Manyanza
Platinum Member
- Nov 4, 2010
- 22,269
- 58,563
TUNDU LISSU ANAMHOJI SHAIDI WAKE JOHN HECHE MAHAKAMANI
SEHEMU YA 17.
Lissu: Shahidi, nimesikia kwamba watu katika kudai mifumo ya uchaguzi wameenda hadi Mahakama za Afrika. Hebu fafanua hapo.
Heche: Waheshimiwa Majaji, kwa uelewa wangu tuna mikataba ya kimataifa na sheria za kimataifa ambazo zinatufunga.
Pamoja na Kesi ya Mtikila, nafahamu pia kuna kesi za Freeman Mbowe, Maalim Seif Hamad na Bob Chacha Wangwe, ambazo zilianzia Mahakama Kuu, Mahakama ya Rufani, baadaye hadi Mahakama ya Afrika.
Kuhusu wasimamizi wa uchaguzi ambao ni wana-CCM kusimamia kwenye uchaguzi wa vyama vingi, wanaleta upendeleo na kuharibu uchaguzi.
Lissu: Waeleze Waheshimiwa Majaji, kwenye mazungumzo yangu na wadau, hilo nilizungumziaje kuhusu matumizi ya nje ya Afrika au ya kikanda?
Heche: Mheshimiwa Tundu Lissu alieleza kwamba kumekuwa na attempts nyingi kuhusiana na watu wetu wengi kujaribu kurekebisha au kuharibu uchaguzi kupitia mfumo wetu wa Mahakama.
Na watawala wamekuwa wakipuuza mfumo wetu wa kimahakama.
Na ndiyo maana wamekuwa wakisema kwamba Mahakamani haendeki.
Ndiyo maana mfumo huu unahitaji kufanyiwa overhaul kisiasa. Umeharibika kiasi kwamba hauwezi kurekebishwa zaidi ya kufanyiwa overhaul ya kisiasa.
Lissu: Waeleze Waheshimiwa Majaji nilizungumza nini na wadau juu ya haja ya kuahirisha uchaguzi wa 2025.
Heche: Alisema kwamba kwa sababu huu uchaguzi una matatizo, unaleta mauaji na hauleti matokeo ambayo wananchi wanayategemea, hasa sisi tulikuwa tupo tayari uchaguzi usogezwe mbele na yafanyike mabadiliko ambayo yangeruhusu kufanyika kwa uchaguzi huru na wa haki.
Kuepusha maafa ambayo yangejitokeza kama chaguzi zingeendeshwa.
WEKA EMOJI KAMA UNASOMA
SHARE ZAIDI UJUMBE UFIKE MBALI