kuzungumzia matatizo ya mfumo wetu wa uchaguzi na Katiba.
.

Heche:

Jaji Ndunguru Sasa hizi ni Sa 7 na Dakika 4

Tu break hapa alafu tukirudi atakuja kujibu

Upande wa Mashitaka unasemaje

Ajuaye ni sawa Mheshimiwa

Jaji Ndunguru: Kwa hiyo Shahidi utaishia hapo

Tutarudi Mahakamani saa 8 na nusu.

MAJAJI WANATOKA

TUKUTANE SAA 8:30.


WEKA EMOJI KAMA TUPO PAMOJA.
 
Baada ya jana Septemba 9, 2026 Makamu Mwenyeekiti wa CHADEMA Bara, Joun Heche kupanda Kizimbani na kuanza kutoa ushahidi wake katika Kesi ya Uhaini inayomkabili Mwenyeekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu na leo tena anaendelea.


Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala Ndogo ya Dar es Salaam leo Septemba 10, 2026, huenda ikatoa uamuzi kuhusu pingamizi la Serikali katika kesi ya uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu.

Pingamizi hilo linahusu ombi la Lissu la kuwaita viongozi na maafisa mbalimbali wa Serikali, wakiwemo Rais Samia Suluhu Hassan, kuwa mashahidi wa utetezi.

Miongoni mwa wanaosubiriwa ni Rais Samia, Makamu wa Rais Mstaafu Philip Mpango, Waziri Mkuu Mstaafu Kassim Majaliwa, CDF Jenerali Jacob John Mkunda, IGP Camilius Wambura na viongozi wa vyombo vya usalama.

Kinachoendelea kutoka Mahakamani - Shahidi John Heche akisalimiana na Dada yake Tundu Lissu.


Tundu Lissu ameshafika Mahakamani tayari kwa mwendelezo wa kesi inayomkabili, kwa ajili ya kuendelea kutoa utetezi wake katika kesi ya uhaini namba 19605/2025.

Leo, Septemba 10, 2026, tunaendelea na Part 387 ya kesi inayomkabili Mwenyekiti wetu wa Chama, Mhe. Lissu, ambapo shahidi wa tano wa utetezi, John Wegesa Heche, anaendelea kutoa ushahidi. Makamu Mwenyekiti amefika mapema katika viunga vya Mahakama, huku tukisubiri Majaji kuingia.

Wasaidizi wa Majaji kitaaluma ni Mahakimu wakazi wa Mahakama za wilaya au Mahakama za Hakimu Mkazi walioteuliwa kufanya kazi hiyo ya usaidizi kwa Majaji kwa maana ya kuwafanyia research za mambo mbalimbali ya Kisheria.

Kwahiyo kwa vile Majaji ni watatu na wasaidizi wa majaji wapo watatu hawa Mahakimu. Sasa hao mahakimu walishaingia na karani alikwisha ingia.

Kumbukeni jana Majaji walisema wataanza na uamuzi wa kwamba je wale mashahihidi wa Mhe. Tundu Lissu ambao ni Samia Suluhusu Hassan, Philip Mpango na Kassim Majaliwa wataitwa kuja kutoa ushahidi au hawataitwa? Ndo tutaanza nacho kabla ya John Heche kuendelea na ushahidi wake.

Majaji wameshaingia na Mwenyekiti Lissu pia ameingia.

Tunasubiri mambo kuanza na kuendelea. Mawakili wa serikali na wao wameingia.

Ajuaye wakili wa Serikali Mkuu amesimama na kutambulisho jopo lake.

Amesema shauri limekuja kwaajili ya kusikilizwa na Upande wa Jamhuri tupo tayari kuendelea.

Jaji Ndunguru anamuuliza Mshtakiwa kwamba unasemaje?

Mhe. Lissu anajibu kwamba yupo tayari

Jaji Ndunguru anamwambia Shahidi kwamba Mahakama inakukumbusha kuwa bado uko chini ya kiapo.

Lissu: Shahidi habari yako, habari za toka jana
Heche: Salama Mwenyekiti
Lissu: Waeleze majaji matukio mengine ya mauaji nyakati za uchaguzi ambayo hukuyataja jana

Heche: Waheshimiwa majaji tukio jingine lilitokea kwenye Uchaguzi mdogo Igunga aliuwawa Mbwana Masudi mwaka 2011 baada ya aliyekuwa Mbunge wa Igunga kujiuzulu na ilifanyika By-Election.
Lissu: Huyu Mbwana Masudi alikuwa nani aliuwawa namna gani na nani alihusika?

Heche: Mbwana Masudi alikuwa kiongozi wa CHADEMA kutoka Ubungo ambapo alienda kushiriki kampeni za uchaguzi Igunga, aliuwawa na viongozi na wanachama wa CCM na hakuna hatua zozote za kisheria zilizochukuliwa dhidi ya wale watu waliomuua

Lissu: Waeleze Majaji ufahamu wako iwapo kuna wanachadema walikamatwa kwenye uchaguzi huo wa Igunga

Heche: Kabla na wakati wa uchaguzi walikamatwa mojawapo ni Mwenyekiti wa Chama wa Kinondoni wakati huo Henry Kileo na Mkurugenzi wa Ulinzi wakati huo Wilfred Lwakatare walishtakiwa wote kwa kesi kubwa ya ugaidi. Kileo alishtakiwa Tabora na Mahakama baadae ilitupilia mbali hiyo kesi na kumuachia huru. Wilfred Lwakatare alishtakiwa mahakamani hapa Dar es Salaam na baadae Mahakama ilimuachia huru baada ya kuwa wamekaa gerezani muda mrefu maana kesi hizo hazina dhamana.

Lissu: Endelea na matukio mengine ya mauaji wakati wa Uchaguzi mdogo na Uchaguzi mkuu

Heche: Matukio ya mauaji yanayotokana na uchaguzi ni mengi mno. Mwaka 2020 kiongozi wa CHADEMA Tunduma aliuwawa, Mwanza aliuwawa kiongozi wa BAVICHA jimbo la Nyamagana

Lissu: Waeleze majaji kama kuna mauaji mengine yanayohusisha wananchi na sio viongozi wa chadema

Heche: Kuna mauaji yanayohusisha wananchi nimeyasoma kwenye vyombo vya habari wakati wa chaguzi za Serikali za mitaa, kuna maeneo ambayo yalitokea Shinyanga, Tunduma.

Lissu: Waeleze majaji juu ya mauaji Pemba na Zanzibar
Katuga: Mshtakiwa anauliza shahidi aelezee mauaji Pemba maana yake ana suggest jibu
Lissu: Shahidi kama anajua atasema anajua na kama hajui atasema hajui

Sehemu ya 388

Makam Mwenyekiti upande wa Bara, John Heche anaendelea kutoa Ushahidi wake

Jaji Ndunguru anasema nadhani hilo swali liondoe au muulize tu kama anakumbuka mauaji mengine

Lissu: Waeleze majaji mauaji mengine yaliyofanyika nyakati za uchaguzi

Heche: Waheshimiwa majaji nakumbuka mauaji makubwa wakati wa Uchaguzi wa mwaka jana yaliyofanywa na vyombo vya Dola na Polisi, mamia ya watu waliuwawa hasa Dar es Salaam, Mbeya, Arusha, Mwanza, Geita, Tarime na maeneo mengine.

Lissu: Waeleze majaji matukio mengine ya uonevu dhidi ya raia tofauti na mauaji

Heche: Matukio mengine ya uonevu ni pamoja na watu kutekwa, kupotezwa, ripoti ya TLS inasema kuna watu 718 wametekwa na kupotezwa, kati ya hao kuna Wanachama wa CHADEMA, viongozi wa CHADEMA, viongozi wengine wa Vyama vya siasa kama CCM ambao wameonyesha msimamo wao dhidi ya Serikali hii.

Lissu: Ripoti ya TLS ni ya mwaka gani, matukio yalitokea lini

Heche: Ripoti ni ya Mwaka 2026 ila matukio hayo ni ya muda mrefu, yapo ya mwaka huu, mwaka jana, mwaka juzi na mengine ni ya tangu 2016, 2017, 2018 na miaka mingine.

Lissu: Waeleze majaji kuhusu matukio ya watu kutekwa na kupotezwa unayoyafamu hasa 2016, 2017

Heche: Waheshimiwa Majaji matukio ya 2016 na 2017 ni pamoja na Kutekwa kwa Ben Saanane aliyekuwa Msaidizi wa Mwenyekiti Freeman Mbowe, Azori Gwanda aliyekuwa Mwandishi wa habari wa Mwananchi, Kanguye aliyekuwa Mwenyekiti wa Halmashauri mojawapo ya Wilaya huko Kigoma.

Lissu: Waeleze Majaji ufahamu wako kuhusu hawa watu endapo walipatikana au vipi

Heche: Mpaka leo hawajawahi kupatikana; familia ya Ben Saanane hawajawahi kuambiwa alipo Ben, vile Azori Gwanda na Kanguye vilevile

Lissu: Waeleze matukio mengine ya watu kutekwa

Heche: Waheshimiwa Majaji matukio mengine ni kutekwa kwa Balozi Humphrey Polepole alikuwa Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, alikuwa Balozi, Mbunge, Mkuu wa Wilaya. Kutekwa kwa Mdude Nyagali mwanachama wa CHADEMA kutoka Mbozi tangu 2024 mpaka leo hajulikani alipo.

Kutekwa kwa Deusdedith Soka Mwenyekiti wa Bavicha Temeke, Jacob Mlay alikuwa Katibu wa CHADEMA Temeke, Daniel Chonchori anatokea Jimbo la Tarime na alikuwa Mjumbe wa Halimashauri Kuu ya CCM Taifa, Sinda Geteba huyu alikuwa mgombea wa Uchaguzi Kata ya Tarime kwenye uchafuzi wa mwaka jana na familia yake ilisema alichukuliwa na RCO wa Tarime, Bhurure Tall alikuwa Mwanachama wa CHADEMA, Amani Manengelo alikuwa Mwenyekiti wa Bavicha Mkoa wa Mwanza, Nyangoko Kina anatoka Sirari Tarime ni Mwananchi tu wa jimbo la Tarime, Dionizi Kipanya alikuwa Kiongozi wa CHADEMA Sumbawanga mjini, Siza Keheta kutoka Tarime. Waheshimiwa majaji orodha ni ndefu kwasasa naomba niseme hao

Lissu: Shahidi jana wakati unatoa ushahidi ulielezea kesi iliyokuhusu wewe na aliyekuwa Mwenyekiti Mbowe na viongozi wengine, naomba uwaeleze majaji ukiachia hiyo kesi, eleza zingine unazozifahamu za aina hiyo zinazokuhusu wewe au viongozi wenzako wa chama

Heche: Kuna kesi ya Ugaidi iliyomuhusu Freeman Mbowe kesi ya Mwaka 2021 na baadae aliachiwa na tukaona picha yake ya kwanza wakati huo akiwa Ikulu na Rais Samia Suluhu, msemo maarufu ni kuwa “kutoka Ukonga mpaka Ikulu”

Lissu: Alikaa gerezani muda gani?

Heche: Miezi 8 waheshimiwa majaji. Siku hiyo mwenyekiti anakamatwa tulikamatwa nae tulikuwa Mwanza.

Tulikuwa pia na viongozi wa dini na wazee; Dkt. Azaveli Lwaitama kwasasa ni Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Chama na Mwanachama wa CHADEMA, tulikamatwa na Mzee Masinde alikuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini CHADEMA, John Pambalu Mwenyekiti wa BAVICHA wakati huo na kwasasa ni Mkurugenzi wa Organization na Mafunzo Makao Makuu ya CHADEMA, Baba Askofu Emmaus Mwamakula, Mwenyekiti wa Njombe ambaye kwasasa ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema Dada Rose Mayemba.

Sehemu ya 389

Lissu:
Shahidi umesema mlikamatwa wewe na Mwenyekiti na hao wengine, ila Mwenyekiti pekee ndio alifunguliwa kesi ya Ugaidi. Nyie wengine nini kiliwatokea?

Heche: Tulishikiliwa vituo mbalimbali vya Polisi ikiwemo Nyakato, Central Police Mwanza.

Tulikaa kwa siku kadhaa mimi nilikaa central Police Mwanza, Police walipekua nyumbani kwangu na baadae nikaambiwa niwe naripoti kituo cha Polisi, wengine walipelekwa Majumbani kwao kama Rose alipelekwa Njombe, Mzee Lwaitama alipelekwa Dar es Salaam.

Lissu: Endelea uwepo wa kesi zingine za aina hiyo

Heche: Oktoba 22, 2025 nilikamatwa hapo nje ya Mahakama hii, Nilikuwa nakuja kwenye kesi hii, nikaambiwa nina tuhuma za kuvuka mpaka kinyume cha sheria na nilishikiliwa Central Police Dar es Salaam na niliambiwa nasafirishwa kwenda Tarime na nilianza safari mpaka tulipofika Dodoma usiku, nikapelekwa kituo cha Polisi Mtumba Dodoma ambapo nilikiwekwa kwenye selo ya peke yangu mpaka nilipokuja kutolewa tarehe 4/11/2025 na kusafirishwa kurudishwa Dar es Salaam.

Waheshimiwa Majaji nilipokuwa kituoni ndugu zangu hawakujulishwa na wala hawakuruhusiwa kuniona mpaka nilipogomea kula na kunywa maji kwa siku tatu:

Lissu: Waeleze Majaji nini kilitokea uliporudishwa Dar es Salaam.

Heche: Niliporudishwa Dar es Salaam nilipelekwa kituo cha Polisi Oysterbay na niliwakuta Nassoro Katuga, Thawabu Issa, Job Mrema.

Lissu: Waeleze Majaji kitu gani kilitokea

Heche: Niliwakuta Mawakili wa Serikali Wakuu na pale kulikuwa na watu wengi siku hiyo wakiwa na majeraha na wengine wameumizwa sana na kukikuwa na watu wengi sana mpaka pale kwenye vyumba vya kwenye korido na hawa mawakili walikuwa na George Bagyemu Deputy ZCO na baadae waliingia kwenye chumba fulani.

Lissu: Waeleze majaji Nini kilitokea ?

Heche: Nilipelekwa kwenye chumba ghorofa ya kwanza, nikasomewa charge ya Ugaidi ya kuchoma vituo vya mwendokasi kutoka Kimara mpaka Ubungo, na hadi Magomeni. Alinisomea askari ambaye aliletwa na DZCO George Bagyemu.

Lissu: Ilikuwaje baadae ya kusomewa hiyo charge?

Heche: Sikuwa tayari kutoa maelezo yangu niliandika tu particulars zangu na nilipelekwa kituo cha Polisi Mburahati.

Lissu: Ulikaa muda gani Oysterbay Police?

Heche: Nilikaa hadi saa nne usiku lakini badae nilipelekwa Kituo cha Polisi Kijitonyama wakasema kimejaa ndio nikapelekwa Mburahati Police.

Lissu: Ulipofika Mburahati kitu gani kilitokea?

Heche: Nilikaa Mburahati kutoka tarehe 4 October mpaka tarehe 10 Mwezi wa 11, 2025.

Lissu: Ilipofika Novemba 10 nini kilitokea? Waeleze Majaji

Heche: Waheshimiwa Majaji nilirudishwa kituo cha Polisi Oysterbay na nilikutana na Naibu Katibu Mkuu Amani Golugwa ambaye alikuwa amekamatwa huko Arusha, Godbless Lema Mjumbe wa Kamati Kuu, Boniface Jacob nae Mjumbe wa Kamati Kuu., nao walikuwa wamekamatwa. Tulimkuta ZCO Mafwele alikuwepo pale, alituambia tudhaminiwe tuondoke na kesho yake tukaripoti central Police Dar es Salaam na baada ya hapo tuliambiwa tuendelee na shughuli zetu mpaka leo.

Sehemu ya 390

Lissu:
Ulisema umekuwa Kiongozi wa Chama toka mwaka 2008 umekuwa diwani na baadae 2011 ukawa Mwenyekiti wa BAVICHA miaka yote hii, kuna kiongozi yoyote Mkuu wa Chama ambae hakukamatwa kwa sababu moja ama nyingine?

Heche: Sina Kumbukumbu ya Kiongozi yeyote ambae hajawai kukamatwa hadi leo.

Dr. Wilbroad Slaa, Wabunge akina Lema, Msigwa, Mwenyekiti Mbowe Mwenyewe.

Lissu: Kwenye kesi hii mimi nimekamatwa Tarehe 09/04 Je unafahamu kesi nyingine ya kwangu?
Heche: Hii sio kesi pekeee ambayo naifahamu uliwahi kukamatwa Tarime maeneo ya Nyamongo miaka ya 2013 na tulipokuwa Bungeni umekamatwa mara nyingi sana.

Na kati ya mwaka 2015 na 2020 umekamatwa mara kadhaa kwa kesi za Uchochezi na vitu kama hivyo.

Lissu: Nilipokamatwa Tarime tuhuma ilikuwa nini na nini kilitokea?
Heche: Nakumbuka kuna watu waliuwawa mgodini na Mhe. Tundu Lissu alikuja pale kwasababu kulikuwa na msuguano kati ya Polisi na familia zilizopoteza ndugu, Mhe. Lissu alikuja kama mtetezi wao hivyo alikakatwa na kufunguliwa kesi.

Lissu: Nilikuwa nani kipindi hicho?
Heche: Waheshimiwa Majaji alikuwa ni Mbunge na Mkurugenzi wa Sheria wa Chama.
Lissu: Hiyo kesi ya Uchochezi Tarime iliyokuwa inanikabili iliishaje?
Heche: Iliisha kama kesi hizi zingine kwenye vituo vya Polisi haikuendelea.
Lissu: Hizo kesi zingine ulizoziita za Uchochezi nazo ziliishaje?
Heche: Hizo kesi ziliisha hivyo hivyo na zingine tuliambiwa Serikali imezifuta kwasababu haikuwa na interest ya kuendelea nazo.
Lissu: Kwa ufahamu wako je nimewahi kutiwa hatiani na Mahakama yoyote nchini?
Heche: Hakuna kesi hata moja amewahi kukutwa na hatia katika kesi hizi nilizosema.
Lissu: Waeleze kwa ufahamu wako wa kesi za Wanachama wa Chadema waliofungwa na kukutwa na hatia?
Heche: Ukiachilia na ile kesi yetu ya Kisutu sina kumbukumbu na viongozi wakuu ambao wamewahi kukutwa na hatia hata mmoja.

Lissu: Waeleze Majaji kwa unavyofahamu wewe kama kuna chama kingine chochote ambacho wapo viongozi wake wanakamatwa kama Chadema?

Heche: Sina kumbukumbu za viongozi wa Chama kingine wamewahi kukamatwa.

Lissu: Hivi vitendo vya kukamata Viongozi na Wanachama na kuwapoteza. Lengo la haya mambo haya kutokea ni nini???

Heche: Waheshimiwa majaji lengo la kukamata kwao ni kuwatisha viongozi hao wa Chadema na wengine, kuwakatisha tamaa kusimamia Misimamo ya Chama mbalimbali ambayo wanakuwa wameichukua.

Lissu: Waeleze Majaji kwa ufahamu wako uhalali wa vitendo hivyo kwa kuwatisha na kuwakamata?

Heche: Hakuna uhalali wowote wa kuyafanya hayo, hakuna uhalali wa kisheria wala ki utu wa kukamata watu na kuwanyanyasa. Ninachokiona ni kile alichokisema Katibu Mkuu wa CCM wa Wakati huo kuwa unatumia Dola kuendelea kubaki kwenye dola kwa CCM.

Lissu: Nini kiliendelea Tarehe 07/09/2017 Dodoma Bungeni?
Heche: Mchana wa Tar. 07/09/20217 mchana akiwa ameenda kula Chakula cha mchana nyumbani kwake, alivamiwa na watu wasiojuliana, aliumizwa vibaya sana kwa risasi za moto. Alishambuliwa kwa risasi mchana kweupe.
Lissu: Wewe ulikuwa wapi siku hiyo?
Heche: Siku hiyo nilikuwa Bungeni Dodoma na tulikuwa na Mhe. Tundu Lissu.
Lissu: Kitu gani kilitokea kabla ya hilo tukio na baada ya hilo tukio?
Heche: Kabla ya hilo Shambulio tulikuwa Bungeni tulikuwa tunajadili Mkataba wa River Songwe Basin na nakumbuka Mhe. Lissu alichangia siku hiyo.

Sehemu ya 391 itaendelea hapa.............
Kwa maelezo haya ,CCM kinakuja kuwa chama kisicho na dola
 
TATHIMINI MPAKA HAPA
1. Heche anakubali kulikuwa na “mpango wa utekelezaji”
2. Heche anakubali viongozi walitakiwa kuhamasisha watu na taasisi kuunga mkono msimamo
3. Heche anakubali Lissu alikuwa msemaji mkuu wa ujumbe
4. Heche anakubali Lissu alihusika kwenye campaign ya kuipeleka “No Reforms, No Election” kwa wadau
5. Heche anakubali Lissu alikuwa akizungumza kuhusu matatizo ya mfumo wa uchaguzi na Katiba
6. Heche anakubali “No Reforms, No Election” ilikuwa msimamo rasmi wa CHADEMA
7. Heche anakubali Lissu alikuwa sehemu ya leadership iliyotakiwa kutekeleza resolution

“Mpango wa utekelezaji”🔴🔴🔴
Mobilisation ya wanachama/wananchi🔴🔴
Kukutana na viongozi, NGOs, diplomats etc.🔴🔴
Lissu alikuwa msemaji mkuu🔴🔴🔴
Lissu alikuwa sehemu ya leadership ya implementation🔴🔴
Lissu alikuwa active kwenye advocacy🔴🔴
No Reform No Election ilikuwa official resolution🔴🔴
 
TATHIMINI MPAKA HAPA
1. Heche anakubali kulikuwa na “mpango wa utekelezaji”
2. Heche anakubali viongozi walitakiwa kuhamasisha watu na taasisi kuunga mkono msimamo
3. Heche anakubali Lissu alikuwa msemaji mkuu wa ujumbe
4. Heche anakubali Lissu alihusika kwenye campaign ya kuipeleka “No Reforms, No Election” kwa wadau
5. Heche anakubali Lissu alikuwa akizungumza kuhusu matatizo ya mfumo wa uchaguzi na Katiba
6. Heche anakubali “No Reforms, No Election” ilikuwa msimamo rasmi wa CHADEMA
7. Heche anakubali Lissu alikuwa sehemu ya leadership iliyotakiwa kutekeleza resolution

“Mpango wa utekelezaji”🔴🔴🔴
Mobilisation ya wanachama/wananchi🔴🔴
Kukutana na viongozi, NGOs, diplomats etc.🔴🔴
Lissu alikuwa msemaji mkuu🔴🔴🔴
Lissu alikuwa sehemu ya leadership ya implementation🔴🔴
Lissu alikuwa active kwenye advocacy🔴🔴
No Reform No Election ilikuwa official resolution🔴🔴
Tathmini yako nzuri, lakini bado imeegemea upande mmoja kiasi kwamba Fact za msingi za kesi hii hazipo kwenye Tathmini hii.
 
Yaani hawajui tuh kuanzisha hii kesi inafanya wanachi kuyajua mambo mengi zaidi ni kama kujipiga risasi wenyewe tuh
Hiyo Syndicate yenu, tunaijua. Tafuteni njia nyingine.

Mnaishia kutukana kuchafua watu majina huku wenzenu Waislamu wakiwekeza na kuchukua kila kitu. Nyie mko busy na akina Warioba with old styles

Shida iko wapi TEC nao wakiwekeza hata kwenye BRT? Ushamba unawasubua na ufia dini badala ya maendeleo
 
Mpaka muda huu (kwa mtazamo wangu hivyo sihitaji kushambuliwa na mtu yeyote yule), waliojitahidi kutoa ushahidi wao kwa utulivu na mpangilio mzuri ni:-
1. John Mnyika
2. John Heche (pamoja na kwamba hajamaliza)
3. Brenda Rupia
4. Amani Golugwa.
 
TATHIMINI MPAKA HAPA
1. Heche anakubali kulikuwa na “mpango wa utekelezaji”
2. Heche anakubali viongozi walitakiwa kuhamasisha watu na taasisi kuunga mkono msimamo
3. Heche anakubali Lissu alikuwa msemaji mkuu wa ujumbe
4. Heche anakubali Lissu alihusika kwenye campaign ya kuipeleka “No Reforms, No Election” kwa wadau
5. Heche anakubali Lissu alikuwa akizungumza kuhusu matatizo ya mfumo wa uchaguzi na Katiba
6. Heche anakubali “No Reforms, No Election” ilikuwa msimamo rasmi wa CHADEMA
7. Heche anakubali Lissu alikuwa sehemu ya leadership iliyotakiwa kutekeleza resolution

“Mpango wa utekelezaji”🔴🔴🔴
Mobilisation ya wanachama/wananchi🔴🔴
Kukutana na viongozi, NGOs, diplomats etc.🔴🔴
Lissu alikuwa msemaji mkuu🔴🔴🔴
Lissu alikuwa sehemu ya leadership ya implementation🔴🔴
Lissu alikuwa active kwenye advocacy🔴🔴
No Reform No Election ilikuwa official resolution🔴🔴
Ukute wee jamaaa ni samuya
Ni vile tuu umejificha kwa jina la presidee wa china
 
Back
Top Bottom