Kesi ya Lissu Septemba 10, 2026: IGP Wambura, DCI Kingai na CDF Mkunda waitwa kutoa ushahidi

Majaji walianza toka jana kuwaweka watu kisaikolojia kuwa sio lazima mashahidi wawe wengi. Na wameshasema kesi ndani ya siku 14 iishe. Wanachomaanisha hata hao mashihidi anaowataka Lisu hawataitwa maana siku zitazidi hizo 14. Pia hao mashahidi anaotaka Lisu waitwe mahakama haiwezi kuwaita.
 
Ivi mkuu mahakama ikiwakataa kisheria inakuwaje ??, na kesi itakuwa na muelekeo upi kisheria
 
TUNDU LISSU ANAMHOJI SHAIDI WAKE JOHN HECHE MAHAKAMANI

SEHEMU YA 9.

Lissu: Waeleze Waheshimiwa Majaji, baada ya hilo shambulio kitu gani kilifuatia?

Heche: Baada ya hilo tukio, Mheshimiwa Tundu Lissu alisafirishwa, ambapo alitibiwa kwa muda mrefu na baadaye Ubelgiji.

Lissu: Waeleze Waheshimiwa Majaji, hizi taarifa za kushambuliwa kwangu, Nairobi kisha Ubelgiji, wewe ulizijuaje?

Heche: Nilizijua kwa sababu nilikuwa naye Bungeni.

Hata hivyo, nilimtembelea Nairobi alipokuwa hospitalini.

Vilevile, aliporudi nyumbani nilizungumza naye.

Lissu: Utaratibu wa matibabu ya Mbunge ndani au nje ya nchi ukoje?

Heche: Mbunge anapopata matatizo ndani ya nchi anatibiwa na bima.

Lakini kama ni nje ya nchi, Ofisi ya Katibu wa Bunge inachukua majukumu ya kulipia matibabu, eneo unalofikia na msaidizi wako mmoja.

Lissu: Waeleze Waheshimiwa Majaji kama utaratibu huo unaosema ulitumika katika matibabu yangu.

Heche: Waheshimiwa Majaji, hakulipiwa matibabu, msaidizi wala eneo alilokuwa amefikia.

Lissu: Waeleze Waheshimiwa Majaji, kwa vile sikutibiwa kwa utaratibu wa Kibunge uliousema, waeleze sasa Waheshimiwa Majaji nilitibiwaje?

Heche: Waheshimiwa Majaji, chama kililipia matibabu.

Michango ya marafiki na TLS pia.

Na pia, hivyo ndiyo ninavyoweza kusema.

Kulikuwa na kuchangiwa na Watanzania na watu wengine Nairobi, ila hasa ni Watanzania.

Lissu: Sasa Shahidi, unasema kipindi hicho nilikuwa Mbunge. Waeleze Waheshimiwa Majaji—

Heche: Waheshimiwa Majaji, Mheshimiwa Tundu Lissu alivuliwa Ubunge.

Lissu: Waeleze Majaji kuhusu Ubunge wangu.

Heche: Alikuwa nje ya nchi kwa matibabu.

Mwaka sikumbuki vizuri.

Ila alivuliwa Ubunge sababu ya utoro.

WEKA EMOJI KAMA UNASOMA

SHARE ZAIDI UJUMBE UFIKE MBALI.
 
Heche hajui tofauti ya Siasa na Sheria. Anapiga siasa Mahakamani 🤣 🤣 🤣
 
Noted
 
TUNDU LISSU ANAMHOJI SHAIDI WAKE JOHN HECHE MAHAKAMANI

SEHEMU YA 10.

Lissu: Ni kiongozi gani, nikiwa hospitalini, alikuja Nairobi?

Heche: Makamu wa Rais Samia alienda Nairobi na baadaye Nairobi Hospital, alipokuwa Tundu Lissu.

Lissu: Waeleze Waheshimiwa Majaji kama Rais Mstaafu Ali Hassan Mwinyi walinitembelea hospitalini nilipokuwa nimelazwa, pamoja na mke wake.

Heche: Hilo nalikumbuka, na lilitangazwa hadharani kuwa Rais Mstaafu Ali Hassan Mwinyi na mkewe walimtembelea Nairobi.

Lissu: Waeleze Waheshimiwa Majaji kama Mawaziri Wakuu Fredrick Sumaye, Joseph Sinde Warioba na Edward Ngoyai Lowassa walinitembelea Nairobi.

Heche: Waheshimiwa Majaji, nina kumbukumbu ya Fredrick Sumaye na Lowassa kumtembelea hospitalini, ila sina kumbukumbu ya Warioba.

Lissu: Una kumbukumbu ya Jaji Mstaafu Othman Chande kunitembelea hospitalini?

Heche: Waheshimiwa Majaji, nina kumbukumbu ya Jaji Mstaafu Othman Chande kumtembelea hospitalini.

Lissu: Waeleze Waheshimiwa Majaji, kwa ufahamu wako, waeleze kama Pindi Chana alinitembelea Nairobi Hospital.

Heche: Waheshimiwa Majaji, nina kumbukumbu kuwa Pindi Chana alimtembelea Nairobi Hospital.

Lissu: Shahidi, nimekuuliza swali hili kwa sababu nataka nikuulize swali hili. Wewe ulienda mara ngapi na umetumia muda gani?

Heche: Waheshimiwa Majaji, nimeenda mara nyingi na, kwa kukadiria muda, nimekaa kama mwezi mmoja na nusu.

WEKA EMOJI KAMA UNASOMA

SHARE ZAIDI UJUMBE UFIKE MBALI.
 
Naona kabisa mahakama ikikataa kuwaita Majaliwa, mpango,IGP, Mh Samia,mkurugenzi wa TISS.
Nipo na Serengeti lite nasubiri hiyo ruling.
Hawawezi kuwaita maana itakuwa aibu kwa taifa. Isitoshe hao ndio waliobumba hiyo kesi kwa ulevi wa madaraka. Mahakama inatazama itachezaje na hiyo hali isionekane haina meno.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…