Kesi ya Lissu: Shahidi wa 18 akwamisha kesi yaahirishwa hadi Agosti 17, 2026

Kesi ya Lissu: Shahidi wa 18 akwamisha kesi yaahirishwa hadi Agosti 17, 2026

Hii KESI inafika KWELI 2030 kwa style hii ,Hadi hapa naamini HAKI ni ngumu sana Tanzania
Hata ikifika hiyo 2030 bado haitaondoa hii chuki iliyojengwa na hawa wahuni. Wananchi wengi wenye uelewa na pia akili timamu, wanamchukia sana huyu mtawala katili. Hivyo hata afanye nini, chuki dhidi yake haiwezi kuisha.
 
Jamani, nimecheka sana kwa kweli! Nilisema hapa hapa juzi kwamba kwa ujumla, Lisu alishawashinda tangu mwaka jana kwenye kesi hii. Na hata kuipeleka Mahakama ya Rufaa ilionekana kama jaribio la kufunika ukweli wa kushindwa mapema. Nilisema pia kuwa ingawa wameirudisha Mahakama Kuu, ukweli unabaki kuwa Lisu ameshawashinda, na sasa serikali haina tena nguvu ya kuendeleza mbinu zao.

Ukweli ni kwamba, sasa mashahidi wenyewe wanaonekana kutokuwa tayari kutoa ushahidi. Hata yule shahidi waliyekuwa wanamtegemea sana juzi, aliishia kupata aibu na kudhalilika mahakamani. Na yule wa jana, alilazimika kukubali kupanda kizimbani kwa shingo upande tu. Hakika, hakuna jambo gumu kama kupambana na mtu anayesimamia haki. Wale wote waliokuwa wakiunga mkono upande mwingine, nina uhakika wanajisikia aibu na fedheha kwa wakati mmoja.
Tlaatlaah Stuxnet ChoiceVariable mdogoee Mtoto wa Shule Stroke MamaSamia2025
Hatuwezi kusikia aibu hadi Jaji atoe hukumu. Usijidanganye na hivyo viswali vya kukejeli na kukera kutoka kwa mtuhumiwa.
 
Hata ikifika hiyo 2030 bado haitaondoa hii chuki iliyojengwa na hawa wahuni. Wananchi wengi wenye uelewa na pia akili timamu, wanamchukia sana huyu mtawala katili. Hivyo hata afanye nini, chuki dhidi yake haiwezi kuisha.
Itakua kubwa zaidi,kila mtu anaona kuwa jamaa anaonewa anateswa
 
kesi itaendelea wakati mwingine kwasababu za kiafya kwa shahidi wa siku. Unacheka nini kwa mfano kama sio unafiki tu gentleman?

yaani kipi cha ajabu hapo,
au kipi cha kushangaza kwenye jambo la kawaida kama hilo?

unaelewa kuna mambo ikiwa huna uelewa au ufahamu wa kutosha juu yake, na unaendekeza hisia potofu, ni vizuri kukaa kimya tu na itapendeza 🐒
Yaani kesi ya uhaini serikali inashindwa kuwa na mashahidi wa kutosha.Hiyo idara ya usalama imejaa vilaza sana aisee.
 
Kesi ya uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu, imeahirishwa hadi Jumatatu, Agosti 17, 2026, baada ya upande wa Jamhuri kuomba muda zaidi kutokana na changamoto za kiafya alizopata shahidi wa 18 aliyepaswa kuanza kutoa ushahidi leo Ijumaa.

Jana, shahidi wa 17 wa upande wa Jamhuri, ambaye utambulisho wake ulihifadhiwa na kutajwa kama ‘P’, alimaliza kutoa ushahidi wake. Miongoni mwa mambo aliyoyaeleza ni namna alivyoshiriki kama mwandishi wa habari katika kuripoti mkutano wa CHADEMA uliofanyika Aprili 3, 2025.

Upande wa Jamhuri umeieleza Mahakama kuwa shahidi wa 18 amepata changamoto za kiafya, hivyo kuomba kesi hiyo iahirishwe.

Mahakama Kuu, Masjala Ndogo Dar es Salaam, imekubali ombi hilo na kuahirisha kesi hadi Jumatatu, Agosti 17, 2026.

Upande wa Jamhuri umeahidi kwamba Jumatatu utawaleta mashahidi wote waliobaki ili kuendelea na ushahidi wa upande wa mashtaka.

Hii kesi ikiwahi kuisha ni 2030 November
 
14 Agosti 2026
Tundu Lissu mambo yakiwa hivi shahidi wangu Samia Suluhu Hassan ataletwa lini ?
1786713952314.png

14 August 2026

EPISODE 44: TUNDU LISSU LASHES OUT AT JUDGES "IF I ASKED FOR SAMIA TO BE BROUGHT IN, WOULDN'T IT ...

View: https://m.youtube.com/watch?v=ZZnowCfvSUg
EPISODE 44: The treason case against Tundu Lissu has been postponed until 17/8/2026 on Monday after the Republic or the prosecution requested the court to postpone the case because their witness has an emergency. Government lawyers have said that witnesses are also human beings and because they are human beings, challenges can happen to any human being, so they have requested to bring all the remaining witnesses.
 
Yaani kesi ya uhaini serikali inashindwa kuwa na mashahidi wa kutosha.Hiyo idara ya usalama imejaa vilaza sana aisee.
kwahiyo kuna kitu gani kumeshindikana gentleman kwa mfano?🤣
 
Hatuwezi kusikia aibu hadi Jaji atoe hukumu. Usijidanganye na hivyo viswali vya kukejeli na kukera kutoka kwa mtuhumiwa.
Kwa wewe mpaka Sasa umeona ushahidi wowote wa uhaini.
 
kwahiyo kuna kitu gani kumeshindikana gentleman kwa mfano?🤣
Mahakama imewapa amri mawakili wa serikali waje na mashahidi zaidi ya mmoja kila siku ya kesi.Kweli kila siku ni kuomba kuahirisha kisa mashahidi wa kusuasua kwenye kesi ya uhaini.q
 
Mahakama imewapa amri mawakili wa serikali waje na mashahidi zaidi ya mmoja kila siku ya kesi.Kweli kila siku ni kuomba kuahirisha kisa mashahidi wa kusuasua kwenye kesi ya uhaini.q
Gentleman,
ikiwa kwako ushahidi ni bora kuliko afya, basi endelea kuipa kipaumbele iphone new model, huku ukipuuza bima ya afya ya laki1 tu🐒
 
Hatuwezi kusikia aibu hadi Jaji atoe hukumu. Usijidanganye na hivyo viswali vya kukejeli na kukera kutoka kwa mtuhumiwa.
Nakwambia hukumu inaendana na ushahidi, labda hukumu inayoandikwa na rais ndio itakuwa kinyume na ushahidi. Hizo hukumu zinazoendana kinyume na ushahidi ndio zinazosababisha wawekezaji hawako tayari kutumia mahakama zetu za ndani kwa mashauri yako. Hakuna lolote litakalotushangaza iwapo hukumu itaendana na utashi wa rais na sio ushahidi wa mahakamani, maana alitangazwa kupata kura 31m, idadi ambayo haikuendana na wapiga kura vituoni.
 
Hiyo kesi inawaabisha sana walioshtaki aisee shahidi anajibu kama anapelekwa na maji sijui kwa nini hawajifunzi wao kila kukicha ni kudharirika na wanaona poa tu..
 
Back
Top Bottom