Kesi ya Lissu: Shahidi wa 18 akwamisha kesi yaahirishwa hadi Agosti 17, 2026

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
5,383
Reaction score
18,776
Kesi ya uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu, imeahirishwa hadi Jumatatu, Agosti 17, 2026, baada ya upande wa Jamhuri kuomba muda zaidi kutokana na changamoto za kiafya alizopata shahidi wa 18 aliyepaswa kuanza kutoa ushahidi leo Ijumaa.

1786696440520.png

Jana, shahidi wa 17 wa upande wa Jamhuri, ambaye utambulisho wake ulihifadhiwa na kutajwa kama ‘P’, alimaliza kutoa ushahidi wake. Miongoni mwa mambo aliyoyaeleza ni namna alivyoshiriki kama mwandishi wa habari katika kuripoti mkutano wa CHADEMA uliofanyika Aprili 3, 2025.

1786696554531.png

Upande wa Jamhuri umeieleza Mahakama kuwa shahidi wa 18 amepata changamoto za kiafya, hivyo kuomba kesi hiyo iahirishwe.

Mahakama Kuu, Masjala Ndogo Dar es Salaam, imekubali ombi hilo na kuahirisha kesi hadi Jumatatu, Agosti 17, 2026.

Upande wa Jamhuri umeahidi kwamba Jumatatu utawaleta mashahidi wote waliobaki ili kuendelea na ushahidi wa upande wa mashtaka.

Kesi ya uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu imeahirishwa mpaka Jumatatu Agosti 17, 2026 baada ya upande wa mashataka ambao ni jamhuri kuomba kesi ihairishwe kwa madai kuwa shahidi wa 18 ambaye alibidi aanze kuhojiwa leo amepata changamoto za kiafya.

Upande wa Jamhuri umeahidi kwamba Jumatatu wataleta mashahidi wao wote waliobaki.
Dunia hii haina haki kabisa.
 
Shahidi amekimbia moto🤣
 
Bwahaaaa bwahaaaaa 🤣🤣 nimecheka kwa nguvu ile mbaya. Juzi nilisema kwa ujumla Lisu alishawshinda toka mwaka jana kwenye hiyo kesi. Hata kuipeleka mahakama ya rufaani ilikuwa ni kuficha aibu ya kushindwa. Na nilisema wameurudisha mahakama kuu lakini kiukweli ni kuwa Lisu kawashinda tayari, na serekali haina pumzi tena

Ukweli ni kuwa mashahidi hawataki tena, hata yule shahidi wa juzi waliyekuwa wanamtegemea aliishia kudhalilika, na yule wa jana alikubali kwa shingo upande kupanda kizimbani. Hakuna kitu kigumu kama kupambana na mtu wa haki. Machawa wote najua watakuwa wanaona aibu na fedheha kwa wakati mmoja.
Tlaatlaah
 
Kesi ya uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu, imeahirishwa hadi Jumatatu, Agosti 17, 2026, baada ya upande wa Jamhuri kuomba muda zaidi kutokana na changamoto za kiafya alizopata shahidi wa 18 aliyepaswa kuanza kutoa ushahidi leo Ijumaa.

Jana, shahidi wa 17 wa upande wa Jamhuri, ambaye utambulisho wake ulihifadhiwa na kutajwa kama ‘P’, alimaliza kutoa ushahidi wake. Miongoni mwa mambo aliyoyaeleza ni namna alivyoshiriki kama mwandishi wa habari katika kuripoti mkutano wa CHADEMA uliofanyika Aprili 3, 2025.

Upande wa Jamhuri umeieleza Mahakama kuwa shahidi wa 18 amepata changamoto za kiafya, hivyo kuomba kesi hiyo iahirishwe.

Mahakama Kuu, Masjala Ndogo Dar es Salaam, imekubali ombi hilo na kuahirisha kesi hadi Jumatatu, Agosti 17, 2026.

Upande wa Jamhuri umeahidi kwamba Jumatatu utawaleta mashahidi wote waliobaki ili kuendelea na ushahidi wa upande wa mashtaka.
Mimi ni shahidi wa 18 bado nakariri matango niliyolishwa pia nitawaomba majaji wamzuie Lissu asinifanyie dodoso.
Mawakili wa serikali wameandaa pingamizi kuomba mahakama ya rufaa itoe katazo la Lissu kujitetea mwenyewe maana huwa anatuvuruga sisi mashahidi.
 
Habari ndiyo hiyo. Majaji wame mute na kukubali ombi hilo. Siwalaumu, hawana the other way out sana sana ni kuhairisha.
Unafikiri wangelifaya nini? Kuifuta? si rahisi kihivyo!

Delaying tactics za serikali...Kenya wangeliweza kuifuta instantly maana wameonywa several times kuleta mashahidi na walipewa amri walete mashahidi wawili kila siku....they do not give a damn....... mtatufanya nini?
 
Back
Top Bottom