Kesi ya Lissu Septemba 10, 2026: IGP Wambura, DCI Kingai na CDF Mkunda waitwa kutoa ushahidi

Kesi ya Lissu Septemba 10, 2026: IGP Wambura, DCI Kingai na CDF Mkunda waitwa kutoa ushahidi

TUNDU LISSU ANAMHOJI SHAIDI WAKE JOHN HECHE MAHAKAMANI

SEHEMU YA 9.

Lissu: Waeleze Waheshimiwa Majaji, baada ya hilo shambulio kitu gani kilifuatia?

Heche: Baada ya hilo tukio, Mheshimiwa Tundu Lissu alisafirishwa, ambapo alitibiwa kwa muda mrefu na baadaye Ubelgiji.

Lissu: Waeleze Waheshimiwa Majaji, hizi taarifa za kushambuliwa kwangu, Nairobi kisha Ubelgiji, wewe ulizijuaje?

Heche: Nilizijua kwa sababu nilikuwa naye Bungeni.

Hata hivyo, nilimtembelea Nairobi alipokuwa hospitalini.

Vilevile, aliporudi nyumbani nilizungumza naye.

Lissu: Utaratibu wa matibabu ya Mbunge ndani au nje ya nchi ukoje?

Heche: Mbunge anapopata matatizo ndani ya nchi anatibiwa na bima.

Lakini kama ni nje ya nchi, Ofisi ya Katibu wa Bunge inachukua majukumu ya kulipia matibabu, eneo unalofikia na msaidizi wako mmoja.

Lissu: Waeleze Waheshimiwa Majaji kama utaratibu huo unaosema ulitumika katika matibabu yangu.

Heche: Waheshimiwa Majaji, hakulipiwa matibabu, msaidizi wala eneo alilokuwa amefikia.

Lissu: Waeleze Waheshimiwa Majaji, kwa vile sikutibiwa kwa utaratibu wa Kibunge uliousema, waeleze sasa Waheshimiwa Majaji nilitibiwaje?

Heche: Waheshimiwa Majaji, chama kililipia matibabu.

Michango ya marafiki na TLS pia.

Na pia, hivyo ndiyo ninavyoweza kusema.

Kulikuwa na kuchangiwa na Watanzania na watu wengine Nairobi, ila hasa ni Watanzania.

Lissu: Sasa Shahidi, unasema kipindi hicho nilikuwa Mbunge. Waeleze Waheshimiwa Majaji—

Heche: Waheshimiwa Majaji, Mheshimiwa Tundu Lissu alivuliwa Ubunge.

Lissu: Waeleze Majaji kuhusu Ubunge wangu.

Heche: Alikuwa nje ya nchi kwa matibabu.

Mwaka sikumbuki vizuri.

Ila alivuliwa Ubunge sababu ya utoro.

WEKA EMOJI KAMA UNASOMA

SHARE ZAIDI UJUMBE UFIKE MBALI.
Ila haya madaraka yanafanya usiheshimu utu wa Binadamu yaani mtu Yuko nje kwa matibabu alafu anaambiwa ni mtoro anavuliwa ubunge huu ni unyama wa kiasi gani
 
TATHIMINI MPAKA HAPA
1. Heche anakubali kulikuwa na “mpango wa utekelezaji”
2. Heche anakubali viongozi walitakiwa kuhamasisha watu na taasisi kuunga mkono msimamo
3. Heche anakubali Lissu alikuwa msemaji mkuu wa ujumbe
4. Heche anakubali Lissu alihusika kwenye campaign ya kuipeleka “No Reforms, No Election” kwa wadau
5. Heche anakubali Lissu alikuwa akizungumza kuhusu matatizo ya mfumo wa uchaguzi na Katiba
6. Heche anakubali “No Reforms, No Election” ilikuwa msimamo rasmi wa CHADEMA
7. Heche anakubali Lissu alikuwa sehemu ya leadership iliyotakiwa kutekeleza resolution

“Mpango wa utekelezaji”🔴🔴🔴
Mobilisation ya wanachama/wananchi🔴🔴
Kukutana na viongozi, NGOs, diplomats etc.🔴🔴
Lissu alikuwa msemaji mkuu🔴🔴🔴
Lissu alikuwa sehemu ya leadership ya implementation🔴🔴
Lissu alikuwa active kwenye advocacy🔴🔴
No Reform No Election ilikuwa official resolution🔴🔴
Unateseka sana aiseee
 
Tathmini ni taaluma ya watu, acha kujitia aibu hapa.
 
Watu wanasoma kinachoendelea mahakamani wewe unapoteza umakini wa watu, unajisikiaje ? Acha upumbavu wako. Hukumu inatolewa na Mahakama wewe kinachokuwasha nini mpuuzi mkubwa wewe. 🖕
Mbona umempunja? Embu muongezee.
 
Back
Top Bottom